Tuesday, November 11, 2014

MKE ANAYEISHI NA WAUME WAWILI MAPYA YAIBUKA


Sakata la mke kuishi na waume wawili  limechukua sura mpya baada ya kikao cha ndugu wa mume halali, Rogers Halinga kuketi kikao katika Kijiji cha Ishungu, Kata ya Ruiwa Mbarali, mkoani Mbeya na kumtaka Biton Mwashilindi kufanya mazungumzo nao kabla hawajafungua madai ya ugoni mahakamani na kudai fidia.
Rogers Halinga akiwa na baba yake mzee Jason Halinga na mtoto anayedaiwa kugombaniwa.
Kikao hicho kizito kilichofanyika nyumbani kwa baba mzazi wa Rogers, mzee Jason Halinga (95), Novemba mosi mwaka huu na kuhudhuriwa na ndugu lukuki nia ilikuwa kumsikiza mke wa Rogers, Juliana (22)  ili abainishe ukweli juu ya mtoto aliyezua utata kuwa ni wa nani baina ya mumewe (Rogers) na Biton Mwashilindi. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Mwanamke huyo  akijikanganya mara kadhaa katika kikao hicho akidai mtoto huyo ni wa Rogers, kwani aliondoka baada ya kutokea mabishano na mumewe akiwa na ujauzito wa miezi minne ndipo alipoanza mahusiano ya kimapenzi na Biton hadi siku anajifungua mwaka 2012 akiwa mikononi mwa Biton na aliamua kumwandikisha mtoto katika kadi ya kliniki kuwa baba yake ni Biton.
...Ndugu wakiwa kwenye kikao.
Kutokana na kauli hiyo, ndugu wa Rogers walikuja juu na kumtaka Juliana atamke wazi mtoto ni wa nani ndipo alijibu kuwa mtoto ni wa Biton Mwashilindi, ambapo alimkabidhi mtoto huyo mwishoni mwa Oktoba kwa hiari yake na wala hakuporwa kama alivyotoa taarifa polisi.
Kauli hiyo ya Juliana iliwafanya ndugu wa mume kupiga simu kwa mzazi wa Juliana anayeishi Lwanjilo wilayani Chunya kujua mustakabali wa kauli ya mtoto wao kwani ilidaiwa kuwa Biton aliwahi kwenda huko kujitambulisha kuwa yeye anaishi na mtoto wao kwa kuwa hakujua kuwa Juliana aliwahi kuolewa kwani alidai kuwa yeye ni mwanafunzi wa VETA Mbeya.
Baba mzazi wa Juliana,  Hosea Mwalukasa alipopigiwa simu alidai kuwa ni kweli Biton alifika kwake lakini hakumpokea kwa kuwa alidai kuwa Juliana ni mke halali wa Rogers Halinga, akawaambia kuwa kama amezaa na Juliana amefanya kosa na kwamba atatozwa faini ya ugoni kwani mwanaye hakuwahi kupewa talaka na Halinga.
Baada ya mvutano wa muda mrefu kikao kiliamua kuwa endapo Biton anadai kuwa mtoto aliyezaliwa na Juliana aliyefahamika kwa jina la Zalida Biton (2) ni wake basi alipe fidia ya kuzaa na mke wa mtu kiasi cha shilingi milioni kumi au n’gombe saba ili aweze kumkomboa mtoto wake na kwamba Juliana bado ni mke halali wa Rogers.
 
Rogers Halinga na mkewe wakiwa kwenye kikao.
Kwa upande wake Biton alidai kuwa hayuko tayari kulipa faini hiyo kwa sababu alikabidhiwa mtoto kihalali na Jeshi la Polisi Oktoba 31, mwaka huu katika Kituo Kikuu cha Kati  mbele ya maafisa wa polisi na kwamba hana kesi ya kujibu na anasubiri mtoto afikishe umri wa miaka saba ndipo amchukue.
“Baadhi ya wadau wamelilalamikia Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuamua  masuala ya kisheria katika vituo vya polisi badala ya kufikisha katika mamlaka za kisheria kama mahakama. Uamuzi uliotolewa umesababisha tatizo kuwa zito,” alisema ndugu wa Rogers aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
 Amedai kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa kipimo cha DNA bado hakijatatua mgogoro huo na kwamba suluhu katika ndoa hiyo ni kitendawili kisicho na majibu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na GPL

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...