Tuesday, December 29, 2015

ARSENAL YAPAA KILELENI


Wachezaji wa timu ya Arsenal

Washika bunduki wa London, Arsenal wamekaa kileleni mwa ligi ya England kwa pointi 39 baada ya kuichapa Bournemouth kwa mabao 2-0.

Arsenal walipata mabao yao kupita kwa beki Gabriel Paulista aliyefunga bao la kwanza Dakika ya 27 ya mchezo kisha kiungo wa Kijeruman Mesut Ozil, akahitimisha kazi kwa bao la pili alilolifunga katika dakika ya 63.

Nao Mashetani Wekundu wa Man United wakaenda sare ya 0-0 na mabingwa watetezi Chelsea, Everton wakicheza katika dimba lao la Goodson Park wakalala kwa kipigo cha mabao 4-3 dhidi ya Stoke city.

Matokeo mengine ni: Crystal Palace 0 – 0 Swansea Norwich 2 – 0 Aston Villa Watford 1 – 2 Tottenham West Brom 1 – 0 Newcastle West Ham 2 – 1 Southampton

Monday, December 28, 2015

MLINZI WA OSAMA BIN LADEN AFARIKI DUNIA


Al Bahri


Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Vyanzo vya habari vya kitabibu vimesema kwamba Nasser al Bahri ambaye pia alikuwa akijulikana kama Abu Jandal alifariki siku ya Jumamosi, katika Hospitali iliyoko kwenye mji wa Mukalla kusini mwa Yemen.

Alirudi nchini humo mwishoni mwa mwaka 2008, baada ya kuachiliwa kutoka katika kizuizi alichowekewa na Marekani huko Guantanamo.

Al Bahri alijulikana kuhusika na mashambulizi yaliyofanywa na mtandao wa kigaidi katika miaka ya 90, katika nchi za Afghanistan, Somalia na Bosnia.

Thursday, December 17, 2015

MAGUFULI "ELIMU BURE ITAPATIKANA"

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kwamba elimu ya bure itapatikana kama alivyoahidi.

Akijibu swali la fedha zitapatikana wapi za kutimiza ahadi yake ya elimu ya bure, Magufuli amesema, mwezi huu wa Desemba pekee, Tanzania inatarajiwa kukusanya kiasi cha dola bilioni 1, ambazo hazijawahi kukusanywa.

Amesema kuanzia mwezi huu fedha za kusomesha wanafunzi bure zitaanza kutengwa kuanzia mwezi huu. Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, Serikali imefikia uamuzi wa kutenga dola milioni 65.5, ambazo zitapelekwa moja kwa moja katika shule zenye uhitaji na kwamba fedha zitakapotumwa, nakala ya barua itapelekwa kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wake.

Rais Magufuli ameonya yeyote atakayetumia fedha hizo vinginevyo kwamba atachukuliwa hatua kali. Amesema fedha hizo zitasaidia katika ununuzi wa vitu kama vile chaki, maandalizi ya mitihani na vitu vingine vya muhimu shuleni.

Thursday, December 10, 2015

MH. MAGUFULI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri - George Simbachawene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Thursday, November 26, 2015

DJIBOUTI, ZANZIBAR HEROES HALI TETE

Kikosi cha Zanzibar Heroes

Michuano ya CECAFA CHALENJI CUP 2015 imeendelea jana Jumatano kwa michezo minne ya hatua ya makundi. Harambe stars ya kenya ilitoka sare ya bao 1-1 na Burundi, wenyeji Ethiopia wameifunga somalia bao 2-0, Malawi imeifunga Djibout bao bao 3-0.

Sudani kusini ikitoshana nguvu na ndugu zao Sudan baada ya kutoka bila ya kufungana.
Michuano hiyo itaendelea tena kesho ijumaa kwa michezo kadhaa, Rwanda wataikabili somalia, Vibonde Zanzibar Heroes watakuwa viwanjani dhidi ya Kenya.

Sudan kusini watawakabili Malawi na Djibout itachuana na SudanMichuano hiyo itaendelea tena kesho ijumaa kwa michezo kadhaa, Rwanda wataikabili somalia, Vibonde Zanzibar Heroes watakuwa viwanjani dhidi ya Kenya.

Sudan kusini watawakabili Malawi na Djibout itachuana na Sudan. Michuano hiyo itaendelea tena kesho ijumaa kwa michezo kadhaa, Rwanda wataikabili somalia, Vibonde Zanzibar Heroes watakuwa viwanjani dhidi ya Kenya.

