MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE,
Kwa
heshima kubwa, Chama cha NCCR-Mageuzi kinapenda kuwasilisha rasmi
mapendekezo yake kwako yenye lengo la kuinusuru elimu ya Watanzania,
kama ifuatavyo:
Utangulizi
Mheshimiwa Rais,
Sisi
Chama cha NCCR-Mageuzi tumeguswa sana na hali isiyoridhisha ya ubora wa
elimu katika Taifa letu la Tanzania. Hivyo tunaona ipo haja ya
kuchukuliwa kwa hatua za dharura kuinusuru elimu, ili taifa
lisiharibikiwe zaidi, badala yake kuwe na elimu yenye ubora wa hali ya
juu na utimilifu wa malengo tuliyonayo kama taifa.
Mheshimiwa Rais,
Katika muktadha wa mapendekezo tunayoyaleta kwako, tunazingatia masuala ya kitaifa yafuatayo:-
(i) Tangu Taifa letu lipate uhuru wake mwaka 1961 (kwa Tanganyika) na
mwaka 1964 (Mapinduzi ya Zanzibar) tulitambua umuhimu wa kufuta ujinga,
kwa kuelimisha wananchi ili tujiletee maendeleo. Ingawa hadi sasa kazi
kubwa imefanyika katika kukuza elimu hapa nchini, bado hatujafika katika
hali ya kuwa na taifa ambalo karibu kila raia mwenye umri stahiki
anajua kusoma na kuandika.
(ii)
Katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, tunataja pamoja na mambo
mengine kwamba, ifikapo mwaka 2025 tuwe tumejenga taifa la watu
walioelimika kwa upeo wa juu katika nyanja mbalimbali.
(iii)
Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, ambao una
malengo nane ya milenia; lengo la pili likiwa ni upatikanaji wa elimu
bora kwa wote (achieving universal primary education)); na
(iv)
Ifikapo mwaka 2015 (takribani miaka miwili toka sasa) tutalazimika kama
taifa kupima utekelezaji wa malengo hayo ya milenia ili kuendana na
viwango vya kimataifa.
Mheshimiwa Rais,
Wakati
tukikabiliwa na malengo hayo ya Kitaifa, kwa muda mrefu kumekuwepo na
viashiria vingi vinavyoonesha kwamba ubora wa elimu itolewayo hapa
nchini katika ngazi zote hauridhishi. Viashiria hivyo ni pamoja na:-
No comments:
Post a Comment