Rais wa Botswana, Ian Khama ameshonwa baada ya kung'atwa na Duma, kwa mujibu wa maafisa wakuu nchini humo.
Mnyama huyo alikuwa analishwa alikokuwa anahifadhiwa katika kambi ya kijeshi wakati alipomrukia rais Khama na kumgwara
Tukio
hilo ilikuwa ajali tu wala sio shambulio kali, kwa mujibu wa msemaji wa
serikali Jeff Ramsay aliyezungumza na waandishi wa habari.
Majeraha ya Bwana Khama, yalikuwa madogo wala haikujitokeza kama ajali kubwa.
Inaarifiwa ajali ilitokea ghafla na kumgutukia Rais Khama na walinzi wake.
"Duma alimgwara tu lakini sio kumshambulia, kama wanavyodahani watu wengi,'' alisema bwana Ramsay.
Bwana Khama alionekana akiwa amevalia plaster kwenye mkutano ulioandaliwa baada ya tukio hilo.
Duma, ambao ndio wanyama wenye kasi kubwa zaidi ardhini, ni moja ya wanyama wanaokabiliwa na tisho kubwa la kuangamia.
Ni wanyama 12,400 pekee wanaosemekana kusalia mbugani katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Botswana.
No comments:
Post a Comment