Sudan kusini watawakabili Malawi na Djibout itachuana na Sudan.

Wednesday, November 25, 2015

BARAZA LA MAWAZIRI LABADILISHWA...!!!


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, na kuwaacha wote wizara zao zilizotajwa katika ufisadi. 

Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa.

Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni. Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni, Rais Uhuru Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka kumi na tisa hadi ishirini na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora zaidi .

KILIMANJARO STARS YACHINJA MTU CECAFA...!!!


Wachezaji wa Kilimanjaro Stars

Michuanao ya Cecafa Chalenji Cup Imeendelea tena jana kwa michezo miwili katika hatua ya makundi. Zanzibar ilifungwa bao 4-0 na Uganda ikiwa ni Mechi ya Kundi B.

Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imeichapa Rwanda bao 2-1 katika mchezo uliopigwa mjini Awassa na kupaa kileleni mwa Kundi A wakiwa na Pointi 6 kwa Mechi 2 na kujihakikishia kucheza hatua ya Robo Fainali.

Mabao ya Kilimanjaro stars yalifungwa na Said Ndemla pamoja na Simon Msuva huku bao la Rwanda likifungwa na mchezaji Tisiyege.

Michuano hiyo itaendelea tena leo jumatano kwa mechi kadhaa ambapo Kenya itachuana na Burundi.

Somalia itaivaa Ethiopia, Malawi itaikabili Djibouti na Sudan kusini watachuana na ndugu zao Sudan.

BARCELONA YAIZIMA AS ROMA


Mchezaji wa As Roma

Barcelona wakiwa nyumbani walichomoza na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya As Roma.

Buyen Munich wakiichapa Olympiakos bao 4-0, Maccabi Tel Aviv wakila hio kwa Chelsea kwa kichapo cha mabao 4-0. 

BATE Borislov wakifungana bao 1-1 na Buyer Liverkusen , FC Porto wakilala bao 2-0 dhidi ya Dynamo Kiev, Zenit St P wakiichapa Valencia bao 2 – 0 na Lyon wakilala mbele ya KAA Gent bao 2-1.

ANDY MURRY TAYARI KWA DAVIS CUP


Kikosi cha Timu ya Tennis ya Uingereza

Timu ya Taifa ya Uingereza ya Tenis, imewasili nchini Ubegiji kwa mchezo wa fainali ya Davis Cup utakaopigwa ijumaa nchini humo. 

Timu hiyo inaongozwa na Andy Murray imewasili chini ya uangalizi wa ulinzi mkubwa kufuatia tishio la matukio ya kigaidi ambayo yameonekana kutishia amani nchini ubelgiji.

Timu hiyo inayojulikana pia kama Great britain ilipaswa kufika nchini humo tangu Jumapili lakini ikaahirisha kutokana na masuala ya kiusalama zaidi.

 Kikosi cha Uingereza kinawakilishwa na Andy Murray, Jamie, Kyle Edmund, Dominic Inglot na James Ward ambao tayari wapo nchini Ubelgiji.

Tuesday, November 10, 2015

MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MUHIMBILI, ABADILISHA USIMAMIZI WA HOSPITALI

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli akiongea na mgonjwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipofanya ziara ya kushitukiza hospitalini hapo.

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo amefanya ziara nyingine ya kushtukiza, wakati huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kufanyia mabadiliko usimamizi wa hospitali hiyo.

Kiongozi huyo mpya amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu. 

“Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko,” katibu wake mkuu Ombeni Sefue amesema.

Sunday, November 01, 2015

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015 YATANGAZWA, UFAULU JUU


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt Charles Msonde


Wahitimu 518, 034 kati ya 763, 602 waliofanya mitihani ya kuhitimu darasa la saba iliyofanyika nchini kote kuanzia Septemba 2 hadi Septemba 10, mwaka huu wamefaulu mitihani yao, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limesema leo.


 Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 67.84, asilimia 10.85 zaidi ya ufaulu wa mwaka 2014 ambapo waliofaulu walikuwa asilimia 56.99. 

Dkt Msonde amesema, ufaulu katika masomo yote umeongezeka kwa asilimia kati ya 4.61 hadi 17.22 ikilinganishwa na mwaka 2014 huku watahiniwa wakifaulu zaidi somo la Kiswahili (asilimia 77.20) na kufaulu kwa kiwango cha chini katika somo la Kiingereza (asilimia 48.56.

