Monday, May 19, 2014

VAN GAAL AMTEUA VAN PERSIE KUWA NAHODHA MPYA MAN UNITED

Double Dutch: Louis van Gaal (right) sees Robin van Persie as his perfect captain at Manchester United
 Waholanzi wawili: Louis van Gaal (kulia) anaona Robin van Persie ndiye nahodha aliyekamilika katika klabu ya Manchester United.
LOUIS van Gaal  anatarajia kumteua mshambuliaji wake hatari Robin van Persie kuwa nahodha wa kikosi chake mara atakapojiunga na Manchester United baada ya kumalizika kwa kombe la dunia majira ya kiangazi nchini Brazil.
Jumamosi iliyopita Van Persia aliifungia bao muhimu timu ya taifa ya Uholanzi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador na kulazmisha sare ya 1-1.
Van Gaal amekuwa na mahusiano mazuri na RVP ambaye ni nahodha wa timu ya taifa na sasa anatarajia kumpa jukumu hilo katika klabu ya Man United na kumpiga chini Rooney ambaye angekuwa nahodha wa kudumu katika utawala wa David Moyes.
A sign of things to come? Van Persie (right) poses with Kluivert (left), Louis van Gaal's assistant manager
Class: Holland captain van Persie scored a fantastic volley in their 1-1 draw with Ecuador on Saturday
  Van Persie alikuwa na majeruhi kwa muda wa wiki sita za mwishoni mwa msimu mbovu wa Man United baada ya kuumia goti katika mechi ya UEFA dhidi ya Olympiacos mwezi machi mwaka huu.
‘Hata kama ametokea katika majeruhi, alifunga bao la maajabu, bao ambalo huwezi kuamini, ni bao zuri mno,’ alisema  Van Gaal baada ya mshambuliaji huyo kusawazisha dakika ya 37 katika uwanja wa  Amsterdam ArenA jumamosi.
Kwa mujibu wa Van Gaal, kwa asimilia 100, Van Persie hayuko fiti lakini alionekana kuwa imara na kuitendea haki pasi ya Feyenoord na kufunga bao muhimu.
‘Nilifurahishwa na kiwango chake, pia ni nahodha wa aina yake,” Alisema Van Gaal. “Nadhani unampa mchezaji unahodha kama mna morali na falsafa inayofanana”.
“Sio tu mambo ya uwanjani na kiwango cha mchezaji, hata maisha ya kawaida tu”.
“Naamini hilo ni muhimu sana. Naamini Van Persie na Van Gaal tuna falsafa moja”. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...