Thursday, December 12, 2013

BASI LA BURUDANI LAPATA AJALI LEO HII MKOANI TANGA, WATU 12 WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA




Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.

Basi la Burudani leo limepata ajali kijiji cha Kwaluguru Kata ya Kwedizinga  wilayani Handeni, Imeripotiwa mpaka sasa watu zaidi ya 12 wamefariki na majeruhi zaidi ya 55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.

Hospitali ya wilaya ya Korogwe.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo ( kushoto) akiangalia mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu.

Manesi wakiendelea na matibabu kwa majeruhi.

Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa kwenye benchi.

Wananchi wakiwa eneo la Hospitali.
 DC wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo akiwa Hospitalini hapo kutoa Huduma kwa Majeruhi.
Wananchi wa Korogwe wakiwa nje ya Hospitali hiyo ya Wilaya ya Korogwe.
 
Basi  lenye namba za usajili T 610 ATR aina ya Nissan la kampuni ya Burudani ambalo  limepata ajali  leo

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...