Amesema kati ya watahiniwa wote waliofaulu 264, 130 ni wasichana ambao ni sawa na asilimia 64.60 ya wasichana wote 408, 900 waliotahiniwa huku wavulana wakiwa 253, 904 sawa na asilimia 71.58 ya wavulana 354, 706 waliotahiniwa.

Wednesday, October 28, 2015

TOYOTA NDIO GARI MAARUFU ZAIDI DUNIANI


Sasa ni rasmi Toyota ndiyo gari maarufu zaidi duniani. Kampuni hiyo ya kutengeneza magari ya Japan imeipiku Volkswagen kutoka kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya makampuni yaliyouza idadi kubwa zaidi ya magari duniani mwaka huu.

Yamkini Toyota imeuza takriban magari milioni 7.5 katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka huu. Wapinzani wao wa karibu Volkswagen kwa upande wao wameuza magari milioni 7.43. Nafasi ya tatu inashikiliwa na kampuni ya kutengeneza magari ya Marekani, General Motors.
GM iliuza magari milioni 7.2 katika kipindi hicho cha miezi 9 ya mwanzo wa mwaka huu. Wadadisi wanasema kuwa sakata ya udanganyifu iliyoikumba kampuni hiyo ya ujerumani itaathiri zaidi mauzo yake katika siku za hivi punde.

Sunday, October 25, 2015

UCHAGUZI WAHAIRISHWA KWA KUKOSA KARATASI ZA UDIWANI


Wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura kwa nafasi ya udiwani kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah Malela amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.

Alisema kuwa kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini karatasi ambazo zimetoka Tume ya ucHaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi ya wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.

RPC ARUSHA AONYA WANAOTAKA KUFANYA VURUGU


Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas .

Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limebaini vikundi vilivyojipanga kufanya vurugu na akavitaka kuacha kutekeleza mpango huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Sabas alisema wamebaini kuwa zaidi ya vijana 100 wamesambazwa mjini Arusha na Arumeru kwa ajili ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi. 

Alisema polisi wamejipanga kukabiliana na uhalifu au vurugu zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwa tayari wamepokea tetesi za kuwapo kwa makundi hayo. “Natoa onyo kwa hayo makundi kuwa kama wanataka usalama waache mara moja kwa kuwa hawatakuwa salama,” alisema Liberatus.

Wednesday, October 14, 2015

RONALDO ATWAA KIATU CHA DHAHABU

Cristiano Ronaldo akiwa na buti za dhahabu 
 
Cristiano Ronaldo ametunukiwa kiatu cha Dhahabu kwa Ufungaji Bora huko Ulaya na kuweka rekodi kwa kutwaa kwa mara ya nne.

Katika msimu wa 2014/15, Ronaldo alifunga mabao 48 kwenye La Liga na kutwaa Buti ya Dhahabu kwa mara 3 akiwa na Real Madrid. Msimu wa 2007/08 akiwa na Manchester United alitwaa tena kiatu hicho baada ya kuwa mfungaji bora.

Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 47 ya Tuzo hii ya Buti ya Dhahabu kwa Mfungaji Bora wa Ligi za Ulaya kuichukua mara 4.

Ronaldo, ameifungia Real Jumla ya Mabao 323, na kufika Rekodi ya mabao mengi iliyokua imewekwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Raúl González Blanco aliyekua kaifungia timu hiyo mabao 323. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

TAIFA STARS KUIVAA ALGERIA NOVEMBA 14

Kikosi cha Taifa Stars ya Tanzania 
 
Timu ya Taifa ya Tanzania itajitupa uwanja Novemba 14 kukipiga na timu ya taifa ya Algeria ikiwa ni hatua ya pili kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.

Katika mchezo huo Stars wataanzia nyumbani katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa marudiano utakuwa huko nchini Algeria siku tatu baadae ambapo Mbweha hao wa Jangwani watakua ndio wenyeji wa mtanange huo.

