Tuesday, November 11, 2014

INTERPOL YAWASAKA WACHINA 30 KWA UJANGILI WA TEMBO

Kamishna wa Interpol Tawi la Tanzania, Gustav Babile 

Siku tano baada ya Serikali kukanusha vikali ripoti ya Shirika la Kimataifa la Mazingira (EIA) iliyoihusisha China na utoroshaji wa meno ya tembo nchini wakati wa ziara ya Rais wa nchi hiyo, Xi Jinping mwaka jana, Shirika la Polisi la Kimataifa (Intepol), Tawi la Tanzania limesema linawatafuta raia zaidi ya 30 wa China ambao wanatuhumiwa kusafirisha meno ya tembo na kufanya uharamia wa kimazingira katika hifadhi za Taifa nchini.
Kauli ya Interpol inakuja huku kukiwa na mkanganyiko kuhusu kashfa hiyo iliyosambaa wiki iliyopita kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa ambayo hata hivyo, Serikali imekanusha kupitia Ikulu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Maliasili na Utalii huku ubalozi wa China nchini nao ukitoa tamko la kukanusha taarifa hizo.
Kamishna wa Interpol Tawi la Tanzania, Gustav Babile alisema jana kuwa raia hao wa China wanatafutwa popote walipo duniani na hivyo watakapopatikana watakamatwa.
“Tunawatafuta popote duniani kwa usafirishaji wa meno ya tembo na uharamia wa mazingira, wakipatikana watachukuliwa hatua,” alisema Kamishna Babile. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Alisema majina na idadi kamili ya Wachina wanaotafutwa ipo na endapo kuna umuhimu wa kutajwa, yatatangazwa.
Mpaka sasa, mtandao wa Interpol umeweka majina ya raia wawili wa China, Mingzhi Zhang na Deng Jiyun ambao wanasakwa kwa tuhuma za kusafirisha meno ya tembo.
Wanadiplomasia kutokaguliwa
Wakati ripoti hiyo ilidai meno hayo yalisafirishwa kwa ndege ya Rais wa China kupitia maofisa wa kidiplomasia wa nchi hiyo ambao hawakaguliwi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema maofisa wataendelea kutokaguliwa kwa kuwa Serikali haiwezi kubadili sheria za kimataifa za maofisa hao kupata kinga ya kutokaguliwa wanapokuwa kwenye msafara wa Rais.
“Kwa ninavyojua, ukaguzi wa mizigo kwa misafara ya kidiplomasia unazingatia na kutawaliwa na sheria za kimataifa kwa hiyo Tanzania haiwezi kubadili tu kama Taifa,” alisema Balozi Sefue.
Hata hivyo, alisema ni vyema kama Wizara ya Mambo ya Nje ingezungumzia suala hilo la sheria za kutokaguliwa kwa mizigo ya maofisa wa msafara wa Rais.
“Ni sheria za kimataifa kwa hiyo ipo, mizigo ambayo inakidhi vigezo vya kimataifa vya kutofanyiwa ukaguzi na ipo ambayo haina vigezo hivyo,” alisema Sefue.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Katibu Mkuu wake, Michael Haule hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo lakini ofisa mmoja wa wizara hiyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema: “Kwa kawaida mizigo ya wanadiplomasia hao hukaguliwa ila wao wenyewe ndiyo hawakaguliwi, hilo ndilo jambo msilolielewa, ingekuwa wamebeba kitu kingeonekana tu.”
Alisema sheria za kimataifa haziruhusu maofisa au rais mwenyewe kukaguliwa mwilini lakini mizigo yao hukaguliwa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Sugu alia na Membe
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi amesema ni lazima Serikali ifanye uchunguzi wa kutosha na kuwawajibisha watu waliohusika kuichafua nchi na utoroshaji wa meno ya tembo badala ya kuja na kauli nyepesi kama alizotoa Waziri Membe kuhusu ripoti hiyo.
Akichangia Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2015/16, Mbilinyi maarufu kama Sugu alisema: “Tanzania imepata coverage (imeandikwa) juzi kwenye vyombo vya kimataifa kutokana na masuala ya meno ya tembo, ikisema kwamba uchunguzi huo ulifanyika kwa miaka 10 halafu leo Membe anasimama hapa na kusema ni uzushi.
“Wazungu wanaleta uzushi? Mbona wakisema kwamba Rais wa Tanzania ni kinara wa utawala bora Membe hakai hapa na kusema ripoti hiyo ni uzushi?”
Alisema alichokitoa Membe ni mawazo yake na alichotakiwa kufanya ni kuliambia Bunge kufanyike uchunguzi wa kimataifa kuhusu suala hilo na ikigundulika kwamba ripoti hiyo ilikuwa ni ya uongo zichukuliwe hatua kwa hao wanaoichafua nchi.
“Taarifa kama ile kuwa kwenye vyombo vikubwa kama BBC na Aljazeera ni kuchafua nchi yetu na kwa aina hiyo hatuwezi kwenda mbele, mambo kama haya wananchi wanahitaji washirikishwe kwani wanaposikia taarifa kama hizi zinawafanya washindwe kuunga mkono mipango ya maendeleo kama hii tunayojadili hapa,” alisema Sugu.
“Kila siku tunapiga kelele linaibuka jingine, mnataka muambiwe hizi pembe zimebebwa na nani ndipo mjue kwamba hili suala limekuwa kubwa na limefika mahala halikubaliki?”
Alisema ripoti hiyo imeeleza kuwa sababu ya yote hayo ni rushwa na uongozi dhaifu kwamba kuna udhaifu wa kiuongozi na Mnyika (John, Mbunge wa Ubungo) aliwahi kusema mkang’aka, lakini leo dunia imesema suala hilo la rushwa na uongozi dhaifu liwe changamoto ili kufanikisha mambo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...