Tuesday, October 14, 2014

MAASKOFU KATOLIKI WAUZUNGUMZIA USHOGA


Mkutano wa maaskofu Vatican
 
Makasisi wanaoshiriki katika mkutano wa maaskofu wanaangazia masuala ya mafunzo ya kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa kanisa hilo duniani kuwachukulia watu wenye mapenzi ya jinsia moja kwa usawa
Kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakati wa mkutano wa synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa mapema wiki hii.
Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa jamii zao.
Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WASICHANA WA CHIBOK NIGERIA BADO WANASHIKILIWA NA BOKO HARAM

Aliyekua kiongozi wa Boko Haram, Aboubakr Shekahu
Walikamatwa na kikundi cha kigaidi cha kiislam boko Haram kutoka shuleni kwao huko chibok. Ingawa kunaahadi nyingi kutoka serikali ya Nigeria kwamba wataokolewa na pia watapewa msaada kutoka dunia nzima lakini mpaka sasa bado hawajaonekana, ripoti ya mwandishi wa BBC Will Ross kutoka Lagos inasomwa na Regina Mziwanda
Miezi sita sasa na wasichana 219 bado wametekwa, ni ushaidi kidogo sana unaojulikana kwa kile kilichotokea kuhusu wao tangu walipoondolewa katika shule yao ya bweni huko chibok na boko haram, serikali ya Nigeria imepata wakati mgumu sio tu kuwaokoa lakini pia kwa kuonesha mwitikio mdogo wa umma..
Wazazi wa chibok wameiambia bbc kuwa wameachwa na maneno tu na ahadi zinazovunjwa kwamba watoto wao wa kike watarudi nyumbani hivi karibuni, baba mmoja amesema wanasiasa wamejikita kwenywe uchaguzi wa mwakani ujao zaidi yakuwaokoa watoto wao waliopotea.
Tangu mwezi April vijana wengi wa kike na wa kiume wametekwa nyara na kikundi cha kiislam cha Boko haram ambao wanaongoza mijini na vijijini karibu na mpaka wa Cameroon.
Serikali ya Nigeria imesema jeshi kwa sasa limepata mafanikio dhidi ya vita na boko haram lakini wamezidiwa nguvu kaskazini mashariki ambapo raia hawako salama na maelfu ya watu wamehama makazi yao katika wiki za hivi karibuni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YANGA WAWEKA KAMBI KUNDUCHI

Kuelekea kwenye mpambano wa watani wa jadi YANGA Vs SIMBA siku ya jumamosi Oktoba 18, kikosi cha timu ya Young Africans kimeingia kambini leo mchana katika hoteli ya Landmark iliyopo eneo la Kunduchi kujiandaa na mchezo huo ambao umeteka hisia za wapenzi wa soka nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kocha mkuu Marcio Maximo ameingia kambini na kikosi cha wachezaji 28 kujiandaa na mchezo huo ambapo kikosi chake kitakua kikifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko – Veterani kila siku kujweka fit kwa kuzisaka pointi tatu muhimu siku ya jumamosi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Monday, October 13, 2014

NDENJELA AZINDUA MABASI MAPYA YA KISASA NDENJELA JET

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akikata utepe kuzindua mabasi ya kisasa ya kampuni ya Mwaji Group  jijini Mbeya.
Ndani ya mabasi ya Ndenjela jet.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahamed Msangi wakifurahia maelezo mafupi toka kwa Mkurugenzi mtendaji    wa Mwaji Group Allan Mwaigaga. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LWAKATARE. DDP KUCHUANA UPYA LEO





Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare. PICHA|MAKTABA 


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare leo anatarajiwa kuchuana upya na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakati Mahakama ya Rufani itakaposikiliza maombi ya marejeo ya hukumu ya Mahakama Kuu iliyomfutia mashtaka ya ugaidi.

Maombi hayo Namba 5 ya mwaka 2014, yalifunguliwa na DPP akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kumfutia Lwakatare mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakimkabili yeye na mwenzake, Joseph Ludovick.

Katika maombi hayo, DPP anaiomba Mahakama ya Rufani iitishe majalada ya kesi hiyo na kuchunguza uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu kuwafutia washtakiwa hao mashtaka ya ugaidi na kisha ifute uamuzi huo wa Mahakama Kuu na amri zote ilizozitoa.

