Wednesday, September 18, 2013

RPF CHAIBUKA NA USHINDI NCHINI RWANDA

zkagame_32c2c.jpg
Chama tawala nchini Rwanda, RPF kimeibuka mshindi katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika Jumatatu.
Chama hicho chake Rais Paul Kagame kimeshinda uchaguzi huo kwa asilimia 76 ya kura zote zilizopigwa .
Aidha chama hicho kiliingia mamlakani baada ya mauaji ya kimbari yaliyofanyika mwaka 1994 na kimepata viti 40 kati ya 53 vilivyokuwa vinawaniwa.


Chama cha upinzani, FDU-Inkingi, ambacho kiongozi wakeVictoire Ingabire yuko jela, hakikushiriki uchaguzi huo kwani hakijasajiliwa rasmi.
Vyama vingine viwili vya kisiasa vinavyosemekana kuwa washirika wa RPF, vilipata asilimia 13 na asilimia tisa ya kura.
Shughuli ya kupiga kura ilifanyika siku mbili baada ya vifo vya watu wawili kutokana na shambulio la maguruneti mjini Kigali.
Hakuna aliyejitokeza kuhusika na mashambulizi hayo, lakini maafisa wa usalama wanawalaumu waasi wa (FDLR),wanaolaumiwa kwa kuhusika na mauaji ya mwaka 1994 pamoja na wakosoaji wa serikali wanaoishi uhamishoni.
Chama cha (RPF) kimepongezwa kwa kudumisha uthabiti na kukuza uchumi tangu mauaji ya kimbari yaliosababisha vifo vya watu 800,000 wengi wao watu wa kabila la Tutsi na wahutu wenye msimamo wa kadri.
Lakini Rais Kagame amekuwa akituhumiwa kwa kupuuza haki za binadamu na kukandamiza upinzani.
RPF kitaendelea kuwa na ushawishi bungeni ingawa kimepoteza viti viwili katika uchaguzi huu.
Chama kingine cha upinzani ambacho kilishiriki kwenye uchaguzi huu PS-Imberakuri, hakikushinda kiti chochote.
Maafisa wa chama waliambia BBC kuwa wafuasi wao walitishwa wakati wa kampeini , madai ambayo chama tawala kimeyakanusha.
Rwanda ndiyo nchi pekee duniani ambayo wanawake ndio wengi bungeni.
Bunge lina viti 80, kati ya viti hivi 24 ni vya wanwake, viwili vya vijana na kimoja cha mwakilishi wa walemavu.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...