Wednesday, March 18, 2015

NYALANDU AMJIBU KINANA; 'SASA NITAZURURA ANGANI KUPAMBANA NA MAJANGILI'

 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akielekezwa kitu na wataalam wa ndege hiyo aliyozindua jana.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana alionekana kumpiga kijembe Katibu MKuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana aliposema kuwa sasa atakuwa anazurura angani.
Nyalandu alitoa kauli hiyo Dar es Salaam alipozindua ndege nyepesi (Micro-Light, 5H – Hel), ambayo itatumika kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Selous.
“Karibuni wote, leo tunazururia hapa uwanja wa ndege na ninazindua ndege hii nyepesi ambayo imetengenezwa Ufaransa, itatumika kupambana na majangili katika Mbuga ya Selous.
“Kwa maana hiyo sasa tunaanza kuzururia angani kupambana na majangili na nasisitiza kwamba ndege hii ni mpya kabisa na gharama za uendeshaji wake ni ndogo kwa vile inatumia petroli,” alisema.
Hivi karibuni Kinana akiwa ziarani mkoani Arusha alimsifia Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kuwa ni mchapakazi lakini Waziri Nyalandu ni mzururaji.


Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa ndege hiyo ya kupambana na ujangili, Nyalandu alisema imetengenezwa kwa gharama ya Dola za Marekani 2,040,000 na ina uwezo wa kubeba askari mmoja na rubani.


Waziri Nyalandu alisema ndege hiyo imeundwa kwa usalama wa hali ya juu kwa kuwekewa puto (parachute) ambalo litatumika kushuka chini iwapo ndege itaishiwa mafuta angani.


“Itakapoanza kutumika itasaidia kuwabaini majangili, inakwenda kwa mwendo mdogo iwapo angani hali ambayo inawezesha kuwaona majangili na kila kinachoendelea ardhini kwa wepesi,”alisema Nyalandu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UBUNGE WA ZITTO WANING'INIA...!!!

Zitto Kabwe 

Kitendo cha kutupiana mpira kati ya Ofisi ya Bunge, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu hatima ya Zitto Kabwe, kimeufanya ubunge wa mbunge huyo kuendelea kuning’inia huku mwenyewe akitazamiwa leo kueleza anachoita ‘maamuzi magumu’.

Kutupiana mpira kulijitokeza jana baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kusema Bunge linasubiri taarifa rasmi ya kufukuzwa uanachama kwa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kutoka NEC, ambayo hata hivyo, nayo ilisema inasubiri taarifa kutoka Chadema huku chama hicho kikisema kinashughulikia kwanza kesi zinazowakabili wanachama wake wanaotuhumiwa kumpiga aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa.
Wakati Makinda akieleza hayo, taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa mbunge Zitto zilieleza kuwa leo ataibuka bungeni kwa nia ya kuwaaga wabunge kama alivyoahidi wiki iliyopita. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

'KURA YA MAONI IPO PALE PALE'

Kaimu kiongozi wa shughuli za serikali bungeni Mh. Samuel Sitta.
SERIKALI imesema haiwezi kubadili msimamo wake kuhusu upigaji wa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, licha ya kuwepo maoni ya viongozi wa dini ambao wanataka jambo hilo lisitishwe.

Kaimu Kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni, Samuel Sitta alisema jana mjini hapa kuwa pamoja na kuwepo kwa tofauti kati ya Jukwaa la Wakristo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, msimamo wa Serikali uko pale pale.

Sitta, ambaye anakaimu shughuli za serikali bungeni kutokana na kutokuwepo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema Serikali inakubaliana na maoni ya Kardinali Pengo kuwa waumini waachwe waamue wenyewe kuhusu Katiba Inayopendekezwa.

Alisema kama viongozi wa dini wamegawanyika hakuna namna ya kuwafanya wawe na kauli moja, lakini akasisitiza kuwa jambo la msingi ni kuachwa kwa mtu aamue mwenyewe aina ya kura atakayopiga.

Hivi karibuni Pengo alitofautiana na Baraza la Maaskofu (TEC) na Jukwaa la Wakristo ambao wanataka upigaji wa kura ya maoni usitishwe, kwa maelezo kuwa wananchi hawajapewa muda wa kuisoma na kuielewa katiba hiyo na kama Serikali itang’ang’ania ni vyema waumini wa kanisa wapige kura ya hapana. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO MARCHI 18, 2015

.
.
.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAASKOFU WA JUKWAA LA WAKRISTO WAMEKOLEZA MOTO KUIKATAA KATIBA

Pichani ni  Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri la Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa

Gazeti la Mwananchi la Machi 13, 2015 lilibeba ujumbe mzito kwa Watanzania. Kichwa cha habari kimoja kilisomeka: “Maaskofu: Pigieni Katiba kura ya hapana.”
Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo ambao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT) Askofu Daniel Awet, kwa sauti moja wamewataka waumini wao kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Wapigakura, kuisoma vyema Katiba Inayopendekezwa na hatimaye kuikataa kwa kuipigia kura ya ‘hapana.’
Sababu kuu za kuwahamasisha waumini wao na Watanzania kuikataa Katiba Pendekezwa ni mbili. Mosi ni kulazimisha kura ya maoni ya katiba mpya kufanyika bila maandalizi ya kutosha, yakiwamo maridhiano ambayo yameligawa Taifa katika vipande vipande. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

AL SHABAAB YAUA WATU WATATU NCHINI KENYA

Alshabaab
Maafisa wa polisi nchini Kenya wanasema kuwa takriban watu watatu wameuawa katika mji wa kazkazini wa Wajir, yapata kilomita 100 kutoka mpaka na Somalia. Watu waliofunika nyuso zao walishambulia duka moja na kufyatua risasi, kulirushia magurunedi kabla ya kulichoma.

Kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab limeongeza mashambulizi yake kazkazini mashariki mwa Kenya katika siku za hivi karibuni ,na kufanya mashambulizi mawili katika mji wa Mandera ambao una pakana na Somali.

Kundi hilo linadhibiti eneo kubwa la Somalia la mashambani na limesajili idadi kubwa ya raia Wakenya. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

MAKAMU WA RAIS WA S LEONE AFUTWA KAZI

Rais wa Sierra Leone Ernest Koroma kushoto na makamu wake Sam Sumana Kulia
Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi makamu wa rais kwa kutafuta hifadhi katika ubalozi wa kigeni nchini humo. Siku ya jumamosi ,Samuel Sam Sumana amesema kuwa alimtaka balozi wa Marekani kumpatia hifadhi ndani ya ubalozi wa Marekani nchini humo akihofia maisha yake.

Awali wanajeshi waliizunguka nyumbani yake na kumpokonya silaha mlinzi wake .
Kumekuwa na wasiwasi kati ya rais na bwana Sam Sumana. Hivi majuzi aliondolewa katika chama tawala cha All People Congress kwa udanganyifu na kuchochea ghasia. Hatahivyo amekana madai hayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

MONACO HAWAKUSTAHILI KUSONGA MBELE

Arsene Wenger,meneja wa klabu ya Arsenal.
Meneja wa klabu ya soka ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger anaamini timu ya Monaco haikustahili kusonga mbele kwenye hatua ya nane bora ya ligi ya mabigwa ulaya.
Licha ya Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Monaco walishindwa kufuzu kwa nane bora baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kuchapwa 3-1.

Kocha Wenger amesema haamini kama timu hiyo ilitakiwa kusonga mbele “ukiangalia idadi ya mashuti yaliyolenga goli utashangaa, kupoteza mchezo kunauma ila hatujapoteza."
Hii imekua ni mara ya tano mfululizo kwa washika bunduki hao wa London kushindwa kufuzu hatua ya nane bora. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SERENA WILLIAMS ATINGA NANE BORA

Serena Williams
Nyota wa mchezo wa tenesi Serena Williams ametinga katika hatua ya nane bora ya michuano ya BNP huko Indian Wells. Serena amefanikiwa kufanya vizuri kwa kumshinda Sloane Stephens anayeshika nafasi ya 33 kwa ubora wa dunia kwa seti 6-7 (7-3) 6-2 6-2,
Sloane alipoteza mchezo huu baada ya kushindwa kuhimili mikiki miki ya mpinzani wake aliekua anacheza kwa juhudi kubwa.

Williams alikataa kucheza hapo baada ya kufanyiwa vitembo vya kudharauriwa mwaka 2001. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Monday, March 16, 2015

WAHAMIAJI 64 KUTOKA ETHIOPIA WAKAMATWA

Ramani ya Tanzania
Polisi mkoa wa Dodoma nchini Tanzania wanawashikilia wahamiaji haram 64 raia wa Ethiopia, huku mmoja wao akipatikana akiwa amekufa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amenukuliwa akisema wanamshikilia dereva wa gari lililokuwa limewabeba watu hao ambao inaaminika walikuwa njiani kuelekea kusini mwa Afrika.
Hii si mara ya kwanza kwa wahamiaji wa aina hiyo kukamatwa katika mazingira hayo.
Mwaka 2012 watu 42 kutoka Eritrea walikutwa wamekufa katika lori mkoa wa Dodoma kwa kile kinachosemekana ni kukosa hewa kutokana na kufichwa ndani ya lori hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAMILIONI WAANDAMANA BRAZIL

