Saturday, March 09, 2013

RAIS KIKWETE NA ABDULRAHAMAN KINAN WAMJULIA HALI MHARIRI MTENDAJI WA HABARI CORPORATION ABSALOM KIBANDA AFRIKA KUSINI


 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika ya Kusini leo jioni. Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...