Rashid Mvungi akimuangalia mtoto wake Nasrah Rashid (4) ambaye ni
mlemavu wa viungo aliyefungiwa chumbani na kufichwa kwenye boksi bila ya
kufanyiwa usafi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.
Morogoro. Zimeibuka taarifa
kwamba mtoto aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka minne na mama
yake mkubwa, Nasra Rashid (4) alikuwa na kaka aliyefahamika kwa jina la
Nasoro ambaye hadi sasa hajulikani mahali halipo.
Wakati polisi ikisema imefurahi kupata taarifa
hizo na kwamba itazifanyia kazi, habari zilizopatikana jana kuhusu hali
ya Nasra zimesema atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake.
Vipimo vya awali, vimebaini kuwa amevunjika mifupa ya mikono na miguu na
kwamba atapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kuhusu kaka yake, baadhi ya majirani wa nyumba
aliyokuwa anaishi mama mzazi wa Nasra enzi za uhai wake walidai kuwa
Mariamu alikabidhiwa watoto wawili kuwalea baada ya mama yao kufariki
dunia.
Mmoja wa majirani hao, Ramadhani Mansuri alisema
wakati mama mzazi wa Nasra akiishi eneo la Mjimpya alikuwa na watoto
wawili akiwamo Nasoro ambaye aliachwa akiwa na umri kati ya miaka 14-15.
Vipimo
Ofisa Ustawi wa Jamii, Mkoa wa Morogoro, Oswin
Ngungamtitu alisema taarifa alizopata kutoka kwa madaktari zinasema kuwa
mtoto huyo atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake.
Akizungumzia matokeo ya vipimo vya awali, Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya alisema
haijafahamika sababu za kuvunjika kwa mifupa hiyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz