Friday, May 23, 2014

BOKO HARAM NI MAGAIDI WA KIMATAIFA - UN


Baraza la Usalama la UN
Baraza la usalama la umoja wa mataifa hatimaye limeidhinisha kuwekewa vikwazo kundi la Boko Haram baada ya utekaji nyara wa takriban wasichana 300 wa shule katika eneo la Chibok Nigeria.
Kundi hilo limeshutumiwa kuwaua maelfu ya watu nchini Nigeria katika miaka michache iliyopita.
Nigeria ni mwanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa kipindi cha miaka miwili. Kwa nafasi hii imeweza kushinikiza baraza hilo kuimulikia tochi.
Hatua ya baraza hilo kuiorodhesha Boko Haram miongoni mwa magaidi wa kimataifa, wakipishana au hata kuhusishwa moja kwa moja na AL Qaeda, huenda isionekane kama hatua kubwa. Lakini hii ina maana kuwa sasa jamii ya kimataifa italichukulia kwa uzito mkubwa zaidi kundi hilo.
Baraza hilo limeidhinisha pia vikwazo kuwekewa kundi hilo, viongozi wake na yeyote anayehusishwa nalo. Hii ina maana kuwa hata mali zao zitazuiliwa na akaunti zao zote zinazojulikana kufungwa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power amepongeza hatua hiyo akisema kuwa itaimarisha vita vya serikali ya Nigeria dhidi ya Kundi hilo, ambalo limetikisa jamii ya kimataifa mwezi uliopita kwa kuwateka zaidi ya wasichana mia mbili wa shule.
Kwa upande wake mjumbe wa Australia katika baraza hilo balozi Gary Quinlan amesema kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa Boko Haram wamepewa mafunzo na kundi la Al Qaeda hasa namna ya kujitengenezea mabomu, mtindo ambao umekuwa mbinu mpya zaidi ya ugaidi.

Abubakar Shekau wa Boko Haram
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau amenukuliwa katika mtandao akitoa matamshi ya kuunga mkono AL Qaeda nchiuni Afghanistan, Yemen na Somalia.
Kabla ya kujumuishwa Boko Haram katika orodha ya Al Qaeda, kulikuweko makundi 62 kote duniani waliowekewa vikwazo kuhusika na Ugaidi, na watu binafsi 162, ambao wamewekewa vikwazo vya usafiri na mali zao kutwaliwa.
Shughuli za Boko Haram katika miaka 5 iliyopita zimesababisha vifo vya maelfu ya waislamu na wakristu wakiwemo watu 1500 waliouawa mwaka huu pekee.
Jina la Boko Haram lina maanisha masomo ya magharibi ni Haram na kundi hilo limetumia nembo hiyo kuendeleza mashambulio yao na chuki dhidi ya chochote kinachhusishwa na nchi za magharibi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...