Saturday, June 29, 2013

MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU "BRIAN DEACON" AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.

 
Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS.
  Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

HII NDIO SABABU YA KAJALA KUNYOA BONGE LA UPARA...!!!

Mwigizaji aliyerudi uraiani hivi karibuni Kajala Masanja amefanya mabadiliko makubwa ya mtindo wake wa nywele baada ya kunyoa kipara “kikavu” kichwani mwake.
 Exclusive: Kajala aamua kunyoa kipara; kisa na mkasa? Soma hapa.
Katika picha alizozitoa mwigizaji huyo kupitia kwenye mtandao jana, mwigizaji huyo ameonekana akiwa na kipara tofauti na alivyozoeleka na nywele nyingi siku za nyuma.

Bongomovies.com tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili kujua “kunani”?? na staili hiyo na tulimpigia simu na maongezi yalikuwa kama ifuatavyo:
Bongomovies.com: Mambo kajala, mzima?
Kajala: Mzima, kwema?

Bongomovies.com: Kwema kabisa, vipi tena na kipara kichwani?
Kajala: Aha,..Siunajua tena mishe mishe, nipo na shoot movie yangu mpya ndo mana imenibidi ninyo kipara maana inanilazimu kuonekana hivyo ndani na Filamu hiyo.
Bongomovies.com: Okay, na itaitwaje?
Kajala: Itaitwa Heart attack

Bongomovies.com: Umewashirikisha nani na nani humo ndani?
Kajala: Atakuwepo Hemedi na mastaa wengine Kibao, kifupi ni bonge la movie yani.
Bongomovies.com: Basi tunaisubiri kwa hamu sana
Kajala: Pamoja sana.

MKE AMFUMANIA MUMEWE AKIWA NA KIMADA GESTI HUKO SINZA, MUME AMKIMBIA MKEWE AKIWA UCHI WA MNYAMA

Tukio hilo lililowashangaza wengi lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika gesti moja iliyopo Sinza jijini Dar. Awali Flaviana na bwana wake huyo walichukua chumba baada ya kushindwa kurudi nyumbani kutokana na kuzidiwa na kilevi.
Ilikuwaje fumanizi likatokea?
Ilielezwa kuwa wakati wawili hao wakiingia kwenye chumba cha gesti hiyo, Flaviana alikuwa bwii hivyo ‘kuzima’ kwenye kochi na kushindwa kufanya chochote.
“Wakati Aron akiwa chumbani pale, alifika shosti wa Flaviana aitwaye Dina na kwa kuwa Flaviana alikuwa hajitambui, wawili hao walianza kupeana malavidavi.

“Flaviana akiwa amelala alikuwa kama vile anasikia watu wakishughulika lakini alishindwa kufanya chochote kutokana na kuzidiwa na pombe.
“Wale wakaendelea kubanjuka. Ilipofika saa 12 asubuhi Flaviana akapata nguvu na kuamka kwenda kujisaidia, aliporudi akabaini shosti wake amemsaliti na ndipo alipoanzisha timbwili,” alidai mtoa habari wetu.

Flaviana apigia simu mapaparazi
Wakati timbwili hilo likiendelea chumbani hapo, Flaviana alipata mwanya wa kuwapigia simu mapaparazi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshuhudia Dina akiwa ndani ya Bajaj huku akivaa nguo kabla ya kumuamuru dereva kuondoka kwa spidi.
Naye mwanaume ambaye alikuwa ndani ya chumba cha gesti hiyo, aliposikia waandishi wamefika, alitokea mlango wa nyuma akiwa amevaa ‘boksa’ na tisheti, akaacha suruali yake chumbani hapo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi huku akiwaonesha mapaparazi kitanda kilichokuwa vululuvululu, kilichotumika katika usaliti huo pamoja kondom, Flaviana alisema: “Nimeumia sana, yaani nimesalitiwa nikiwa humuhumu chumbani, Aron kanidhalilisha sana na huyo Dina naye kumbe siyo mtu, nitahakikisha namsaka nimshikishe adabu.”

MAMIA NCHINI AFRIKA KUSINI WAJITOKEZA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA KUJA KWA RAIS OBAMA WAKATI ALIPOTUA JANA JIONI KATIKA JIJI LA PRETORIA

 Waandamaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Rais Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika jana Jioni wakati Raisi Obama alipotua Katika Jiji Hilo jana Jioni Juni 28
 Waandamaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Rais Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya Juni 28
 Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Rais Obama Nchini Humo Mapema jana wakati Rais Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ametokea Nchini Senegali na Kutua Nchini Afrika Kusini huku Akihitisha Ziara Yake Nchini Tanzania wiki ijayo.
Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Rais OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo. Mwandamaji huyu amebeba bango jana Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao. Picha Zote na REUTERS/AFP

Friday, June 28, 2013

BIBI YAKE OBAMA MAMA SARAH OBAMA KUJA TANZANIA KUMSALIMIA MJUKUU WAKE ATAKAPOWASILI DARESALAM.

 
SIKU CHACHE KABLA YA ZIARA YA RAIS WA MAREKANI KUJA NCHINI TANZANIA IMEFAHAMIKA KUWA BIBI YAKE NA RAIS OBAMA MAMA SARAH OBAMA ANATARAJIA KUJA NCHINI TANZANIA KUJA KUMSALIMIA MJUKUU WAKE HUYO.
AKIZUNGUMZA  JUZI KIJIJINI KWAKE ENEO LA KWEGERO HUKO KISUM BIBI HUYO ALIEZALIWA MWAKA 1922 AMESEMA KUWA HAJISKII VIBAYA OBAMA KUTOITEMGELEA KENYA KWANI ANAJUA KUWA OBAMA NI RAIS WA TAIFA KUBWA DUNIANI, HIVYO ANAKUWA NA RATIBA AMBAYO INAZINGATIA MAMBO MENGI NA NI VIGUMU SANA KUIVUNJA.
BIBI HUYO AMEENDELEA KUSEMA KUWA ANAJISIKIA FURAHA KUONA MJUKUU WAKE HUYO KUJA TANZANIA KWANI HISTORIA INAONYESHA KUWA KABILA LA KIJALUO LINAMUINGILIANO MKUBWA KATI YA NCHI HIZI MBILI ZA TANZANIA NA KENYA HIVYO WAO WANAAMINI KUWA OBAMA AMEITEMBELEA NCHI YA NYUMBANI KWAO.

NAY WA MITEGO NA DIAMOND KUJA NA NGOMA MPYA..."SALAMU ZAO"

 
Baada ya kutamba na Muziki Gani, Diamond na Nay Wa Mitego wako mbioni kuachia ngoma nyingine hivi karibuni baada ya kupembua ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’.

Nay ameiambia mpekuzi kuwa kuna nyimbo tatu ambazo zipo tayari, Salamu Zao, Kwa Masela na Utakula Jeuri Yako, hawajajua ipi itaanza kutoka kwasababu kila mmoja yupo katika tour zinazoendelea. 

Wamesema wakikaa wakashauriana na wadau mbalimbali ndipo watakapoamua mzigo upi uingie mtaani kwanza.

“Kuna kazi ambazo zinakuja hivi karibuni ambazo nimefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi sijajua ni ipi ambayo itaanza kutoka lakini tutawaita wadau wachague ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’ ambazo zipo tayari na ‘Utakula Jeuri Yako’ nimefanya mwenyewe...

"Ilibidi tutoe nyimbo ambayo tumefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi hakuna maamuzi ya moja kwa moja tuitoe au kila mtu atoe ya kwake au tutaendelea na project yetu iliyoendelea, kwahiyo wadau wakae mkao wa kula,” amesema Nay.

BAADA YA MIAKA KUPITA LADY JAY DEE NA Q CHIEF WAINGIA STUDIO TENA

 
Wakali wa bongo fleva wenye vocal zenye ladha na nguvu ya aina yake Lady JayDee ‘Anaconda’ na Q-Chillah, wamekutana tena studio kurekodi wimbo mpya ikiwa ni miaka kadhaa imepita walipotisha na wimbo wao ‘Zamani’. 
Lady JayDee alipost picha kupitia akaunti yake ya Twitter ikimuonesha yeye na Q-chilla wakiwa ndani ya studio za Combination sound na Man Walter, na kuisindikiza na maelezo. 
"Mtu 3 ndani ya studio. Mwaikumbuka Zamani - Q Chief feat Jide?? Nikilala naotaa, naota km unaniita. Sasa yaja mpya."Alitweet Jide June 26.

Hakuchelewa kutaja jina la wimbo huo “Sukari” na kuonesha kuikubali sana, hii inatoa picha kuwa kitu kikubwa kinakuja.
“Sukari - Qchillah & Jide another hit ??? ☺ #Justasking.” Aliongeza.

Tuisubiri hiyo sukari tuonje ladha yake kwa masikio.

WAGANGA WA JADI AFRIKA KUSINI WAMFANYIA TAMBIKO MZEE MANDELA

Sasa ni dhahiri kuwa maisha ya kiongozi wa zamani wa nchi hii, Nelson Mandela yamo hatarini kutokana na kwamba anaishi kwa msaada wa mashine, imethibitishwa na mmoja wa wazee wa ukoo wa kiongozi huyo.

Binti yake mkubwa Makaziwe naye amethibitisha hilo, akisema hali ni mbaya na chochote chaweza kutokea.
"Naweza kusisitiza hilo, kwamba Tata (baba) hali yake ni mbaya sana, chochote chaweza kutokea, lakini nataka nisisitize tena, kwamba ni Mungu tu ndiye anajua muda wa kuondoka,” alikiambia kituo cha utangazaji cha SAFM jana.
Hali hiyo inayotia mashaka imesababisha hata Rais Jacob Zuma afute safari yake ya Msumbiji ambako alipanga kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
“Ndiyo, anatumia mashine kupumua,” Mzee Napilisi Mandela aliiambia AFP muda mfupi baada ya kumtembelea Mandela hospitalini juzi. “Hali ni mbaya, lakini tutafanyaje.” 
Zuma alifuta safari yake iliyokuwa ifanyike jana baada ya “kubaini, kwamba kiongozi huyo wa zamani hali yake bado ni mbaya,” taarifa kutoka Ofisi ya Rais ilisema.
Wakati huo huo, kiongozi wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-moon alisema juzi kwamba dunia yote inamwombea Mandela wakati huu ambapo anapigania maisha yake.

BINTI AJIFUNGUA BARABARANI AKIKIMBIZWA HOSPITALI KWA BODABODA

Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.
Na Dustan Shekidele, Morogoro
BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.


Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume ‘dume la nguvu’.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 28, 2013

.
.

Thursday, June 27, 2013

MELI YA MAGUFULI YAZAMA BAHARINI.


 
PICHA ya maktaba ikionyesha meli ikizama baharini.

ILE meli maarufu kwa jina la ‘Meli ya Magufuli’ ambayo serikali iliinasa katika eneo lake la bahari ya Hindi ikivua samaki bila ya kibali, imezama baharini, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Habari ambazo gazeti hili limezipata, meli hiyo ambayo ina uwezo wa kuvua samaki kwenye kina kirefu baharini, imezama  baada ya wajanja wachache kukata vyuma vyake na kuuza kama chuma chakavu.

Kwa mujibu wa habari hizo, wajanja wamekuwa wakiingia na kukata vyuma vya meli hiyo baada ya serikali kuitelekeza kwa muda mrefu bila uangalizi tangu ilipoitaifisha.

Vyanzo vyetu vya habari vilipasha kuwa vyuma chakavu vya meli hiyo vimekuwa vikiuzwa kwa kampuni zinazonunua na kuvisafirisha nje ya nchi na kujiingizia mabilioni ya fedha.

Sehemu kubwa ya vyuma chakavu kutoka kwenye meli hiyo, vimeuzwa kwa kampuni moja inayomilikiwa na mmoja wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano.

Inaelezwa kuwa sehemu kubwa ya meli hiyo imetengenezwa kwa malighafi aina ya Brass ambayo kilo moja kwa sasa inauzwa kwa sh 5,200.

Malighafi nyingine zilizotumika na bei yake kwa kilo kwenye mabano vikuzwa kama chuma chakavu ni Cast Aluminum (sh 1,700), Stainless (sh 1,500) na Soft (sh 2,000).


CCM WANG'ANG'ANIA SERIKALI MBILI KATIKA KATIBA MPYA.

 

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kimemalizika mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa kuwa chama hicho kimeweka msimamo wa kutaka kuwepo kwa mfumo wa Serikali mbili katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania upo katika hatua ya rasimu na watu mbalimbali kupitia Mabaraza ya Katiba, wamekuwa wakitoa maoni yao.Tayari Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa chama hicho kitakuwa moja ya mabaraza ya katiba na kupata nafasi ya kuichambua, kuijadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ilitolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Habari za ndani zilisema kuwa kikao hicho kilichoongozwa na Rais Kikwete kilijadili mchakato wa Katiba Mpya, masuala ya maadili ndani ya chama na kuyatolea uamuzi.


Hata hivyo mmoja wa watendaji ndani ya chama hicho alisema kikao kilikuwa cha kawaida na kwamba kilikuwa kinapitia majukumu na kwamba hakuna kubwa lililojadiliwa. Habari zaidi zinadai kuwa mbali ya kuunga mkono mfumo wa Serikali mbili, CCM imetoa adhabu kwa wanachama wake wawili ambazo zitatangazwa katika siku iliyopangwa.

WATU 10, 799 WANASWA NA DAWA ZA KULEVYA TANZANIA

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Mizengo Pinda

WATU 10,799 wamenaswa wakijihusisha na dawa za kulevya katika kipindi cha miaka mitano pekee na kuonyesha namna gani biashara ya dawa hizo lilivyo tatizo nchini.
Kwa mujibu wa hutuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Urasimu na Bunge) William Lukuvi katika Siku ya Kupiga vita Dawa za Kulevya Duniani ni kwamba biashara ya dawa za kulevya ni tatizo nchini.
Pinda alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

WATU WA MIKOANI WASHAURIWA KUTOENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA HADI ATAKAPO MALIZA ZIARA YAKE.

 

Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe(PICHANI) amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.

Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

 

“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.

Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 27, 2013





Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...