Saturday, July 20, 2013

SIKILIZA WIMBO WA MZEE MAGARI...!!!


Daaaah! Mzee Magari kweli kipaji kipo hebu chukua dakika chache kusikiliza wimbo huu afu dondosha comment yako.

AJALI MBAYA: KICHWA CHA MWANAMKE CHANASA KWENYE KIOO...!!!


Wakimtoa Dereva kwanza
Wakianza kumuokoa yeye
Hatimaye ameokolewa
Mwanamke mmoja raia wa China amenusurika kifo baada ya gari aliliokuwa amepanda kupata ajali mbaya iliyomsababishia yeye kunasa kakita kioo cha Mbele maeneo ya Jimbo la Guanxi, Mwanamke huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika alikuwa kashapoteza fahamu huku damu nyingi zikimtoka katika kioo hicho.

Juhudi za ziada zilifanywa na askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji kwa kukitanua kioo hicho kwa ustaadi mkubwa huku wakihakikisha hawamkati zaidi mwanamke huyo.

KIKOSI CHA WAASI NCHINI KONGO M23 CHAWEKA PICHA YA PASSPORT YA ASKARI WA JWTZ WALIYEMKAMATA ASUBUHI YA LEO AKISHIRIKIANA NA FDLR

m23-tanzania-twitterchristopher-george-yohana 

Waasi wa M23 wa DR Congo, wanadai kuwa wamemkamata askari wa Tanzania anayeitwa Christopher George Yohana, wakati akishirikiana na waasi wa Rwanda (FDLR) wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya Watusi mwaka 1994.

Waasi hao wa M23 wameweka picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. Kwa mujibu wa chimpreports.com,   M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47 yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook ikiambatana na picha hiyo ya Passport Juu hapo:
“Leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe. Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”

WASTARA JUMA .... "WANAUME WALIO MSAIDIA SAJUKI WAMENIGEUKIA NA KUNITAKA KIMAPENZI"


Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.

Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.

ANGALIA PICHA ZAIDI ZA MAPOKEZI YA MIILI YA MASHUJAA WA TANZANIA WALIOUAWA DARFUR ILIVYOPOKELEWA LEO JIJINI DAR




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni.




 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. 



Miili hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa kumi.

"HAKUNA UCHAGUZI WA MEYA ARUSHA" NAPE NNAUYE

Nape Nnauye
MKURUGENZI WA Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye amesema suala la uchaguzi wa Meya wa Mji wa Arusha limefikia tamati na kamwe uchaguzi huo hautafanyika tena. Nnauye alisema hayo alipozungumza na MTANZANIA jana, huku akiwataka wananchi wa Jiji la Arusha kupuuza kauli za vitisho zinazotishia kumwondoa madarakani Meya wa Jiji, Gaudence Lyimo.
Kauli ya Nnauye inafuatia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema Arusha Isaya Doita, aliyesema kuwa ushindi wa udiwani wa chama chao katika kata nne za mji huo ni chachu katika msimamo wa chama chao kutaka uchaguzi wa Meya wa Arusha urudiwe.

Doita akiamini kuwa Lyimo alichaguliwa kwa mizengwe, alisema ana imani muda si mrefu Jiji la Arusha litapata meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria.

Hata hivyo, siku chache baadaye Katibu wa Chadema wa Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema suala la nafasi ya umeya siyo tena ajenda ya chama hicho.

Akizungumzia suala hilo jana, Nnauye alisema CCM imezoea kusikia kauli mbalimbali za vitisho zinazotolewa Chadema na kuwataka wananchi wa Arusha kuzipuuza kauli hizo.

“Ni kazi yao vitisho nia yao ni kutaka watu wasifanye shughuli zao, lakini suala la meya yupo pale na ataendelea kuwapo kwani uchaguzi ulishafanyika na hautafanyika tena.

“Kazi iliyobaki sasa kwa wananchi wa Arusha ni kujenga mji wao kwa kufanya kazi, watu wafanye kazi zao wala hakuna sababu ya kuhofia kauli za vitisho.

“Ni upuuzi kuanza kuzungumzia kila siku suala la Arusha, waliopewa dhamana wawajibike kilichobaki ni kufanya kazi, waache kusikiliza upuuzi,” alisema Nnauye.

CHANZO MTANZANIA

KOCHA MZUNGU TAIFA STARS AFARIKI DUNIA JANA

Bert Trautmann

 
Tumempoteza: Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Bert Trautmann amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89 jana.


Na Mahmoud Zubeiry na Chris Wheeler,
KOCHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na giwji wa zamani wa klabu ya Manchester City, Mjerumani Bert Trautmann amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 89.
Baada ya BIN ZUBEIRY kusoma taarifa za kifo cha kocha huyo Daily Mail, ilimpigia Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Leodegar Chilla Tenga ambaye alifundishwa na Mjerumani huyo na akasikitisha.
Tenga, ambaye sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alisema kwamba Trautmann, ambaye alikuwa anasumbuliwa alikuwa mwalimu mzuri na wachezaji walimpenda sana.
Alisema kocha huyo aliyefariki asubuhi ya leo nyumbani kwake, La Losa, karibu na Valencia aliifundisha Taifa Stars kati ya mwaka 1975 na 1976.
“Alikuwa kocha mzuri, kwa sababu ni kocha aliyetokea kuwa mchezaji wa kulipwa, alikuwa anaelewa saikolojia ya wachezaji, na alikuwa mwalimu ambaye ukienda kambini unaona raha kuwa kambini.

MAAJABU:MBUZI AZALIWA NA VICHWA VIWILI TENA KWA MAUMIVU MAKALI

Kuanzia Saa 10 Alfajiri zilisikika kelele za Maumivu kutoka kwa mbuzi jike ambaye alikuwa anajifungua, Kelele zilikuwa kubwa mno kuashiria maumivu makali alikuwa anayapata kiumbe huyo, palipozidi kupambazuka ilibidi majirani waende kushuhudia kulikoni kwa mbuzi kuwa na kelele kiasi kile, na ndipo walipojionea maajabu baada ya mbuzi jike huyo kujifungua watoto watatu, wawili kati ya hao wakiwa ni wa kawaida kabisa na mmoja akiwa na vichwa viwili.

Hayo ndio yaliyojiri Alhamisi ya jana tarehe 18 July 2013 Huku katika Jimbo la Irolini Kwara, Nigeria. Hata hivyo mbuzi huyo alizaliwa na vichwa viwili alifariki saa chache baadae

Friday, July 19, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA PROFESA LIPUMBA KWA MAZUNGUMZO IKULU DAR


  
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.
 
 Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya siasa na uchumi nchini.Pichani Rais Kikwete akiwa na Professa Lipumba katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
 
Rais Kikwete, akiagana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba baada ya mazungumzo yao jana. Picha na Fredy Maro

MNYIKA AANIKA NAMBA ZA MAWAZIRI KWA UMMA...!!!

  Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba; “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:

Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

WEMA SEPETU KUOZEA JELA, ALICHOKIFANYA SAFARI HII....!!!


KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.

Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.


Kabla ya  kupandishwa  kwa ‘pilato’,  staa huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame alikuwa akisakwa na askari kwa siku kadhaa na kufanikiwa kuwapiga chenga za hapa na pale.

ANASWA AKIFUTURU
Hata hivyo, mbio zake ziliishia ukingoni Julai 16, mwaka huu, alipokamatwa saa mbili usiku akiwa anafuturu na wageni wake nyumbani kwake, Kijitonyama Dar.

MTITI KIDOGO
Askari saba walifika nyumbani kwake wakiwa ndani ya Land Rover ‘difenda’ kwa ajili ya kumkamata, hata hivyo walipata upinzani kidogo kutoka kwa mlinzi wa staa huyo ambaye alikuwa akizuia bosi wake asikamatwe ambapo ilibidi askari hao wakaze msuli na kutuliza mtiti uliokuwa ukitaka kutokea.

MZEE WA MIAKA 63 ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMBAKA MSICHANA WA MIAKA 16 NDANI YA MSIKITI...!!!


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma, imemhukumu Ahamad Fadhil (63), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 ndani ya Msikiti wa ni Mwembe Mmoja, mjini hapa.

Hukumu hiyo ilitolewa na jana na Hakimu wa mahakama hiyo, Obadiah Bwegoge, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.


Hakimu Bwegoge alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili liwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.


  Alisema upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi watano ambao bila kuacha shaka, walithibitisha kuwa mshtakiwa huyo alimbaka msichana huyo (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.


Alisema shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri ambaye ni mlalamikaji, alidai kuwa siku ya tukio, saa nane 8:00 mchana, alikwenda msikitini hapo kuomba msaada kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.

SERIKALI YASISITIZA KUWA "KODI YA LINE ZA SIMU" IKO PALE PALE...!!!


Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.

Akizungumza na mwandishi juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.

Pia alieleza kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini na kodi hizo zinakwenda kutumika huko.

Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa ikatumike kusaidia maji na uwezo wa Serikali kupeleka elimu vijijini jambo ambalo ni la maendeleo.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 19, 2013

MASISTER BANDIA WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ...!!!

Wanawake watatu wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya kupitia uwanja wa ndege wakiwa wamevalia kama masista.
 
Wasafirishaji hao walisimamishwa wakati wakiwasili kwenye kituo maarufu cha mapumziko nchini Colombia, sababu polisi walifikiri kwamba mavazi yao hayakuwa yakionekana halisia.
Maofisa waligundua kwamba kila mwanamke kati yao alikuwa na zaidi ya kilo 4 za cocaine zikiwa zimefungwa katika miguu yake.

Wakiwaongezea fedheha katika mashitaka, wasafirishaji hao walipangwa mstari mbele ya waandishi wakiwa bado wamevalia mavazi yao ya kituko kuficha ukweli.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...