Wagombea wa uraisi
nchini Kenya
Wakati harakati za kampeni za uchaguzi wa
uraisi zinafikia ukingoni nchini Kenya, Marekani imewataka raia wa Kenya kufanya
uchaguzi wa amani ili kumpata kiongozi mpya kwa amani.
Akizungumza kwa niaba ya serikali naibu msemaji
wa serikali ya Marekani Patrick Ventrell ameongeza kuwa Kenya inapita katika
kipindi cha muhimu na kihistoria na hivyo kuwasihi wagombea kuhakikisha
wanaepuka kuwa sababisho la umwagaji damu kama uliowahi kutokea katika uchaguzi
wa mwaka 2007.
Hata hivyo hali ya mvutano imeongezeka ambapo
serikali ya Marekani imewataka wakenya kutumia fursa hiyo kudumisha ukomavu wa
demokrasia na kutekeleza matakwa ya katiba mpya.
Msemaji huyo amesema kuwa ni matarajio ya wengi
kuwa wakenya hawatajali jinsi,kabila,dini,eneo analotoka mgombea ili kuchagua
bali bali watamchagua kiongozi bora kulingana na sifa stahiki.
Takribani raia elfu moja walipoteza maisha huku
laki sita wakiyakimbia makazi yao katika machafuko yaliyotokea katika kipindi
cha uchaguzi wa mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment