Tuesday, December 17, 2013

JAMAA AISHI KWENYE HANDAKI MIAKA MINNE...!!!


 
Stori: Makongoro Oging’
DUNIA haiishi vituko! Chacha Makenge (36) mzaliwa wa Kijiji cha Kisangula, Mtukula, Serengeti mkoani Mara anaishi jijini Dar lakini ndani ya handaki aliloligeuza chumba kwa miaka minne sasa, ni ajabu lakini ni kweli.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni nje ya handaki hilo lililopo mita chache kutoka majengo ya biashara ya Mlimani City, Makenge alisema alichukua uamuzi huo baada ya rafiki yake (jina linahifadhiwa) kumchomea nyumba na kuteketeza samani zote.

“Ilikuwa mwaka 2009 mwanzoni rafiki yangu huyo ndiye alinipa sehemu ya kiwanja chake nijenge nyumba. Nikawa naishi hapo huku nikiendelea na shughuli zangu za kila siku.

“Siku moja akabadili mawazo, akanitaka nihame katika eneo lake bila kunipa sababu, nilimwomba anipe muda nitafute pa kwenda.

“Julai 2009 akaja na polisi, akanikamata na kunipeleka Kituo cha Polisi cha Stakishari, nilipowauliza kosa langu, hawakunieleza.
“Baada ya siku mbili majirani walikuja kuniona na kuniambia kwamba nyumba yangu imechomwa moto na kila kitu kilichokuwa ndani kimeteketea, aliyefanya hivyo ni rafiki yangu. Nilijisikia vibaya sana.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 17, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

Monday, December 16, 2013

"KATIBA MPYA 2014 HAIWEZEKANI" LIPUMBA


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba (pichani) amesema mchakato wa Katiba Mpya una vikwazo vingi na kwamba Katiba haiwezi kupatikana mwaka 2014 kama Rais Kikwete alivyoahidi hivyo, kuna haja ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Bara.
              Hii ni mara ya pili kwa Lipumba kutoa kauli hiyo. Mei mwaka huu, alitoa tamko kama hilo alipoonyesha wasiwasi wake kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya akadai ni janja ya CCM kumwongezea muda Rais.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Lipumba alisema kuwa amekuwa akiutafakari kwa kina mchakato wa Katiba Mpya kama unaweza kukamilika mwaka 2014, lakini jibu linalomjia, hakuna.
Alitaja baadhi ya vikwazo ambavyo vinaweza kukwamisha kupatikana kwa Katiba Mpya kuwa ni Daftari la Kudumu la Wapigakura kama halijaboreshwa na kasi ndogo ya utoaji wa vitambulisho vya utaifa ambavyo vitatumika kupigia kura hiyo.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 16, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

ANGALIA MATUKIO YALIYOJILI JANA WAKATI WA MAZISHI YA MZEE MANDELA, QUNU AFRIKA KUSINI




Goodbye to an icon: Nelson Mandela's coffin is slowly lowered into the ground in the hills close to where he grew up at the small, private burial today in Qunu as military salute and mourners watch the poignant moment

Poignant: Nelson Mandela's coffin was carried to his grave and then the flag of the country he loved so ardently was removed and handed to his widow Graca Machel

United in grief: Mandela's widow Graca Michel and his ex-wife Winnie Mandela tearfully comforted one another as they sat next to president Jacob Zuma and Mandela's grandson Mandla as he was laid to rest

Special tribute: The South African air force fly over Mandela's grave in the hills of Qunu where he grew up, which was accompanied by a 21-gun salute


Friday, December 13, 2013

AZIMIO LA KUWANG'OA MAWAZIRI LAPITISHWA RASMI NA BUNGE...!!!


Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia.
********
Bunge limepitisha azimio la kuwataka mawaziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kujipima iwapo wanatosha kuendelea kuongoza wizara hiyo nyeti.
Azimio hilo lilipitishwa jana na wabunge kwa kura ya ndiyo bila kupingwa, baada ya kuhojiwa na Spika wa Bunge Anne Makinda iwapo wanaipokea taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Laac) iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake Rajabu Mbaruku.
Moja ya mapendekezo yake ni Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia na manaibu wake, Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa kujipima kama wanatosha kuendelea kuongoza wizara hiyo kutokana na kugubikwa na vitendo vya ufisadi.
Kwa mujibu wa taratibu za Bunge, taarifa ya kamati inapowasilishwa na kupitishwa pamoja na mapendekezo yake, huwa ni azimio kamili ambapo Serikali hutakiwa kutoa maelezo ya utekelezaji wake.
Kabla ya azimio hilo kupitishwa, Mwenyekiti wa Laac, Rajabu Mbaruku alijibu michango ya wabunge waliochangia katika taarifa ya kamati yake iliyowasilishwa Ijumaa iliyopita, akiwemo Waziri Ghasia.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 13, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.

