Monday, August 18, 2014

ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME: WANYARWANDA WAANZA KUTIFUANA LEO, AZAM, EL MERREIKH KESHO

AZAM FC
MICHUANO ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame, imefikia patamu mjini Kigali, Rwanda ambapo hatua ya robo fainali inaanza kutimua vumbi leo hii.
Mechi ya kwanza itaanza majira ya 9:00 alasiri kwa kuwakutanisha Polisi dhidi ya Atletico, zote za Rwanda.
Robo fainali ya pili itaanza majira ya saa 11:00 jioni ambapo timu mbili pinzani nchini Rwanda, Rayon Sport na wanajeshi wa APR wataoneshana kazi.
Kibarua kingine kitaendelea kesho ambapo mechi iliyotabiriwa kuwa ngumu zaidi katika hatua hii ya kombe la Kagame itawakutanisha mabingwa wa Tanzania, Azam fc dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
Kutokana na historia nzuri ya El Merreikh katika soka la Afrika mashariki na kati, hakika Azam wametumbukia katika daraja zito, lakini kama watajipanga vizuri wanaweza kuibuka na ushindi.
Meneja wa Azam fc, Jemedari Said alisema wamejiandaa vizuri na wanafurahia kuchuana na timu ngumu ambayo itawapa kipimo kizuri  cha kujua maendeleo ya kikosi chao.
“Sio pambano jepesi, El Merreik ni timu yenye historia kubwa. Sisi kama Azam hatuwaogopi, tunawaheshimu, tutapambana kupata ushindi ili kutinga nusu fainali na hatimaye fainali na kutwaa ubingwa”. Alisema Jemedari.
Jemedari alisema katika mazoezi ya jana jioni, wachezaji wote waliokuwa majeruhi, Waziri Salum ambaye hajacheza mechi yoyote, Saint Prex Lionel, Shomari Salum  Kapombe wote walifanya mazoezi, na kwa mara ya kwanza kikosi kizima kilikuwa uwanjani kujiandaa na mchezo huo.
Mechi nyingine ya kesho jumatano itawakutanisha KCC ya Uganda dhidi ya Altabara ya Sudan Kusini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Baraka Mpenja

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...