Wakati mchakato
wa Katiba mpya unaendelea mjini Dodoma na suala la theluthi mbili
likisumbua vichwa vya wengi, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
ameeleza kuwa kura za wajumbe 14 kutoka Zanzibar ndizo zitauokoa au
kuukwamisha mchakato huo.
Profesa Lipumba alikuwa kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi
nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kuhusu mustakabali wa
mchakato wa Katiba baada ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
kususia kuhudhuria vikao.
Kundi hilo lilisusia vikao Aprili 16 kwa madai
kuwa Bunge lilipoteza mwelekeo kwa kuacha kujadili Rasimu ya Katiba,
hasa katika suala la muundo wa serikali ya Muungano na kwamba chama
tawala, CCM kiliingiza suala la serikali mbili ambalo halimo kwenye
rasimu hiyo badala ya serikali tatu.
Kutokana na uamuzi wa Ukawa, ambayo inaundwa na
wajumbe kutoka CUF, Chadema, NCCR Mageuzi na baadhi wa kundi la 201
kutoka taasisi mbalimbali za kijamii, kuna shaka kwamba mchakato huo
huenda usifanikiwe kutokana na ukweli kuwa Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba inataka uamuzi upitishwe na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Bara
na idadi kama hiyo kutoka Zanzibar. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kutokana na utashi huo wa kisheria, Profesa
Lipumba alisema wana uhakika kuwa Katiba haitapita kwa kuwa wanao
wajumbe 14 kutoka kundi la 201 ambao ndiyo tegemeo lao.
“Sisi tunao wabunge na wawakilishi kutoka Zanzibar
wa vyama vyetu ambao hawakwenda hata kwenye vikao. Tukiwajumlisha,
tunahitaji watu 14 kutokana na wale wajumbe 77 (wa Zanzibar) wa Kundi la
201 na kule tuna uhakika wa watu kama 21,” alisema.
“Wapo baadhi waliokwenda kuhudhuria vikao, lakini
tunajua misimamo yao. Tunajua kuna mbinu zinafanyika kuwarubuni, lakini
tunawafuatilia kwa karibu.”
Alisema kuwa Ukawa wana uhakika pia wa kuungwa
mkono na wabunge na wawakilishi wa CCM kutoka Zanzibar katika kutetea
mamlaka ya Zanzibar.
“Kama mnafuatilia mazungumzo ya Baraza la
Wawakilishi, katika malalamiko ya suala la Muungano, mazungumzo ya CUF
na CCM yalikuwa yanafanana na hata ule waraka uliopelekwa bungeni kutoka
CCM Zanzibar ambao sasa wanaukana, unataka mamlaka tatu. Maana yake
nini? Mamlaka ni Serikali,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza:
“Hata kura zitakapopigwa, CCM hawawezi kupata theluthi mbili za upande wa Zanzibar. Suala la Katiba ni suala la maridhiano.”
Aitetea Tume ya Jaji Warioba
Huku akitetea uamuzi wa Ukawa kutoka nje ya Bunge
la Katiba, Profesa Lipumba ametaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja
na rasimu iheshimiwe kwa kuwa imefanya kazi kubwa.
Utata Bunge la Katiba, NEC
“Pamoja na kwamba kila kundi lilikuwa na mambo yake katika
Katiba, yale mambo ya msingi yaliyoletwa na Jaji (mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Joseph)Warioba na Tume yake tuyasimamie na
yaongoze mchakato wa Katiba. Ukiisoma rasimu ile kwa kweli utaona Tume
hiyo imefanya kazi kubwa,” alisema Profesa Lipumba.
Amewataja makamishna wa iliyokuwa Tume hiyo ya
Mabadiliko ya Katiba akisema kuwa utaalamu wao ndiyo umezingatia umuhimu
wa muundo wa serikali tatu.
“Kati ya wataalamu waliobobea katika Katiba ni
pamoja na marehemu Dk Sengondo Mvungi na Profesa Palamagamba Kabudi.