Pamoja na mambo mengine, DPP anadai kuwa haikuwa sahihi Mahakama Kuu kuamua kuwa mashtaka hayo hayakuwa halali, kwani hapakuwa na taarifa zilizowasilishwa dhidi ya washtakiwa ambazo Mahakama Kuu ingezizingatia katika kuamua uhalali wake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 13, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAALIM SEIF: TUTAZUNGUKA NCHI NZIMA KUPINGA KATIBA INAYOPENDEKEZWA


 
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake kitazunguka nchi nzima kupiga kampeni ili wananchi waikatae Katiba Inayopendekezwa.
Alisema watafanya hivyo kwa kuwa Katiba iliyopendekezwa imepoteza uhalali kwa vile theluthi mbili (ya wajumbe wa Zanzibar) inayodaiwa kupatikana haiwiani na takwimu za wabunge waliokuwamo ndani na nje ya Bunge na wale waliopiga kura ya hapana na kuwataka wananchi kuikataa wakati ukifika.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza Zanzibar, alisema hayo jana akihutubia mkutano wa hadhara wa kwanza tangu Katiba hiyo inayopendekezwa kukabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ikipendekeza mfumo wa Muungano wa serikali mbili badala ya tatu kama ilivyokuwa imependekezwa na rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na iliyokuwa Tume ya Marekebisho ya Katiba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MSOMI MKENYA PROFESA MAZURI AFARIKI

Profesa Mazuri alisifika sana kwa kuangazia tamaduni za kifarika kwa dunia nzima
Msomi mashuhuri wa Kenya,duniani Profesa Ali Mazrui ameaga dunia nchini Marekani.
Mazrui alikuwa msomi wa maswala ya kisiasa, utamaduni wa kiafrika na maswala ya dini ya kiisilamu.
Mazrui aliyekuwa na umri wa miaka 81 alifariki nchini Marekani ambako amaekuwa akiishi baada ya kuugua kwa mda mrefu.
Duru zinasema kuwa Profesa Mazrui atazikwa mjini Mombasa Pwani ya Kenya alikozaliwa.
Alitoa ombi la kutaka kusikwa Mombasa kabla ya kifo chake akisema angependa kuzikwa katika jumba la kihistoria la Fort Jesus.
Kabla ya kifo chake Marehemu Mazrui alikuwa anafunza katika chuo kikuu cha Binghamton mjini New York. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WAKILI DAMAS NDUMBARO ‘ ATUPWA JELA YA SOKA’ MIAKA SABA

ndumba
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchi TFF, imemfungia wakili Damas Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha pesa. Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa TFF, Ndugu, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam Tv.
Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.
Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu. Ndumbaro ambaye alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi amekanwa ‘ hadharani’ na vilabu huku vikisema kuwa ‘ havikumtuma’ kuzungumza yale ambayo alisema mbele ya vyombo vya habari. Klabu zimesema alizungumza kwa ‘ utashi’ wake mwenyewe, na si wao walimtuma.
‘ Kilichomuhuku’ ni yeye kutaka kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana. Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji ni kosa la kinidhamu. Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa hayo na kama angezungumza kwa niaba ya klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwa kwao, lakini yeye alijizungumzia tu kama vile alivyotaka iwe. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

AMRI KIEMBA AMEFIKISHA UJUMBE KWA PHIRI APANGWE KIKOSI CHA KWANZA, DAR-PACHA…!!!

20140913_160508
Simba SC itacheza na mahasimu wao Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika michezo mitatu iliyopita Simba haijapata ushindi, huku mahasimu wao wakiwa na pointi sita katika nafasi ya tatu ya msimamo. Yanga ni timu iliyokamilika kwa sasa, kwa maana ya kucheza kitimu, umoja na ushirikiano.
Screen Shot 2014-10-13 at 10.58.05 AM
Kabla ya safari ya Afrika Kusini, kikosi cha Simba kimeonekana kukosa ‘ utimamu wa mwili na akili’ kwa maana ya wachezaji wake kucheza mpira huku wakiwa na mambo yanayowasumbua, umoja, kiwango cha chini kutoka kwa baadhi ya wachezaji, majeraha, na ufiti wa mchezaji mmoja mmoja, kikosi cha Patrick Phiri kimekuwa katika ‘ majanga’ hayo, lakini kama, mwalimu hapaswi kutumia sababu hizo kufungwa na mahasimu wao ambao wanaingia katika mchezo wa tano mfululizo wakiwa katika ‘ umbo zuri’.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Sunday, October 12, 2014

MJUMBE WA NCCR AWATESA VIGOGO...!!!


“Kutokana na alichofanyiwa kwa kupigiwa kura bila huku akiwa hajafanya hivyo tumemwandikia barua IGP tukimwomba amwekee ulinzi (Hamis) kwani kwa siasa za Pemba (anakoishi Hamis) wanaweza kumdhuru.” PICHA|MAKTABA 

Siku moja baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi- Zanzibar, Haji Ambar Hamis kutoa tuhuma za ‘kupigishwa’ kura ya kupitisha Katiba inayopendekezwa bila ridhaa yake, uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba umethibitisha kuwapo kwa dosari hizo.
“Sikuwahi kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye kupitisha katiba hiyo. Ukweli ni kwamba nimeumia sana na hadi sasa sielewi hatma ya maisha yangu na usalama wa familia yangu kwa ujumla” alisema Hamis alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Akizungumzia tuhuma hizo za Hamis, Naibu Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Dk Thomas Kashililah alisema: “Kwa taarifa zetu hakupiga kura siku zote tatu za zoezi hilo. Jina lake katika orodha ya wapiga kura lilikuwa namba 63 na hakupiga kura.”
Alisema hata hivyo wakati wa kuondoa majina ya Wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wale ambao hawakushiriki jina lake lilisahaulika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NYARANDU: HAKUNA TEMBO ALIYEUAWA SELOUS HIVI KARIBUNI


Waziri wa Maliasili na Utaslii, Lazaro Nyalandu. PICHA|MAKTABA 

Serikali imesema vita vya kupambana na ujangili vinaonyesha mafanikio katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita na hakuna taarifa za kuuawa kwa tembo katika Pori la Akiba la Selous.

Waziri wa Maliasili na Utaslii, Lazaro Nyalandu alisema jana wakati akiaga wanafunzi zaidi ya 100 kutoka China na Tanzania Makao Makuu ya Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) waliokwenda kutembelea pori hilo kubwa kuliko yote barani Afrika kupata mafunzo ya uhifadhi.

Alisema baada ya serikali kuvalia njuga suala la ujangili wananchi wameelimika na sasa wamekuwa wakitoa taarifa za majangili ambazo zimesaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na ujangili.

“Baada ya Rais Jakaya Kikwete kukerwa na kukithiri kwa majangili tulianza mapambano na taarifa nilizonazo hadi hivi sasa kwa kipindi cha miezi mitatu hakuna tembo hata mmoja aliyekutwa ameuawa,”alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

POSHO ZA BUNGE ZAIBUA MAPYA


Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta. PICHA|MAKTABA

Siku chache baada ya Bunge la Maalumu la Katiba kumaliza muda wake, matumizi ya fedha zilizobaki kwenye Bunge hilo yameibua mvutano baada ya kuwapo taarifa kuwa fedha hizo ziliisha, huku Wizara ya Fedha ikieleza kuwa bado zipo.
Idadi ya wajumbe wa Bunge hilo kisheria ni 629 na wajumbe ambao hawakuhudhuria vikao vya Bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu, wanakadiriwa kufikia 140.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, aliwahi kukaririwa akiwaeleza wajumbe wa Bunge hilo kuwa fedha zitakazookolewa zitatafutiwa utaratibu badala ya kurudishwa zilikotoka.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad, alisema hakuna pesa zilizobaki na kwamba waliomba Serikali kuwaongezea fedha za siku nne zilizobakia kabla ya kukabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete Jumatano wiki hii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 12, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI ‘ YACHAPWA’ KWA MARA YA KWANZA NA POLAND

Poland imeifunga UJerumani kwa mara ya kwanza na kukwea juu ya kilele katika kundi la Nne kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Ulaya, Euro, 2016 nchini Ufaransa. Mabingwa wa dunia , Ujerumani ilikuwa na rekodi ya kucheza mara 18 mfululizo bila kupoteza mchezo wowote dhidi ya majirani zao, Poland ambao walipata mabao yote mawili katika kipindi cha pili.
Mshambulizi kinda wa klabu ya Ajax Amsterdam, Arkadiusz Milik, 20 alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 51, na dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo, Sebastian Mila aliwahakikishia wenyeji ushindi baada ya kufunga bao la pili katika mchezo huo uliopigwa jijini, Warsaw.
Mabingwa hao wa sasa wa dunia, walifungwa mara ya mwisho na Jamhuri ya Czech, Oktoba, 2007 katika michezo ya kufuzu. Ujerumani ilicheza michezo 33 ya kufuzu pasipo kupoteza. Kipa wa Ujerumani, Manuer Neur aliokoa mabao manne ya wazi katika mchezo ambao walishambuliwa sana. Poland iliyokuwa na mshambulizi wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ilipiga jumla ya mashuti 19, huku mashuti 12 yakilenga bao.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alikwenda Poland huku baaddi ya wachezaji wake muhimu wakikosekana. Ujerumani ilibanwa hasa na walimudu kufanya mashambulizi machache . Walipiga mashuti saba tu ambayo yote yalilenga lango lakini nyota wa mchezo huo, golikipa, Wojciech Szczesny alikuwa imara, kipa huyo wa klabu ya Arsenal aliokoa mara 14. Tomas Mueller, Andre Schurrle na Mario Gotze walishindwa kufunga kwa muda wote waliokuwa uwanjani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...