Saturday, March 02, 2013

PINDA AZINDUA TUME NA KUSEMA: TUSAIDIENI KUTAFUTA KIINI CHA KUSHUKA KWA ELIMU


Waziri Mkuu akihutubia leo asubuhi



Azindua tume ya watu 15, aipa wiki sita kukamilisha kazi


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa
matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na
kuwataka wajumbe wa Tume hiyo watafute kiini cha mserereko wa kushuka kwa
ufaulu kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumamosi, Machi 2, 2013) wakati akizungumza na wajumbe
wa Tume hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es
Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk. Shukuru Kawambwa.

“Nimetafuta takwimu za tangu mwaka 2005, Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani na
kubaini kuwa tangu wakati huo hadi mwaka 2009 tulikuwa tukifanya vizuri, lakini
kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 matokeo yamekuwa yakishuka sana,” aliwaambia
wajumbe wa Tume hiyo na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.

Alisema hali hiyo haikuwa kwenye shule za sekondari za umma (kata) peke yake bali hata
kwa shule za Serikali, za watu binafsi na kwenye seminari ambazo kwa miaka
mingi zimekuwa na sifa ya kufanya vizuri kuliko shule za kawaida.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...