Siyo Profesa Issa Shivji (namheshimu sana huyo, kwani ameandika mengi
kuhusu Zanzibar kwamba imebanwa sana),” alisema.
“Lakini, utaalamu wa Profesa Shivji ni sheria za
kazi. Ni msomi mwenye uelewa mpana… lakini wanafunzi wake ni wataalamu
wa masuala ya Katiba ambao ni Dk Mvungi na Profesa Kabudi ndiyo wameona
hivyo.
“Hawa ni wazalendo. Huwezi ukahoji uzalendo wa
Jaji Warioba, Jaji Augustino Ramadhani, Joseph Butiku, Dk Salim Ahmed
Salim na wengineo.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Utata Bunge la Katiba, NEC
Lipumba amesisitiza kuwa hata Bunge hilo
likiendelea na vikao vyake, bado Katiba ya wananchi haitapatikana kwani
haitakuwa na maridhiano ya kisiasa.
“Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar
Bakari hayumo katika Bunge Maalumu, unajadili vipi Katiba? Huwezi kupata
Katiba bila maridhiano ya kisiasa ya Wazanzibari, hakuna maridhiano ya
kisiasa. Kwa hiyo, tunataka mchakato usitishwe,” alisema.
Kwa upande mwingine, Profesa Lipumba alisema kuna
mikanganyiko mingi katika Bunge hilo pia kukiwa na utata wa kufanyika
kwa kura ya maoni kutokana na maandalizi hafifu ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC).
“Tume ya Uchaguzi ilivyo sasa, hata Daftari la
Wapigakura wanasema hawana, wameshafuta vitambulisho vya kupigia kura.
Wanasema wataliandaa ifikapo Septemba wakati hadi tufikie kwenye
Uchaguzi Mkuu 2015 tuna mwaka mmoja,” alisema.
Aliongeza: “Halafu wanachanganya mambo, leo
utasikia mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta anakutana na
jamii ya wafugaji. Kwamba wafugaji hawamo kwenye rasimu?
“Tunafahamu Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeeleza
katika ripoti zao kwamba mambo hayo yote walikuwa nayo, lakini
hawakuyaweka kwa kuwa hii ni Katiba ya Muungano.
Rais Kikwete msahaulifu
“Mambo ya ardhi, serikali za mitaa hayakuwekwa. Sasa, utaletaje
mambo ya Tanzania Bara yaamuliwe na Wazanzibari wakati wana Katiba yao?
Hata ile mantiki iko wazi tu,” alisema Profesa Lipumba.
Rais Kikwete msahaulifu
Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema
Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kusimamia ahadi zake, hali inayochangia
kupwaya kwa utawala wake.
Akifafanua hoja yake, mwanasiasa hiyo alisema,
“Katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka 2011 ambapo pia alianzisha
mchakato wa Katiba, alisema kutakuwa na kituo cha kufua umeme cha
megawati 300, kutakuwa na Kinyerezi (I) ya megawati 200, megawati
nyingine 200 za makaa ya mawe na uzalishaji wa umeme kwa upepo.
“Hadi sasa imeshapita miezi 36, hakuna hata kimoja
alichomaliza kukitekeleza, kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi (I)
kinaendelea kujengwa.”
“Kwa jumla, Kikwete ameshapoteza dira ya
maendeleo kwa kipindi cha miaka tisa alichokaa madarakani, hivyo sioni
cha kumshauri. Alisema tangu Kikwete aingie madarakani, hakuwa na ajenda
maalumu ya maendeleo, ndiyo maana nchi imeendelea kuwa maskini.