Kikosi cha Stars chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa kimefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Malawi (The Flames) kwa jumla ya mabao 2-1, nyumbani ikishinda 2-0, na kufungwa 1 – 0 jijini Blantyre. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Monday, October 05, 2015

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA 13





Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete 

Rais Jakaya Kikwete amewateua wakuu wapya 13 wa wilaya na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba.
Walioteuliwa ni Shaaban Ntanambe ambaye anakwenda Chato; Thabisa Mwalapwa (Hanang), Richard Kasesera (Iringa), Ruth Msafiri (Kibondo) na Abdallah Njwayo (Kilwa).

Wengine ni Asumpta Mshama (Wanging’ombe), Mohammed Utaly (Mpwapwa), Dauda Yasin (Makete), Honorata Chitanda (Ngara), Vita Kawawa (Kahama), Christopher Ng’ubyagai (Mkalama), Hawa Ng’humbi (Kishapu) na Mrisho Gambo (Uvinza).

Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka Mkalama, kwenda Wilaya ya Arusha, Wilson Nkambaku anahamishiwa Arumeru, kutoka Kishapu, Francis Miti ambaye anahama Hanang kwenda Monduli na Jowika Kasunga ambaye anahamia Mufindi kutoka Monduli.

Wengine waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Makete kwenda Morogoro; Hadija Nyembo anayehamia Kaliua kutoka Uvinza na Benson Mpesya ambaye anahamia Songea Ruvuma kutoka Kahama. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

DEREVA BODABODA AUAWA NA KUNYOFOLEWA KICHWA NA SEHEMU ZA SIRI



 Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wakiwa katika kijiwe chao. PICHA NA MAKTABA

Watu wasiofahamika wamemuua kwa kumchinja mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, Hosam Abdallahaman (18) na kutoweka na kichwa chake, sehemu zake za siri na pikipiki.   

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo juzi usiku katika Kijiji cha Silimka, Kata ya Itilo wilayani hapa.



Kamanda Issa alisema kabla ya mauaji hayo, saa moja usiku, Hosam alikodiwa na abiria ampeleke eneo la Silimka na hakurudi kwenye kituo chake cha kazi hadi alipokutwa akiwa ameuawa majira ya saa 4 asubuhi siku iliyofuata. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

KIKWETE NA UHURU WAZINDUA BARABARA MUHIMU

Barabara hiyo ni ya pili kufadhiliwa na AfDB baada ya ile ya Arusha-Namanga / Namanga - Athi River
 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Tanzania Jakaya Kikwete wamezindua mradi wa ujenzi wa barabara ya Taveta-Mwatate ambayo inatarajiwa kurahisisha uchukuzi kati ya kataifa hayo mawili.

Barabara ya Arusha-Holili upande wa Tanzania pia inakarabatiwa. Rais Kikwete yumo nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu na Jumanne anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili ya Kenya.

Mradi wa ujenzi wa barabara hizo mbili umefadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali za Kenya na Tanzania. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

WENGER AFURAHIA USHINDI DHIDI YA MAN UTD

Arsene Wenger
 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza furaha yake baada ya klabu hiyo kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili.

Wenger amesema alifurahishwa sana na uchezaji wa timu yake na kueleza kuwa walishangaza Manchester United kuanzia mwanzo wa mechi.

“Kuanzia kwa Petr Cech hadi kwa Theo Walcott wote walicheza vyema. Nimenoa timu nyingi kali lakini hakuna hata moja iliyoweza kucheza mechi 60 katika kiwango sawa. Lazima ukubali kwamba sisi ni binadamu,” alisema.

“Tuko kwenye kinyang’anyiro (cha kushindania taji), tuko alama mbili nyuma ya viongozi Manchester City na natumai matokeo ya leo yatatupa imani ya kuendelea kupigania taji.” Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

TP MAZEMBE KUKUTANA NA ALGER FAINALI

Timu ya TP Mazembe 
 
Klabu ya TP Mazembe ya Congo DRC, Itakutana na klabu ya Algeria USM Alger katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika.

Mazembe ilijihakikishia nafasi yake siku ya jumapili yaani jana baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merrekh ya Sudan mjini Lubumbashi.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta alifunga mara mbili katika ushindi huo huku Muivarycoast Roger Assale akifunga goli la tatu. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 05, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Sunday, October 04, 2015

LUBUVA: MABADILIKO YA WATENDAJI NEC NI YA KAWAIDA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametetea uteuzi wa viongozi wapya ndani ya tume huku akisema wanasiasa hawatakiwi kuingilia mambo hadi jikoni.

