Tuesday, March 19, 2013

IGP SAID MWEMA AIBUKA SAKATA LA DK. ULIMBOKA, KIBANDA.


 IGP SAIDI MWEMA.
 Dk Ulimboka kabla hajaanza kutibiwa.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.




MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema amesema upelelezi wa kesi ya kutekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka bado haujakamilika.

Mbali na Dk. Ulimboka, IGP alisema kesi nyingine zote za aina hiyo pamoja na za mauaji ya watu mbalimbali, akiwemo Padri wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili lililopo Mji Mkongwe Zanzibar, Evaristus Mushi (56), uchunguzi wake unaendelea.
IGP Mwema, aliyasema hayo jana wakati wa semina ya wakuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mjini Dar es Salaam jana.
Dk. Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, alitekwa usiku wa kuamkia Juni 27, 2012. 
Hata hivyo, suala hilo lilizua sintofahamu ya aina yake baada ya mtuhumiwa Joshua Mulundi, raia wa Kenya kukamatwa na kufunguliwa kesi, akishtakiwa kwa kosa la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.
Akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari waliotaka kujua upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi, licha ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kesi hiyo, ambaye anaendelea kusota gerezani, IGP Mwema alisema upelelezi wa kesi unategemea kupatikana mapema kwa ushahidi husika, vinginevyo kesi za aina hiyo zinaweza kuchukua muda mrefu.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...