WEKUNDU wa Msimbazi Simba
wanaendelea vyema na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania
bara unaotarajia kuanza kushika kasi septemba 30 mwaka huu.
Simba wamepiga kambi visiwani
Zanzibar (Unguja) chini ya kocha mkuu mpya, Mzambia, Patrick Phiri
akisaidiwa na kocha msaidizi, kiungo wa zamani wa klabu hiyo na timu ya
taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ na
kocha wa makipa, Idd Pazzi ‘Father’.
Simba ilianza programu ya mazoezi
mara moja kwa siku hapo jana katika fukwe za bahari ya Hindi, lakini
Phiri ameamua kuongeza dozi ambapo leo atafanya mazoezi mara mbili,
(asubuhi na jioni).
Lengo la Phiri ni kupata muda wa
kutosha wa kusuka kikosi chake akijua wazi kuwa msimu ujao atakumbana na
changamoto kubwa ya kusaka ubingwa wa Tanzania bara.
Pia kocha huyo alisisitiza suala
la mechi za kirafiki ili kukiona kikosi chake kwa mara ya kwanza na
kujua nini cha kufanya zaidi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kocha huyo aliyerejea nchini kwa
mara ya tatu kuifundisha Simba baada ya kutimuliwa kwa Mcroatia, Zdravko
Logarusic ‘Loga’ aliahidi mambo mazuri kwa Simba iliyoshinda kuwika kwa
miaka mitatu mfululizo.
Wakati huo huo, mwenyekiti wa
kamati ya usajili ya Simba, Keptein wa zamani wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe yuko mjini Kigali, nchini Rwanda
kufuatilia michuano ya kombe la Kagame inayoendelea nchini humo.
Uwepo wa Poppe huko Kigali
unatafsiriwa kuwa ni kujaribu kuona vifaa vipya vya kuongeza Msimbazi
ikizingatiwa Shirikisho la soka Tanzania jana limetangaza kuongeza siku
10 zaidi za usajili mpaka Agosti 27 mwaka huu badala ya siku ya mwisho
iliyokuwa jana Agosti 17.
Katika siku hizo zilizoongezwa
mtu makini na mwenye mapenzi makubwa na Simba sc, Hans Poppe anaweza
kuibuka na vifaa vipya hususani wakati huu Kombe la Kagame likifikia
hatua ya robo fainali itakayoanza kutimua vumbi leo hii.
Wakati hayo yakijiri Msimbazi,
nao mahasimu wao, Dar Young Africans wanatarajia kuondoka wiki hii
jijini Dar es salaam kuelekea kisiwani Pemba, Zanzibar ambapo wataweka
kambi ya kujiandaa na ligi kuu Bara.
Yanga sc watakuwa huko chini ya kocha anayesemekana kurudisha morali ya kila mchezaji kwasasa, Mbrazil, Marcio Maximo.
Nao wagosi wa Kaya, Coastal Union wanatarajia kutua Pemba kesho jumanne,.
Kwa maana hiyo, mashabiki wa
Zanzibar watashuhudia timu tatu za ligi kuu soka Tanzania bara zikijivua
katika ardhi yao inayosifika kwa uzalishaji wa zao la Karafuu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Baraka Mpenja
No comments:
Post a Comment