Msemaji rasmi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood amekamatwa nchini Misri. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali
Gehad al-Haddad alikamatwa akiwa na mwanachama mwingine mmoja wa vuguvugu hilo katika nyumba moja mjini Cairo.
Taarifa zinazohusianaMisri
Bwana Haddad aliwahi kuhudumu kama afisa wa ngazi ya juu wa naibu mkuu wa majeshi, Khairat al-Shater, wa vuguvugu hilo na kawaida alizungumza na vyombo vya habari vya kigeni.
Bwana Haddad aliwahi kuhudumu kama afisa wa ngazi ya juu wa naibu mkuu wa majeshi, Khairat al-Shater, wa vuguvugu hilo na kawaida alizungumza na vyombo vya habari vya kigeni.
Serikali ya Misri imekuwa ikifanya
msako dhidi ya makundi ya kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani
aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi Julai.
Awali, mahakama ya uhalifu mjini
Cairo, iliamua kuwa mali zote za viongozi wa vuguguvu hilo pamoja na
lile la Gamaa Islamiya kupigwa tanji.
Viongozi wa mashtaka waliwaekea
vikwazo maafisa wa ngazi ya juu wa Brotherhood akiwemo, Mohammed Badie,
Shater na wengine wengi mnamo mwezi Julai.
Wengi wao wamezuiliwa kuhusiana na madai ya kuchochea ghasia na mauaji.
Mamia ya watu wanataka Bwana Morsi kurejeshwa mamlakani , wengi wakiwa wanachama wa Brotherhood .
Aidha makabiliano yaliyotokea mwezi
jana kati na polisi na wafuasi wa Morsi yalisababisha vifo vya wanachama
wengi pale polisi walipovamia kambi zao mbili walipokuwa wanataka Morsi
kurejehswa mamlakani. Chanzo: bbcswahili