Jaji Lubuva alisema hayo leo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha Funguka kilichorushwa moja kwa moja na televisheni ya Azam.

"Kuhamishwa au kuteuliwa kwa kiongozi ni jambo la kawaida kwenye taasisi yoyote...uteuzi unaweza kutokea wakati wowote,"alisema Jaji Lubuva. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

MAMA NA MWANA WAUAWA KWA MAPANGA

Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Peter Kakamba . 

Mkazi wa Kijiji cha Saragulwa, Kata ya Nyamwilolela mkoani hapa na mwanaye wameuawa kwa kukatwa mapanga na watu ambao hawajajulikana. 

Tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati mwanamke huyo, Mageni Hongera (25) akiwa amembeba mgongoni mwanaye, Joyce Ndarusanze (1), akitokea kwenye kibanda chake cha biashara kwenda nyumbani kwake. 

Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Peter Kakamba alisema jana kuwa askari wa jeshi hilo wanaendelea kufuatilia chanzo cha mauaji hayo. “Ni kweli tukio limetokea, bado sijakusanya vizuri taarifa zake,” alisema Kakamba.  Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

TANESCO: UZALISHAJI WA UMEME UMESHUKA


Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limesema kuwa mgao wa umeme unaoendelea nchini umesababishwa na kushuka kwa uzalishaji wa umeme katika mabwawa ya maji kwa asilimia 81.3. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema leo jijini dar es Salaam kuwa uwezo wa juu wa mitambo yote ya kuzalisha umeme wa maji ni megawati 561, lakini kwa sasa uzalishaji wote wa umeme wa maji ni megawati 105 ambazo ni sawa na asilimia 18.7. 

Kuhusu umeme wa gesi, TANESCO walisema kuwa uwezo wa kuzalisha umeme kupitia Kampuni ya Pan Africa ulishuka kutoka megawati 340 hadi kufikia megawati 260. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 04, YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
.
.

Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Monday, September 28, 2015

MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA DODOMA MJINI APATA DHAMANA

Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini kupitia
Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini kupitia Chadema, Benson Kigaila  

Ulinzi mkali leo umewekwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Dodoma ili kuzuia wafuasi wa Chadema waliokwenda kusikiliza kesi inayomkabili mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Benson Kigaila na kusababisha lango la kuingilia lifungwe.

Kigaila na wenzake 10 wanakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kumpiga na kumjeruhi polisi, kufanya maandamano bila ya kibali na pamoja na kutoa lugha za matusi katika kituo cha polisi makosa ambayo watuhumiwa hao waliyakana yote.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha, Wakili wa Serikali Beatrice Nsana amesema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa yote Septemba 25 mwaka huu majira ya jioni.
Nsana amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama ipange tarehe ya kuanza kusikilizwa ambapo mahakama imekubali na kupanga Oktoba 12 mwaka huu huku dhamana ikiwa wazi.
Mara baada ya kutimizwa kwa masharti ya dhamana kwa washitakiwa wote, viongozi hao waliondoka chini ya ulinzi mkali wa polisi na kusindikizwa hadi katika ofisi za kanda za chama hicho ambako Kigaila alizungumza na waandishi wa habari. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

CELINE DION ARUDI KWENYE MUZIKI

celine dion
BAADA ya Celine Dion kukaa kwa muda mrefu bila ya kufanya muziki kutokana na kumuuguza mume wake, Rene Angelil, sasa ameanza kazi ya muziki upya.

Celine alipanda jukwaani juzi huku mume wake akiwa pembeni na kabla ya kuimba aliwaambia mashabiki: ‘Nadhani kila mmoja anajua nini ninataka kukufanyia leo siku yangu rasmi.’

Hata hivyo, msanii huyo alijikuta akidondosha chozi kutokana na mapokezi aliyoyapata kutoka kwa mashabiki wake.

Baada ya kumaliza kuimba msanii huyo aliwashukuru mashabiki hao na kuwaahidi kuwapa burudani mbalimbali siku zijazo. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

“Nashukuru kwa uwepo wenu hapa, lakini kikubwa kilichonifanya niwe hapa ni watoto wangu watatu na mume wangu ndio waliniambia nifanye hivi, nawapenda sana watoto wangu pamoja na mume wangu na nipo tayari afie mikononi mwangu,” alisema Celine

SIMBA WASHIKANA UCHAWI, YAMSHTAKI MWAMUZI

Simba-vs-Yanga-8

KIPIGO ilichokipata timu ya Simba kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga juzi kimezua mapya kwa wekundu hao baada ya wachezaji watatu wa safu ya ulinzi kudaiwa kufanya hujuma

Yanga ilivunja uteja dhidi ya Simba kwa kuichapa mabao 2-0 yaliyofungwa na washambuliaji, Amissi Tambwe na Malimi Busungu.

