Tuesday, March 19, 2013

AU YAMKARIBISHA RAIS WA UJERUMANI

Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Joachim Gauck anaendelea na ziara yake rasmi nchini Ethiopia. 
Baada ya mazungumzo pamoja na viongozi wa serikali ya nchi hiyo , Rais Gauck aliwahutubia wawakilishi wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa. 
Hotuba ya Rais Gauck mbele ya wawakilishi wa Umoja wa Afrika ilikuwa ikiangaliwa kama kilele cha ziara ya siku nne ya rais huyo wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini Ethiopia. Rais Gauck alizungumzia  zaidi  kuhusu  demokrasia na haki za binaadamu.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 73 amewatolea mwito viongozi wa Afrika wafungue ukurasa mpya wa demokrasia na utawala unaofuata sheria. Rais Gauck amesema kuwa  "Afrika inabidi izishinde  changamoto zilizoko na kubuni njia ya Kiafrika kuelekea demokrasia". 
Rais Gauck amezitaka  nchi zote za Afrika  ziwe na serikali zilizochaguliwa kwa njia za kidemokrasia na bunge kujipatia madaraka makubwa zaidi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...