Dar es Salaam. Mkurugenzi wa zamani wa
Utawala na Utumishi (DPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba
anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na simu gerezani, ameiomba mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imfutie shtaka hilo na kumuachia huru kwa madai kuwa
kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kumkomoa.
Liyumba aliyaeleza hayo jana wakati
akijitete mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando anayetarajia kutoa
hukumu ya kesi hiyo, Januari 15, mwaka na kuzitaka pande zote mbili
kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho kama mshtakiwa ana hatia ama la,
Desemba 30, mwaka huu.
"Kesi hii imepangwa kwa ajili ya
kunikomoa, wakati natumikia kifungo sijawahi kuvunja sheria, kupewa
adhabu wala kuonywa kwa kosa lolote, simu yenye namba 0653004662 siijui
nimeiona hapa na kama imesajiliwa ni lazima mhusika atajulikana."
alieleza Liyumba.
Alidai kuwa, Julai 2011 alikuwa
mfungwa akitumikia kifungo cha miaka miwili na unapofikishwa huko ni
lazima upekuliwe mara tatu kwa kuvuliwa nguo zote.