Uongozi wa klabu ya Young Africans SC
umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu
mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana
Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa
matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza
la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
Hatua ya Young Africans SC kusitisha
huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya
kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo
mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja
mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo
wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho
kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza
chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata
ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30,
Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au
kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.