Rais Dilma Roussef wa Brazil
Zaidi ya watu milioni moja kutoka nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff, huku wengi wao wakitaka rais huyo afunguliwe mashtaka ya ufisadi mkubwa uliofanyika katika shirika la mafuta la serikali, Petrobras.
Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingi ya Brazil ikiwemo mji mkuu wa nchi hiyo Brasilia.
Maandamano makubwa kabisa yamefanyika katika mji wa Sao Paulo ambalo ni eneo la upinzani waliokuwa wakipita mitaani.
Mmoja wa waandamanaji Francisco Pestana alilalama akisema"Dilma hana uwezo wa kuongoza nchi yetu. Tunachokabiliwa nacho ni bahati mbaya sana, namna mamabo yanavyokwenda, yanaweza kuelekea kubaya zaidi, tutakuwa Venezuela nyingine."
Naye mwandamanaji mwingine mwanamke Janaina Lima anasema "leo ni maandamano ya watu. Watu wamejitokeza mtaani kusema hakuna ghasia zaidi, hakuna rushwa, hakuna uvivu zaidi, hakuna uzembe zaidi, hakuna utawala mbaya. Na kuunga mkono Brazil mpya." Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

YANGA YAIADHIBU PLATNUM YA ZIMBABWE 5-1

Kikosi cha Yanga kilichoisambaratisha Platnum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1
Timu pekee iliyobakia kwenye mashindano ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika kutoka Tanzania, Yanga, imeendelea kuweka matumaini hai ya kusonga mbele baada ya kuiangushia kipigo kikali timu ya Platnum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1.
Mchezo huo wa raundi ya kwanza ya vilabu vinavyoshiriki Kombe la Shirikisho la CAF, ulifanyika Jumapili jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa kufungana mabao 2-1.
Kipindi cha Pili ndicho kilichokuwa kiama chya Platnum baada ya kuruhusu mabao matatu zaidi.
Wafungaji wa timu ya Yanga ni Mrisho Ngasa aliyefunga magoli mawili, Haruna Niyonzima, Salum Telela, na Amisi Tambwe walifunga bao moja kila mmoja. Kwa matokeo hayo Yanga imejenga mazingira ya kusonga mbele. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Sunday, March 15, 2015

ZITTO: IPO SIKU NITASHIKA NAFASI KUBWA TANZANIA

Wananchi wa Kijiji cha Nyalubanda wakiwa wamembeba Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alipowasili katika kijiji hicho jana katika hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa alilotoa ahadi katika kampeni za Uchaguzi wa mwaka 2010.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema kutimuliwa uanachama na Chadema ni dhoruba inayomkumba mwanasiasa yeyote anayefanikiwa na kwamba iko siku atashika “nafasi kubwa ya uongozi ya kuwatumikia Watanzania”.
Zitto aliwasili mjini hapa juzi, ikiwa ni siku chache baada ya Chadema kutangaza kumtimua uanachama kwa kosa la kupeleka mgogoro wa ndani ya chama kwenye mahakama.
Alifungua kesi Mahakama Kuu akitaka imuamuru katibu mkuu wa Chadema kumpa nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua madaraka yote na baadaye kukizuia chama hicho kumjadili. Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali shauri lake na Chadema ikatangaza mara moja kumtimua. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

PENGO ATOFAUTIANA NA MAASKOFU....!!!

 
Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akibariki matoleo yakiotolewa na Umoja wa Wanawake wa katoriki(WAWATA), wakati wa Ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam jana.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema waumini hawana budi kusoma vizuri na kuelewa Katiba Inayopendekezwa ili wakati ukifika, wafanbye uamuzi kwa hiari na utashi wao wakati wa kupiga Kura ya Maoni.
Ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku mbili baada ya Jukwaa la Wakristo kutoa tamko linalowataka waumini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura, kushiriki kikamilifu kwenye shughuli zote za elimu ya Katiba Inayopendekezwa na kupiga kura ya “hapana” kuikataa Katiba Inayopendekezwa.
Lakini jana, Kardinali Pengo alisema kuisoma na kuielewa katiba hiyo ndiyo wajibu wa msingi ambao Wakristo wanao kwa sasa ili kupiga kura inayostahili wakati ukifika. Kuhusu maaskofu kuagiza waumini waikatae Katiba Inayopendekezwa, Kardinali Pengo alisema wao wakiwa viongozi wa watu, hawana mamlaka wala uwezo huo, bali wenye uwezo ni wananchi wenyewe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

LIPUMBA AKUBALI TAMKO LA MAASKOFU

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba  

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba ameunga mkono tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kupinga Katiba Inayopendekezwa, akisema hoja zao ni za msingi kwa kuwa kuna mambo mengi yanayopingwa na wananchi.
Kauli ya Profesa Lipumba ni mwendelezo wa kauli tofauti zilizotolewa na watu mbalimbali kuhusu tamko la jukwaa hilo, wakiwamo wasomi, viongozi wa dini, wanaharakati na wanasiasa kuhusu hatima ya Kura ya Maoni na muswada wa Makahama ya Kadhi.
Alhamisi iliyopita, jukwaa hilo linaloundwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) liliwataka waumini wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, kushiriki kikamilifu katika elimu ya Kura ya Maoni, na kisha kuipigia kura ya “hapana” Katiba Inayopendekezwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...