MSANII
wa filamu za Kibongo, Wastara Juma hivi karibuni alikataa kuolewa na
kuwa mke wa pili baada ya kupigiwa simu na mwanamke mmoja jijini Dar
akimtaka awe mke mwenzake.
Wastara
ambaye hivi sasa yuko Uarabuni kwa ajili ya mapumziko baada ya kufiwa
na mumewe, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Januari mwaka huu, alikataa
ofa hiyo na kusema kwamba kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini, mwanamke huyo aliamua kufanya hivyo
baada ya kushauriana na mumewe kuhusu Wastara kuingia katika familia
yao.
“Mwenyewe
alisema alishauriana na mumewe na haoni tatizo Wastara kuwa mke
mwenzake kwa sababu imani ya dini yao inaruhusu,” kilieleza chanzo
hicho.
UTHIBITISHO NI HUU
Baada
ya kuzinyaka habari hizo, kama kawaida yate lilimnyanyulia mkonga
mwanamke huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe, akathibitisha
kumpigia Wastara.
“Lengo
langu
lilikuwa zuri tu, unajua dini yetu ya Kiislamu inaturuhusu kuolewa
wanawake mpaka wanne hivyo niliona ni heri nikae na mwenzangu.
“Halikuwa
suala la kukurupuka...tulizungumza na mume wangu na tulishajipanga
kwenda kutoa mahari kwao. Nimesikitika sana alivyokataa ila namtakia
kila la heri katika maisha yake,” alisema.
WASTARA SASA
“Ni
kweli nilipigiwa simu na mwanamke wa huko nyumbani (Tanzania),
nilimjibu kama ninavyokuambia wewe sasa hivi, kwamba sifikirii kuolewa
kwa sasa,” alisema Wastara kwa njia simu alipopigiwa na mwandishi wetu.
No comments:
Post a Comment