Wednesday, December 25, 2013

HILI NDILO BARAZA LA MAWAZIRI LINALOTAKIWA


Rais Kikwete. 
********
Baada ya kizaazaa cha wiki iliyopita ambapo mawaziri wanne walipoteza kazi zao kutokana na kuwajibishwa kwa vitendo vya ukatili na mauaji vilivyotokea wakati watendaji katika wizara zao walipokuwa wakiendesha ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’ nchi nzima, kinachosubiriwa na wananchi hivi sasa ni Rais Jakaya Kikwete kuunda Baraza jipya la Mawaziri.
Kutokana na udhaifu mkubwa katika utendaji ambao kwa muda mrefu umeonyeshwa na mawaziri wengi katika Baraza la Mawaziri, hatudhani kama kuna mwananchi hata mmoja  anayemtarajia Rais Kikwete kujaza tu nafasi za mawaziri aliowafukuza wiki iliyopita.
Nderemo na vifijo vilivyotokana na furaha ya wananchi katika kila kona ya nchi baada ya mawaziri hao kuondolewa katika nyadhifa zao ni ishara tosha kwamba hawamtarajii Rais Kikwete kuishia hapo, isipokuwa kuwaondoa mawaziri wengine wengi ambao tayari wamethibitika na hata kutajwa na chama chao cha CCM kuwa ni ‘mawaziri mizigo’.

KHERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA KWA WADAU WOTE WA JAMBO TZ

Tunapenda kuwatakia kheri ya Chistmas na Mwaka mpya wapenzi wasomaji wa blog hii na page yetu ya facebook.

WaTanzania hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu na upendo miongoni mwetu kwa gharama yeyote ile na bila kuyumbishwa au kutetereka ili  tuweze kuachia vizazi vyetu vijavyo Urithi ulio mwema kuliko wowote Ule. TANZANIA yenye Amani, Upendo na Utulivu.
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"

HII NDIO KADI YA CHRISTMASS TOKA KWA MHE. EDWARD NGOYAI LOWASSA KWENDA KWA WATANZANIA WOTE

Tafadhari Like ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO YA X-MASS DESEMBA 25, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.



 

.

Tuesday, December 24, 2013

SOMA TAARIFA KUHUSU BEI MPYA ZA UMEME ZITAKAZOANZA KUTUMIKA TAREHE 1 JANUARI 2014

tanesco
Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.
Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.
Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.


Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. 
Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).

HII HAPA TAARIFA RASMI YA KUFUKUZWA KOCHA WA YANGA ERNST BRANDTS


Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.

WANAMUZIKI WA KUNDI LA PUSSY RIOT WAACHIWA HURU

Wanamuziki wote wa kundi la muziki wa Punk la Pussy Riot la nchini Russia wameachiliwa huru kutoka gerezani chini ya sheria ya msamaha.
Nadezhda Tolokonnikova aliachiwa huru kutoka hospitali moja ya gereza lililopo Siberia, wakati mwenzake Maria Alyokhina aliachiliwa huru Jumatatu huko Nizhny Novgorod.
Wote wameuita msamaha huo kuwa ni sawa na sarakasi za serikali za kujisafisha kabla ya kufanyika kwa michezo ya olimpiki ya majira ya joto itakayofanyika Russia Februari mwakani.
Wanawake hao wanamuziki walifungwa Agosti 2012 baada ya kuimba nyimbo inayokejeli katika kanisa kuu jijini Moscow.
Kitendo chao kilitafsiriwa kama kumkufuru mungu na wananchi wengi wa Russia lakini kutiwa kwao hatiani kwa kosa la utukutu ukichochewa na chuki dhidi ya dini ulishutumiwa na vikundi vya kutetea haki za binadamu, wanaharakati wanaompinga Rais Vladmir Putin na mataifa ya nje.
Watu wengi wanaotumikia vifungo wanauona msamaha huo kama jaribio la Rais Putin la kusafisha taswira yake katika nchi za magharibi na kuiboresha rekodi yake ya haki za binadamu kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki huko Sochi Februari 2014.
Siku mbili baada ya sheria hiyo ya msamaha kuanza kutumika, Rais Putin alimsamehe Mikhail Khodorkovsky, ambaye siku za nyuma alikuwa ni mtu anayeongoza kwa utajiri nchini Russia na mkosoaji binafsi wa sera za serikali, hatua ambayo pia ilitafsiriwa kama kuyaridhisha mataifa ya magharibi.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 24, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA

Sunday, December 22, 2013

MWIGULU NCHEMBA AMWONYA SPIKA WA BUNGE


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba, amemwonya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuacha kutumia vibaya fedha za Serikali kwa kuwapa posho wabunge kwa ajili ya kwenda kwenye michezo nje ya nchi.
Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa bidhaa ya mwaka 2013 iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salumu.
Mkuya katika maelezo yake alisema kuwa kodi hiyo imefutwa kwa laini za simu kwa mtu mmoja mmoja na badala yake imeongezwa katika kodi kutoka asilimia 14.5 hadi asilimia 17.
Katika mchango wake, mbunge huyo alionya kuwa kumekuwa na tabia ya kutumia vibaya fedha za umma jambo alilosema linaanzia ndani ya bunge.

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MWENYEKITI WA YANGA YUSUPH MANJI BAADA YA KUFUNGWA NA SIMBA JANA


Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.

DUUUUUH...!!! WASANII WETU MIZINGUO TU, ANGALIA MAKOSA KWENYE MOVIE MPYA YA RAY


kwenye scene hii anaonekana camera man kwa mbali ukiangalia kwenye viio vya nyumba io ni baada tu ya wazee wao kurudi kutoka Zanzibar 
....

MAN UNITED YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI ENGALND, LIVERPOOL NAO KAMA SIMBA SC, YAUA 3-1 SUAREZ APIGA BAO MBILI

article-2527121-1A3CB4FD00000578-469_634x428_876c6.jpg
Adnan Januzaj akishangilia baada ya kuifungia Manchester United dhidi ya West Ham
Manchester United imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi ya nne mfululizo, baada ya jana kuilaza West Ham mabao 3-1 Uwanja wa Old Trafford.
Danny Welbeck alifunga bao la kwanza nyumbani tangu Oktoba 2012 dakika ya 26 na Adnan Januzaj akafunga la pili dakika ya 36 kabla ya Ashley Young kumaliza kazi kwa bao la dakika ya 72 na Carlton Cole akaifungia West Ham bao la kufutia machozi dakika ya 81.

KWA UPANDE WA LIVERPOOL article-2527114-1A3C51FE00000578-586_634x433_3b6f0.jpg
Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Cardiff Uwanja wa Anfield jana.
MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameendeleza makali yake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Liverpool wa 3-1 dhidi ya Cardiff jioni hii Uwanja wa Anfield.
Nyota huyo wa Uruguay alifunga mabao yake katika dakika za 25 na 45, wakati bao lingine la Liverpool lilifungwa na Raheem Sterling dakika ya 42 wakati bao la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Jordon Mutch.
Ushindi kama huo imepata Simba SC nchini Tanzania jana wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC na Mrundi Amisi Tambwe akifunga mabao mawili moja Awadh Juma.
 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu click neno Jambo Tz kisha like page

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 22, 2013

..

ASKARI WA MAREKANI WAJERUHIWA BOR

131217114544_south_sudan_304x171_reuters_nocredit_045bc.jpg
Jeshi la Marekani linasema kuwa wanajeshi wake wane wamejeruhiwa Sudan Kusini pale ndege yao ilipopigwa risasi karibu na mji wa Bor, wakijaribu kuwahamisha raia wao.
Ndege kadha zililazimika kurudi Uganda.
Jeshi la serikali ya Sudan Kusini linajaribu kuukomboa mji wa Bor, kaskazini ya mji mkuu, Juba, kutoka wanajeshi walioasi na kujiunga na makamo wa rais wa zamani, Riek Machar ambaye aliuteka mji huo Jumatano.
Siku hiyo pia Marekani ilipeleka wanajeshi 45 kuwalinda raia na mali ya Marekani Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa gazeti la taifa la Uganda, New Vision,ndege mbili za jeshi la Uganda pia yalinasa katika tukio hilo.
Pamekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kutoka Sudan Kusini kwamba ndege za Uganda piya zimekuwa zikiisaidia serikali kuukomboa mji wa Bor kutoka kwa wanajeshi walioasi - taarifa ambazo zinakanushwa na nchi zote mbili.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...