Friday, May 23, 2014

KAKA WA MTOTO ALIYEFUNGIWA KWENYE BOKSI NAYE 'APOTEA'

 Rashid Mvungi  akimuangalia mtoto wake Nasrah Rashid (4) ambaye ni mlemavu wa viungo aliyefungiwa chumbani na kufichwa kwenye boksi bila ya kufanyiwa usafi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.  

Morogoro. Zimeibuka taarifa kwamba mtoto aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka minne na mama yake mkubwa, Nasra Rashid (4) alikuwa na kaka aliyefahamika kwa jina la Nasoro ambaye hadi sasa hajulikani mahali halipo.

Wakati polisi ikisema imefurahi kupata taarifa hizo na kwamba itazifanyia kazi, habari zilizopatikana jana kuhusu hali ya Nasra zimesema atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake. Vipimo vya awali, vimebaini kuwa amevunjika mifupa ya mikono na miguu na kwamba atapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kuhusu kaka yake, baadhi ya majirani wa nyumba aliyokuwa anaishi mama mzazi wa Nasra enzi za uhai wake walidai kuwa Mariamu alikabidhiwa watoto wawili kuwalea baada ya mama yao kufariki dunia.

Mmoja wa majirani hao, Ramadhani Mansuri alisema wakati mama mzazi wa Nasra akiishi eneo la Mjimpya alikuwa na watoto wawili akiwamo Nasoro ambaye aliachwa akiwa na umri kati ya miaka 14-15.

Vipimo

Ofisa Ustawi wa Jamii, Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu alisema taarifa alizopata kutoka kwa madaktari zinasema kuwa mtoto huyo atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake.

Akizungumzia matokeo ya vipimo vya awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya alisema haijafahamika sababu za kuvunjika kwa mifupa hiyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Dk Lyamuya alisema jana kwamba, mtoto huyo ameshafanyiwa vipimo vingine kadhaa ambavyo vinaonyesha kwamba anasumbuliwa na homa ya mapafu (pneumonia) na utapiamlo unatokana na kukosa lishe bora.

“Tulilazimika kumfanyia vipimo hivyo vya awali kwa sababu alikuwa anaonekana kama anayeugulia maumivu, kwa hiyo vipimo vingine vitaendelea kufanywa kadri tutakavyoona inahitajika,” alisema Dk Lyamuya.

Alisema kipimo cha X- Ray ndicho kilichoonyesha kuvunjika kwa mifupa yake ya miguu na mikono na kwamba hali hiyo ndiyo inayosababisha ashindwe kusimama na kutembea.

“Wakati anafikishwa hapa hospitalini alikuwa amebanwa na kifua na alikuwa anashindwa kupumua vizuri. Ilitulazimu kumwekea mashine ya oksijeni ili imsaidie kupumua, lakini sasa hali yake inaendelea vizuri na tayari tumeondoa mashine, anaendelea na matibabu mengine,” alisema.

Mbali na tiba, Nasra pia alifanyiwa usafi wa mwili wake ambao ulikuwa mchafu kutokana na kutoogeshwa kwa muda mrefu na sasa inaelezwa kuwa yuko kwenye hali ya kuridhisha na wasamaria wema wameanza kujitokeza kumpa misaada ya nguo na chakula.


Mjomba wa Nasra
Akizungumzia tukio hilo, Kaka wa Mariam, Mohamed Said alisema baada ya dada yake kufariki dunia, Nasra alianza kulelewa na mama yake mkubwa kutokana na baba yake mzazi kushindwa kutoa ushirikiano.
“Mimi hali yangu ya maisha ni ngumu sana nisingeweza kumlea Nasra kwa hiyo dada (Mariamu), aliamua kumchukua amlee na naamini alikuwa akimhudumia kwa kumpa chakula na mahitaji mengine, lakini cha kushangaza juzi napata taarifa kuwa amekamatwa kwa kosa la kumfanyia vitendo vya kikatili mtoto Nasra,” alisema Said. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Said alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito mdogo na afya yake ilianza kudhoofika wakati mama yake alipokuwa mgonjwa na baada ya kufariki dunia, viungo vya Nasra vilionekana kulegea na kushindwa kutembea na kusimama.
“Kabla ya kifo cha mama yake, Nasra aliumwa sana, lakini dada Mariamu alimlea vizuri na baada ya kugundua kuwa na ulemavu alijitahidi kumfanyisha mazoezi ya kumsimamisha lakini mtoto mwenyewe alikuwa anagoma, alipolazimishwa alikuwa analia sana, hivyo alikuwa anakaa tu mahali pamoja na kujisaidia haja ndogo na kubwa hapohapo,” alisema Said.
Alisema taarifa kwamba Nasra alikuwa akiishi kwenye boksi na kuteswa, si za kweli kwani licha ya kumlea, Nasra dada yao alishawahi kuwalea watoto wengine wa ndugu zao bila ya kuwafanyia vitendo vya aina hiyo.
Alisema familia haitaweza tena kumlea mtoto huyo, kwani imepatwa na hofu ya kupata lawama kama aliyoipata dada yake, hivyo wanaiachia Serikali kumlea mtoto huyo au baba yake ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Kuhusu malezi, Ngungamtitu alisema: “Tumeongea na Rashid Mvungi ambaye ni baba mzazi wa Nasra na yeye amesema itakuwa vigumu kumchukua kwenda kumlea kwa sababu alimzaa nje ya ndoa na hakuwahi kumwambia mke wake mpaka tukio hilo lilivyotokea. Hatuwezi kumlazimisha.”
Uchunguzi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na kwamba jeshi hilo limefunga chumba cha mtuhumiwa kwa ajili ya usalama na kuepuka kuharibika kwa ushahidi wa mazingira.
Alisema jeshi lake litashirikiana na Ofisi ya Ustawi wa Jamii kuhakikisha kuwa Nasra anakuwa salama hospitalini na kwingineko atakakopelekwa kwa sababu mbalimbali.
Nasra aligundulika akiwa amewekwa katika boksi nyumbani kwa mama yake mkubwa, Mariamu Said, mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro aliyekuwa akimlea. Hivi sasa, Mariam pamoja na mumewe, Omar Mtonga wanashikiliwa na polisi kwa kumficha mtoto wa huyo kwenye boksi kwa miaka minne. Mama yake Nasra alifariki wakati mwanaye huyo akiwa na umri wa miezi tisa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...