Wednesday, May 21, 2014

VIFO VYA BOMU NIGERIA VYAFIKIA 118

Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos.
Mabomu mawili yalilipuka mojawepo ikiwa imefichwa ndani ya gari na kulipuka katika soko moja kubwa. Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea karibu na hospitali.
Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo.
Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini wengi wanaamini kuwa Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram lilihusika.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amejitokeza kukemea mashambulio hayo na kusema kuwa amejitolea kuangamiza kabisa ugaidi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...