Monday, December 16, 2013

"KATIBA MPYA 2014 HAIWEZEKANI" LIPUMBA


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba (pichani) amesema mchakato wa Katiba Mpya una vikwazo vingi na kwamba Katiba haiwezi kupatikana mwaka 2014 kama Rais Kikwete alivyoahidi hivyo, kuna haja ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Bara.
              Hii ni mara ya pili kwa Lipumba kutoa kauli hiyo. Mei mwaka huu, alitoa tamko kama hilo alipoonyesha wasiwasi wake kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya akadai ni janja ya CCM kumwongezea muda Rais.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Lipumba alisema kuwa amekuwa akiutafakari kwa kina mchakato wa Katiba Mpya kama unaweza kukamilika mwaka 2014, lakini jibu linalomjia, hakuna.
Alitaja baadhi ya vikwazo ambavyo vinaweza kukwamisha kupatikana kwa Katiba Mpya kuwa ni Daftari la Kudumu la Wapigakura kama halijaboreshwa na kasi ndogo ya utoaji wa vitambulisho vya utaifa ambavyo vitatumika kupigia kura hiyo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...