Thursday, August 28, 2014

TUHUMA NZITO KWA MAWAZIRI


 “Tunalipa wajumbe wanaohudhuria bungeni, kama hilo linatendeka lazima nilifuatilie. Ninachosema kama kuna waziri amelipwa na hayupo itabidi aturejeshee hiyo fedha. Lakini hili tatizo ni gumu kwa sababu mtu analipwa na tunajua yupo kumbe pengine hajaingia katika vikao,”

Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limedai kuwa baadhi ya mawaziri na manaibu wao wamekuwa wakilipwa posho za kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu la Katiba hata wanapokuwa hawapo bungeni.

Kaimu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda alisema jana: “Mawaziri na manaibu ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioko mjini Dodoma wanapokuwa na safari za kikazi huaga kwa Waziri Mkuu lakini jambo la kushangaza ni kuendelea kulipwa posho wakati hawapo.”

Alisema hali hiyo husababisha Bunge hilo kuendelea kuwalipa posho kupitia akaunti zao za benki lakini wakiwa hawapo Mjini Dodoma. Mwakagenda alisema mawaziri hao wanapotoka kwenda kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali nako hulipwa posho. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz


“Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma, mawaziri na manaibu wanalipwa posho hata wanapokuwa nje ya Bunge Maalumu la Katiba, wanaposafiri pia wanalipwa posho na Serikali,” alisema Mwakagenda.

Alisema pamoja na kwamba Ofisi Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba imeonyesha kubana mianya kwa wajumbe kusaini bila kufanya kazi, bado kuna ufujaji wa fedha eneo la mawaziri.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema ruhusa za kutoka nje ya Dodoma hutolewa na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta na kwamba wasiohudhuria huwa hawalipwi.

“Tunalipa wajumbe wanaohudhuria bungeni, kama hilo linatendeka lazima nilifuatilie. Ninachosema kama kuna waziri amelipwa na hayupo itabidi aturejeshee hiyo fedha. Lakini hili tatizo ni gumu kwa sababu mtu analipwa na tunajua yupo kumbe pengine hajaingia katika vikao,” alisema.

Alisema kanuni za Bunge hilo zinataka mjumbe anapoondoka aombe ruhusa kwa Mwenyekiti wa Bunge na nakala kwa Katibu.

“Wakicopy (wakinakili) kwangu mimi nawaorodhesha nampelekea mhasibu, tukikaribia kulipa namwambia hawa hawapo, kwa hiyo mtu siku ambazo anaomba ruhusa hata kama anaumwa hatumlipi, labda awe amelazwa hospitali ambaye tunamlipa half (nusu),” alisema.

Hata hivyo, alisema tatizo linalowapa shida kiutendaji ni kwa wale wasioaga wanapotoka nje ya Dodoma na kwamba hilo atalifuatilia kwa kuangalia orodha za mahudhurio kwenye vikao.

Mahudhurio hafifu

Kuhusu mahudhurio Hamad alikiri kwamba hilo ni tatizo kutokana na baadhi ya wajumbe kutokuwa makini na kwamba mahudhurio hafifu yanaathiri uendeshaji wa vikao hivyo.
“Kama leo nilikwenda katika kamati nikawaambia kama haupo ni haupo tu, wengine wakasema unajua wengine walikuwa wanaumwa, nikawaambia mimi najua hiyo ni luck of seriousness tu (kukosekana kwa umakini), hakuna lingine. Wakanitaka niombe radhi lakini mimi nikawaambia wala siombi radhi... Umakini mdogo... Unakuta wengine wanajadili na wengine wanaathiri kura kwa uzembe tu, nafikiri kama kila mtu angekwenda katika vikao tusingekuwa na shida.”
Mwakagenda alisema katika wiki mbili zilizopita, mahudhurio yamekuwa madogo katika vikao vya kamati za Bunge.
Alisema Bunge hilo limesema wajumbe 441 wanahudhuria vikao hivyo lakini uchunguzi wa Jukata umeonyesha baadhi yao wamekuwa wakisaini tu kitabu cha mahudhurio.
Mwakagenda alisema uchunguzi huo ulionyesha kwamba wajumbe 100 hawahudhurii kwenye kamati.
Aidha, alisema kitendo cha Bunge hilo kuendelea kupokea maoni ya makundi mbalimbali ya kijamii ni kwenda kinyume na Sheria ya Mabadiliko ya Kifungu namba 9 (1) ambacho alisema kinaeleza kwamba kazi ya kukusanya maoni ni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...