Habari za kutoka ndani ya Simba zilizolifikia gazeti hili zimedai kuwa wachezaji hao wa safu ya ulinzi walishindwa kabisa kuwazuia washambuliaji wa Yanga, waliofunga mabao rahisi jioni hiyo. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Wednesday, September 23, 2015

DIEGO COSTA KUKOSA MECHI TATU


Diego Costa atakosa michezo mitatu baada ya chama cha soka cha England FA kuthibitisha kukutwa na makosa.

Costa alikana mashtaka yaliyokuwa yakimkabili kuhusiana na kumfanyia fujo mlinzi wa Arsenal Laurent Koscielny katika ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Arsenal.

Costa mwenye miaka 26 alionekana kuweka mikono yake juu ya uso wa Koscielny kabla ya kuanza kuzozana na Gabriel Paulista ambaye baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu. Mlinzi huyo wa Arsenal alitolewa nje na mwamuzi Mike Dean kwa kumfanyia vurugu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania.

Costa atakosa mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Walsall siku ya jumatano sambamba na ile ya ligi kuu kati ya Newcastle na Southampton. 

Baada ya kuthibitisha kuwa mwamuzi wa mchezo hakuona tukio la Costa na Koscielny, chama cha soka England kimesambaza kanda hizo za vidio kwa waamuzi wakongwe watatu wa zamani.

Monday, September 14, 2015

MTUHUMIWA WA UGAIDI AJARIBU KUJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI



Kamishna wa polisi Kanda Maalum wa Dar es
Kamishna wa polisi Kanda Maalum wa Dar es Salaam, Suleiman Kova 

Mtu anayedaiwa kuwa mratibu wa matukio ya ugaidi, uporaji wa silaha na mauaji katika vituo vya polisi , Ally Ulature (60) amejeruhiwa baada ya kujirusha katika ghorofa  kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni azimio la kujiua  au kutoroka.

Akizungumza leo, Kamishna wa polisi Kanda Maalum wa Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema Ulature ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mnandimkongo, wilayani Mkuranga  alikamatwa mwezi huu baada ya msako mkali wa polisi.
Kamanda Kova amesema Ulature amejirusha kutoka ghorofa ya tatu katika jengo la makao makuu ya polisi alipokuwa akihojiwa na maofisa upelelezi. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Sunday, September 13, 2015

MATOKEO YA MECHI ZA UFUNGUZI WA LIGI KUU TANZANIA BARA (VPL) HAYA HAPA


Pazia la ligi kuu Tanzania bara limefunguliwa rasmi jana ambapo michezo saba zimechezwa kwenye viwanja tofauti wakati jumla ya timu 14 zilikuwa viwanjani zikiwania pointi tatu muhimu, matokeo ya mechi zote zilizochezwa siku ya Jumamosi ni kama ifuatavyo; 

Azam FC 2-1 Tanzania Prisons (Azam Complex, Chamazi) 

African Sports 0-1 Simba (Mkwakwani, Tanga) 

Ndanda FC 1-1 Mgambo JKT (Nangwanda Sijaona, Mtwara)

Toto Africans 1-0 Mwadui FC (CCM Kirumba, Mwanza) 

Stand United 0-1 Mtibwa Sugar (Kambarage, Shinyanga)

Majimaji FC 1-0 JKT Ruvu (Majimaji, Songea) 

Mbeya City FC 0-1 Kagera Sugar 

Leo utachezwa mchezo mmoja wa ligi kuu Tanzania bara kwa kuzikutanisha Yanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA EPL ZILIZOPIGWA JUMAMOSI NDIO HAYA HAPA

Jana kulipigwa michezo saba kwenye ligi kuu nchini England (VPL) ambapo mbali na mchezo wa Manchester United dhidi ya Liverpool, kulikuwa na michezo mingine ambayo huenda hukupata muda wa kuitazama yote kwa pamoja. hapa chini kuna matokeo ya mechi zote saba zilizochezwa Jumamosi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...