KUMBE GRACA MACHEL NA WINNIE MANDELA NI MTU NA 'DADA YAKE'

https://www.facebook.com/jambotz

Winnie Madikizela-Mandela, (77) aliinama kumbusu Graca Machel (68), kabla ya kukaa katika kiti cha tatu kutoka kile alichokalia mwanamke huyo. Graca Machel alimwambia maneno machache ‘dada yake’ Winnie wakati akimbusu.
Wanawake hao wote wakiwa wamevalia majaketi meusi na vilemba, walikumbatiana kwa sekunde kadhaa huku Winnie akitabasamu na Graca akitazama mbele.
Wote wawili wanaheshimika nchini Afrika Kusini kutokana na sababu mbalimbali. Winnie anaheshimika kwa mchango wake mkubwa wa kupigania ubaguzi wa rangi; Graca kwa moyo wake wa kujitolea kumtunza kiongozi wao mpaka anafariki dunia.

Hata hivyo Winnie amekuwa akikosolewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ile ya kuruhusu wapinzani wake wauawe kwa kuchomwa moto wakitumia mafuta ya petroli na matairi ya magari.

ZITTO AWASHA MOTO MPYA CHADEMA...!!!



Siku moja baada ya kuwasilisha maelezo yake ya utetezi baada ya kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya Chadema, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe amekata rufaa Baraza Kuu kupinga hatua hiyo.


Zitto pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo walivuliwa nyadhifa zao na Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Novemba 20 na 21 jijini Dar es Salaam.


Akizungumza jana, Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando alitaja sababu mbili za kukata rufaa kuwa ni kukiukwa kwa taratibu za kuchukua hatua za nidhamu na sababu zilizotolewa kutokuwa sahihi.


Hata hivyo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema mambo hayo yalishatolewa ufafanuzi na chama na kwamba kukata rufaa ni haki ya kikatiba kwa mwanachama yeyote.


“Kukata rufaa ni haki ya kikatiba ya wanachama yeyote. Rufaa ikatwe tu, itashughulikiwa kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama. Hata hivyo, ieleweke, rufani inahusu kuvuliwa nafasi za uongozi, kusudio hilo haliwaondolei wajibu wa kujieleza kwa maandishi mbele ya Kamati Kuu kwa nini wasifukuzwe uanachama,” alisema Mnyika.

Thursday, December 12, 2013

DR. ASHA ROSE MIGIRO ALA KIAPO BUNGENI DODOMA LEO


PG4A9627
Mbunge wa Kuteuliwa , Dr. Asha Rose Migiro akiongozwa na Mpambe wa wa Bunge  na kusindindikizwa na badhi ya wabunge wa CCM kuingia Bungeni ili kuapishwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mjini Dodoma Desemba 12, 2013.
PG4A9630
Mbune wa Kuteuliwa , Dr. Asha Rose Migiro akiongozwa na Mpambe wa wa Bunge  na kusindindikizwa na badhi ya wabunge wa CCM kuingia Bungeni ili kuapishwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mjini Dodoma Desemba 12, 2013.

OPRAH WINFREY AELEZEA KWA NINI HANA WATOTO...!!!


Kwenye taarifa za hivi karibuni za Waandishi wa Hollywood, Oprah amefunguka juu ya kwa nini hana watoto na ukweli wa juu ya hali hiyo kutohusani na wanachohisi wengi kwamba hana uwezo wa kushika ujauzito huku akielezea kwa sababu kuu ni yeye kutaka kuwa mwanamke mwenye nguvu.

"Kama ningekuwa na watoto, watoto wangu wangenichukia. "Wangeishia kwenye hali ya kuniongelea kama ilivyo kwenye Oprah show; sababu kuna kitu katika maisha yangu kingeishia kuteseka na inawezekana kabisa wangekuwa wao. 
Gayle [King, rafiki wa karibu Winfrey ambaye ni mama wa watoto wawili] alikuwa ni aina ya mtoto ambaye, kwenye daraja la saba la darasa, alikuwa anaandika jina lake chini na majina ya watoto wake. 
Wakati alipokuwa na ndoto hizo za mchana, nilikuwa na ndoto za mchana juu vipi naweza kuwa Martin Luther King.

BASI LA BURUDANI LAPATA AJALI LEO HII MKOANI TANGA, WATU 12 WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA




Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.

Basi la Burudani leo limepata ajali kijiji cha Kwaluguru Kata ya Kwedizinga  wilayani Handeni, Imeripotiwa mpaka sasa watu zaidi ya 12 wamefariki na majeruhi zaidi ya 55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.

Hospitali ya wilaya ya Korogwe.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 12, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.


.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...