Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Mizengo Pinda |
WATU
10,799 wamenaswa wakijihusisha na dawa za kulevya katika kipindi cha
miaka mitano pekee na kuonyesha namna gani biashara ya dawa hizo lilivyo
tatizo nchini.
Kwa
mujibu wa hutuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa kwa
niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Urasimu na
Bunge) William Lukuvi katika Siku ya Kupiga vita Dawa za Kulevya Duniani
ni kwamba biashara ya dawa za kulevya ni tatizo nchini.
Pinda
alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika
biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba,
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita watuhumiwa 10,799 walikamatwa
kwa kujihusisha na dawa hizo.
Aidha, amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.
“Vile
vile katika kipindi hicho jumla ya Watanzania 240 walikamatwa katika
nchi mbalimbali, zikiwamo Brazil, Pakstani na Afrika Kusini,” alisema
Pinda.
Alisema
hali hiyo imekuwa ikiharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania
wasio na hatia kupata usumbufu, masharti magumu wanapotaka kusafiri
kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda alisema hali hiyo inatokana na sifa mbaya inayojengeka kwa Watanzania wanaosafiri katika nchi hizo.
Alisema
zipo dalili kwamba, endapo biashara hiyo itaachwa iendeleee, athari
zaidi, zikiwamo kuingiliwa kwa misingi ya kiutawala na wafanyabiashara
wa dawa kwa manufaa binafsi, kuongezeka kwa waathirika wa rushwa.
Aidha,
alisema uwapo wa biashara hiyo huongeza mzunguko wa fedha haramu na
kusababisha mfumko wa bei na hivyo kuongeza hali ya umaskini.
Pinda
alisema kwa mujibu wa vyombo vya dola, takwimu zinaonyesha viwango vya
Heroin na Cocaine zinazoendelea kukamatwa nchini, kuanzia mwaka 2000 ni
vikubwa kuliko vile vilivyokamatwa miaka 10 iliyopita.
Alisema
mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika
eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na nchini .
Kwa mujibu wa Pinda, jumla ya kilo 914 za Heroin zilikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia uharamia cha Jeshi la Kimataifa.
Alisema
askrimu, mikate na maandazi vilivyofanyiwa uchunguzi katika moja ya
shule jijini Dar es Salaam vilibainika kuwa na kiasi kidogo cha dawa
hizo za kulevya.
Aliwataka
walimu na walezi kuwa makini na watu wanaouza vyakula katika maeneo
karibu na shule ili kuepuka wauzaji hao kuwafundisha wanafunzi kutumia
dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment