Marcel
ambaye ni mume wa mtu, alifunguliwa kesi namba 29/2013 katika Mahakama
ya Mwanzo ya Bashneti mkoani Babati kwa kosa la kuiingilia kimwili
mifugo, kinyume na kifungu cha 325 kanuni ya adhabu, sura ya 16 na kesi
hiyo ilisomwa hivi karibuni.
Mshitakiwa
aliwekewa dhamana lakini siku chache baadaye kesi ilipotakiwa
kuendelea, hakuonekana na imebainika mahakamani hapo kuwa ametoroka.
Kesi
hiyo ipo mbele ya Hakimu Julius Dagharo wa mahakama hiyo na
aliyethibitisha mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa ametoroka ni Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Bashneti, Omari Mwanditi.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki iliyopita, mmiliki wa mbuzi anayedaiwa kuingiliwa,
Clementina Masay alidai kuwa mtuhumiwa huyo amemsababishia hasara kwani
mbuzi wake alikuwa na mimba lakini baada ya kitendo hicho, imeharibika.
Jamii
ya wafugaji wa Kiiraq wa eneo hilo wamesikitishwa na kitendo cha
mtuhumiwa kudaiwa kuiingilia mifugo yao kimwili mara kwa mara na
wameahidi kumsaka hadi wamkamate.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Babati, ACP Akili Mpwapwa amekiri
kutokea kwa tukio hilo na ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa
wakimuona mtuhumiwa huyo ili afikishwe mahakamani.
AMA
kweli dunia imekwisha kwani mtu mmoja, Daniel Marcel (27), mkazi wa
Kijiji cha Madunga, wilayani Babati, Manyara, amekamatwa na kufikishwa
mahakamani kwa madai ya kufanya mapenzi.