“Kwa sasa, Rais Kikwete amebakiza muda wa mwaka
mmoja, hakuna la kutegemea. Kwanza, hakuwa na mtazamo au dira ya
kufanikisha mambo, kwa hiyo kwa mwaka huu mmoja huwezi kutegemea kuwa
ataleta mabadiliko makubwa,” alisema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba, akirejea utawala wa kiongozi wa
serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alisema kuwa utawala wa
Kikwete umeshindwa kuwa na nidhamu ya fedha kiasi cha kuzorotesha
uchumi.
“Ili uweze kusimamia maendeleo ya nchi yetu, ni
lazima uwe na matumizi mazuri ya fedha za umma na uwe na Serikali
inayosimamia vizuri matumizi na malengo yaliyowekwa,” alisema msomi huyo
wa nyanja ya uchumi.
“Rais Mkapa alikuwa na nidhamu ya utendaji wa
Serikali kibajeti, kwa sababu alikuwa akitumia bajeti ya fedha taslimu.
Ilitumika kuleta nidhamu kwa kuwa fedha zilizokuwapo, ndizo
zilizotumiwa.
“Tatizo kubwa ambalo limejitokeza katika kipindi
hiki… Bajeti kwa ujumla wake, ule mgawanyo wa kila wizara haukuwa na
mwongozo mzuri wa nini Serikali itatekeleza. Tatizo hilo lilikuwa ni
muhimu kwa awamu ya mwanzo kuleta nidhamu katika matumizi ya ujumla
yalingane na mapato, lakini hilo jambo limeendelea mpaka leo.”
Kuondokana na umaskini
Na Mwananchi
Ili kuondokana na umaskini nchini, Profesa Lipumba alishauri
Serikali kukubali kuwekeza katika huduma za jamii, zikiwamo elimu na
afya huku rasilimali nyingine zikifuata.
“Ukizungumzia mambo ya afya katika hotuba, si
jambo utakalopigiwa makofi, lakini ndilo jambo linalosababisha umaskini,
yaani watoto na kinamama kukosa lishe bora.
“Kwa takwimu za sasa, asilimia 42 ya watoto wa
Tanzania wana utapiamlo, wamedumaa. Kwenye ‘Big Result Now’ (Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa), sekta ya afya haimo, nimebaki nastaajabu,”
alisema.
Huku akitaja utajiri wa dhahabu kama mojawapo ya
rasilimali zilizopo nchini, alisema Serikali haiko wazi katika mapato
yake, badala yake imejikita zaidi katika kodi ya bidhaa ndogo ndogo.
“Tumejaliwa kuwa na rasilimali za asili. Tuna
dhahabu, lakini ukisikiliza hotuba ya bajeti kila mwaka huwezi kusikia
wakizungumzia tumepata kiasi gani katika sekta ya madini. Tunarudi kule
kwenye sigara na bia na konyagi,” alisema.
“Tumegundua gesi, lakini hatuna mikakati inayoeleweka,” alisema.
. Kuna gesi imegunduliwa katika maji mafupi ndiyo
hiyo ya Msimbati, Mnazi Bay na Songosongo iliyoko kusini mwa Tanzania
ambayo ilitakiwa itumike kuzalisha megawati 300 za kuingiza gridi ya
Taifa, lakini haikufanyika.”
“Sasa kuna gesi ya kina kirefu... lakini
ukiangalia mkataba wa mfano ulioko kwenye tovuti ya TPDC, unasema
Serikali itakuwa inapata asilimia 80 hadi 90. Lakini, mkataba halisi
uliotolewa na (kampuni ya utafiti na uchimbaji mafuta) Statoil,
unaonyesha kuwa Serikali itapata chini ya asilimia 50, hatuna uwazi
katika mapato ya gesi,” alisema.
Aliongeza kuwa licha ya Kampuni za China kujenga
bomba la gesi, bado hata mikataba yake haiko wazi hata kwa wabunge ili
waweze kuhoji.
Aliitaka Serikali kuweka mikakati endelevu ya
kufaidika na gesi ikiwa pamoja na kuihakiki ili kuhakikisha kuwa ina
faida kwa Watanzania. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment