Friday, September 05, 2014

WATOTOMILIONI 120 WAFANYIWA UKATILI DUNIANI

Mtoto akijilia nyama
Umoja wa mataifa umetoa kauli kwamba wasichana zaidi ya milioni 120 duniani kote,sawa na msichana mmoja kati ya kumi atakua amaebakwa ama amewahi kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kabla hajatimiza umri wa miaka 20.
Kitengo cha umoja wa mataifa kinachoshughulikia masuala ya watoto UNICEF kimegundua mnamo mwaka 2012 pekee watoto na mabinti wapatao elfu tisini na watano waliuawa,wengi wao ni kutoka Marekani kusini na Caribbean.
Ripoti hiyo ya UNICEF iliangazia nchi zipatazo mia moja na tisini, na kusema kwamba duniani kote watoto wametendewa ukatili,mauaji na mashambulizi ya kingono ikiwemo kuonewa na uadabishaji watoto unaokiuka haki zao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Wednesday, September 03, 2014

SITTA AKANA KUTUMIA BUNGE LA KATIBA KUSAKA URAIS 2015, TAZAMA VIDEO

Wakati joto la Urais mwakani likizidi kuongezeka nchini, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta ameweka wazi kuwa hana nia ya kuwania Urais kwa kutumia kigezo cha kuongoza Bunge hilo maalum.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha thelathini na moja cha Bunge Maalum la Katiba ambalo limeanza kupokea taarifa za kamati zake, Sitta hata hivyo alisema atakuwa tayari kufanya hivyo kama wananchi wataona anafaa kwani wao ndio wenye dhamana ya kuchagua mtu wanayetaka awaongoza.
“Wengine wananikejeli, wanasema kwa shughuli hii naonesha sifai Urais, me sijaomba Urais,” alisema Sitta na kufuatiwa na idadi kubwa ya makofi bungeni hapo.
Sitta aliongeza: “Naifanya kazi hii kama Mwenyekiti wa Bunge la Katiba basi, lakini nasema wanaochagua ni wananchi, inawezekana mwakani, wananchi wa Tanzania wakatamani mtu mzima, aliyetulia na muadilifu, kama itakuwa hivyo wajue tupo na sisi wengine.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HARUSI YA KIPEKEE YAFANYIKA NDANI YA MAJI

Katika mtaa, mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza kufanyika hapa.
Biashara hii ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.
Duka lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding ...Biashara ndogo ambayo inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika historia ya nchi hii.
Kulingana na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.
Duka hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.
'Mtindo tofauti wa picha'
''Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, '' asema mmiliki wa duka hili Tina Liu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 03, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC_0041

DSC_0039
DSC_0042
DSC_0043 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

OBAMA KUONGEZA VIKOSI IRAQ

Rais Barack Obama
Rais Barack Obama wa Marekani ameidhinisha kupelekwa vikosi vya wanajeshi wapatao 350 kwa lengo la kuwalinda wanadiplomasia na wafanyakazi raia wa nchi hiyo waishio mji mkuu wa Iraq Baghdad.
Ikulu ya Marekani imesema wanajeshi hao watakaopelekwa baadhi yao ni wale wanaojihusisha na diplomasia ya ulinzi ya iraq ambao ni zaidi ya mia nane.
Hata hivyo Marekani inatarajia kuwatuma maofisa waandamizi akiwemo John kerry katibu mkuu wa marekani na Chuck Hagel katibu wa ulinzi ambao watakwenda mashariki ya kati katika harakati za kuimarisha ushirikiano.
Hatua hiyo inafuatia vitendo vya mashambulizi na mauaji yanayoendelea Iraq ikiwa ni matokeo ya utofauti kati ya Marekani na makundi ya wapiganaji ambao wamekuwa wakiwalenga raia wa Marekani waliopo nchini humo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MWANDISHI WA HABARI MWINGINE "ACHINJWA"


Mwandishi aliyechinjwa na IS Steven Sotloff
Wapiganaji wa dola ya Kiislam IS wamesambaza picha za video katika mitandao kwa lengo la kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia Marekani Steven Sotloff ambaye ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji hao.
Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwakajana.
Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley.
Wapiganaji hao wa katika picha hizo pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa Uingereza.
Baada ya mauaji ya mwandishi wa awali Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa Sotloff alitoa ombi maalumu kwa kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi kutoa muua mtoto wake.
Msemaji wa Ikulu ya White House Josh Earnest amesema kuwa maofisa wa Marekani wanaendelea na uchunguzi wa ripoti hiyo.
Marekani hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini Iraq.
Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC Frank Gardner amesema hatua hiyo ya wapiganaji wa IS ni kulipa kisasi kwa Marekani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Tuesday, September 02, 2014

SASA UKICHUKUA FEDHA BENKI ROHO MKONONI


Katuni inayoonyesha ujambazi wa kutumia pikipiki na bastola unavyoshika kasi jijini Dar es Salaam. 

Ni roho mkononi. Hayo ndiyo maneno matatu yanayofaa kuelezea hali ilivyo jijini Dar es Salaam na maeneo kadhaa nchini kwa sasa, hasa pale mtu anapobeba fedha nyingi.
Matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha yamekuwa sugu na kusababisha wananchi wanaopeleka au kutoa fedha benki kuvamiwa, kujeruhiwa au kuuawa mchana kweupe na majambazi wanaotumia pikipiki.
Wananchi wamekuwa wakihoji ni kwa jinsi gani majambazi hao hupata taarifa za mtu aliyekwenda benki ama kuweka au kuchukua fedha.
Mkazi wa Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Salum Mashati alisema: “Haiingii akilini, utasikia mtu kaporwa fedha akitoka benki. Eti majambazi wanasema kabisa toa hizo milioni 20, wanajuaje kuwa una kiwango hicho? Huenda watu wa benki wanashiriki uhalifu huu.”
Hata hivyo, meneja wa tawi moja la benki lililopo Mlimani City, ambaye hakupenda jina lake litajwe alikanusha madai hayo... “Si kweli kwamba benki zinashirikiana na majambazi kufanya uhalifu huu. Kwanza wahudumu (bank tellers) hawaruhusiwi kuingia na simu wanapohudumia wateja.
“Hata mteja anapoingia benki hukatazwa kuongea na simu au kuandika ujumbe. Mazingira tuliyojiwekea hayaruhusu kabisa mawasiliano kati ya benki yetu na watu wa nje wakati wa kazi. Nadhani vitendo hivi vya ujambazi vinaanzia kwa wateja wenyewe kutoa taarifa juu ya mipango yao kwa watu ambao si waaminifu,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JAY DEE "MAADUI ZANGU WAMEBADILISHA WIMBO"


Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee  

 Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee amedai kuwa maadui zake wamebuni njia mpya ya kumwangusha, baada ya zile za awali kutofanikiwa.
Katika waraka mrefu aliouandika katika mtandao wa facebook, Lady Jay Dee alisema watu wasiopenda mafanikio yake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kumwangusha, lakini hata hivyo wameshindwa.
Jay Dee analalamikia habari iliyoandikwa juu yake kuwa amekuwa katika uhusiano mpya na kijana aliyemzidi umri, jambo analosema halina ukweli.
Habari hiyo inahusishwa na kile kilichodaiwa kuwa mwanamuziki huyo ameachana na mume wake, Gadner G Habash, ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio Times FM. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NDEGE YA KENYA YAANGUKA TANZANIA


Masalia ya ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited iliyoanguka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuua watu watatu jana.
Ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited imeanguka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwateketeza watu watatu waliokuwamo ndani.
Ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-SXP iliruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumapili saa 1:26 usiku ikielekea Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) Kenya ambako ilitakiwa kutua saa 2:36 usiku.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Paschal Shelutete alikiri ndege hiyo kuanguka kwenye hifadhi hiyo na walikuwa katika harakati za kuitafuta.
Mkaguzi Mkuu wa Ajali za Ndege nchini, kutoka Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, David Nyamwihura alisema ajali hiyo ilitokea takriban maili 20 kutoka Serengeti, katika eneo la Kogatembe na watu wote watatu waliokuwamo wamefariki dunia.
Meneja wa Udhibiti wa JKIA, Clever Davor aliliambia gazeti la Daily Nation la Kenya kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada ya uwanja huo ikiwa imeruka angani urefu wa futi 14,000. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAM WAUTEKA MJI MUHIMU NIGERIA

Wanajeshi wa serikali ya Nigeria.
Kundi la Boko haram limefanya mashambulizi katika mji wa Bama na kusababisha mauaji ya watu wengi huku wengine wakitoroka.
Wanamgambo hao waliuteka mji wa Bama ,ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno siku ya Jumatatu baada ya jaribio la awali la kutaka kuuteka mji huo kuzimwa na vikosi vya serikali.
Akizungumza na BBC ,wakaazi wamethibitisha kuwa mji huo umetekwa na kundi hilo na kwamba maelfu ya watu sasa wameachwa bila makao.
Mamlaka ya Nigeria bado haijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Taarifa zinasema kuwa watu wengi wametoroka wakiwemo wanajeshi.
Zana za kivita zinazotumiwa na wapiganaji wa Boko Haram
Hapo awali jeshi la Nigeria lilitoa ripoti kuonyesha kuwa mpaka sasa limewaua wapiganaji 70 wa Boko Haram ,kutokana na mapigano kati ya kikundi hicho na wanajeshi Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Bama.
Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo kwa magari ya kivita.Taarifa kutoka katika mji huo zinaeleza kwamba mashambulizi yalianzishwa na vikosi vya jeshi la Nigeria.
Msemaji wa kundi hilo la Boko Haram ameelezea hali ya mji huo kwa sasa kuwa wakaazi wa mji wa Bama wamekimbilia katika mji mwingine wa Borno na Maiduguri .
Nalo shirika la Amnesty International limetoa takwimu kuwa raia wapatao milioni nne wamekufa mwaka huu katika mgogoro huo kati ya Boko Haram na vikosi vya ulinzi vya Nigeria.

KIONGOZI WA AL-SHABAB ASHAMBULIWA

Haijulikani ikiwa Ahmed Abdi Godane aliuawa kwenye shambulizi hilo
Wanajeshi wa Mreakani wamefanya mashambulizi ya angani dhidi ya msafara wa magari ya mmoja wa viongozi wa kundi la Al Shabaab nchini Somalia.
Haijulikani ikiwa kiongozi wa kundi hilo, Ahmed Abdi Godane aliuawa kwenye shambulizi hilo lililofanyika umbali wa kilomita 240 kusini ya mjini mkuu Mogadishu.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa wanajeshi wa Marekani walionekana wakishuka katika eneo hilo kwa helikopta na kuchukua miili ya wapiganaji waliouawa.
Msemaji wa idara ya ulinzi ya Marekani, (Rear Admiral John Kirby) alisema bado inadurusu matokeo ya shambulizi hilo.
Baadhi ya taarifa zinasema kuwa wapiganaji waliwakamata wakazi walioshukiwa kutoa taarifa kwa Marekani.

Na BBC

Thursday, August 28, 2014

TUHUMA NZITO KWA MAWAZIRI


 “Tunalipa wajumbe wanaohudhuria bungeni, kama hilo linatendeka lazima nilifuatilie. Ninachosema kama kuna waziri amelipwa na hayupo itabidi aturejeshee hiyo fedha. Lakini hili tatizo ni gumu kwa sababu mtu analipwa na tunajua yupo kumbe pengine hajaingia katika vikao,”

Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limedai kuwa baadhi ya mawaziri na manaibu wao wamekuwa wakilipwa posho za kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu la Katiba hata wanapokuwa hawapo bungeni.

Kaimu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda alisema jana: “Mawaziri na manaibu ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioko mjini Dodoma wanapokuwa na safari za kikazi huaga kwa Waziri Mkuu lakini jambo la kushangaza ni kuendelea kulipwa posho wakati hawapo.”

Alisema hali hiyo husababisha Bunge hilo kuendelea kuwalipa posho kupitia akaunti zao za benki lakini wakiwa hawapo Mjini Dodoma. Mwakagenda alisema mawaziri hao wanapotoka kwenda kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali nako hulipwa posho. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MTOTO WA MIAKA 9 AMUUA MWALIMU WAKE KWA BUNDUKI

Screen Shot 2014-08-28 at 7.07.03 AM
Hiki ni kipande cha video ya mfunzo hayo kabla ya tukio.

Unaweza kushtushwa na umri mdogo wa mtoto mwenyewe aliekua anafundishwa kufyatua risasi kwenye bunduki, hii imetokea Arizona nchini Marekani ambapo mtoto wa miaka 9 ndio kichwa cha habari kwenye mafunzo ya kutumia submachine gun iliyotengenezwa Israel.
Mtoto huyu wa kike anaetokea New York alikua kwenye mapumziko na matembezi kama mtalii kwenye mji wa Arizona ambako pia ndio alichukua time yake ya ziada kujifunza kutumia bunduki lakini kwa bahati mbaya risasi ikafyatuka na kumjeruhi mwalimu wake aitwae Charles Vacca mwenye umri wa miaka 39 ambae alifariki baadae hospitalini.
Screen Shot 2014-08-28 at 7.34.27 AM 
Wakati tukio linatokea mtoto huyu alikua na wazazi wake ambapo tovuti ya bullets and burgers imesema watoto kati ya miaka 8 na 17 wanaweza kufyatua risasi kama iwapo tu watakua chini ya uangalizi wa Mzazi au Mwalimu.
Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili, ilishawahi kutokea mwaka 2008 ambapo mtoto wa miaka 8 alijiua kwa bahati mbaya kwa risasi kwenye onyesho la bunduki hukohuko Marekani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANAWAKE WA BAWACHA WAMCHUKULIA FOMU HALIMA MDEE


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (kushoto) akifuta machozi huku akiwa ameshika fomu za kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Bazara la Wanawake wa Chadema (Bawacha) alizokabidhiwa na baadhi ya wanakwake makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam  jana. 


Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya jana baadhi ya wanawake kujitokeza kumchukulia fomu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

Mbunge huyo anaungana na Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao na wanachama wengine, Lilian Wasira na Sophia Mwakagenda ambao nao wamesharejesha fomu kuwania nafasi hiyo inayoshikiliwa na Suzan Lyimo.

Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Agosti 30 na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MACHIFU WAOMBA UTAWALA WAO UREJESHWE


Makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samia Hassan Suluhu (kulia) akimsikiliza mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Machifu Tanzania, Chifu John Mgemela wa Magu (katikati) na Chifu Ndutu Ndaturu wa Bariadi waliotembelea ofisini kwake bungeni Dodoma juzi kutaka mapendekezo yao umoja huo yaingizwe kwenye Katiba mpya. 


Umoja wa machifu nchini juzi uliwasilisha mapendekezo yao katika Bunge la Katiba ukitaka yaingizwe kwenye Katiba inayotungwa.

Machifu hao wamependekeza kurudishwa kwa utawala wa Kichifu na Kitemi ili kutoa nafasi ya kurekebishwa kwa jamii ambayo kwa maoni yao imeanza kupoteza mwelekeo.

Mapendekezo ya viongozi hao wa jadi, yalipokelewa na makamu mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan ambaye aliwaahidi kuyafanyia kazi.

Wakizungumza mbele ya vyombo vya habari jana, Chifu John Mgemela wa Magu na Agnes Ntuzu wa Bariadi, walisema maoni hayo yalitokana na mapitio ya Rasimu ya Katiba inayoendelea kuboreshwa na Bunge hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

“Tunataka Katiba ieleze wazi kuwa sera na sheria zitakazotungwa zihakikishe kunakuwa na tume ya taifa ya utamaduni itakayoanzishwa kisheria kusimamia masuala ya utamaduni,”a lisema Chifu Mgemela.

Alisema ni vyema Katiba ijayo ikatoa fursa kwa machifu na watemi kutambulika katika mfumo rasmi wa uongozi wa jamii, ili wasaidie kudhibiti mwenendo wa jamii ambao kwa sasa umepoteza mwelekeo kimaadili.

Akipokea mapendekezo hayo, Suluhu alisema ingawa Bunge hilo halifanyi kazi ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya kukusanya maoni, hawawezi kukataa kuwapokea wananchi wanaopeleka mapendekezo yao.

Alisema muda mfupi baada ya kukutana na machifu hao, ratiba ilikuwa inaelekeza kuwa kamati ndogo ya uongozi wa Bunge hilo ikutane na miongoni mwa kazi ambazo zingefanywa ni kujadili mapendekezo yaliyopokelewa.

Alisema ikiwa mapendekezo hayo yatakubalika, maoni hayo yatawasilishwa kwenye kamati zote za Bunge hilo zinazoendelea kupitia na kujadili Rasimu ili yafanyiwe kazi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...