Josephine Michael
akiwa barabarani baada ya kujifungua.
Na
Dustan Shekidele, Morogoro
BINTI
mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo
ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani
wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.
Tukio hilo lililowashtua watu wengi
lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya
Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.
Mwandishi
wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha
usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya
kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo
akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto
wa kiume ‘dume la nguvu’.
NA GPL
NA GPL
Mmoja wa akina mama waliofika eneo hilo akiwa
amembeba mtoto wakati mama yake akihojiwa na mwanahabari.
Awali, wanawake hao walizungusha
kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao
alipokuwa akijifungua.
Mara baada ya
zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri
ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya
wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa
barabara.
Kulia ni trafiki aliyemsaidi Josephine
kujifungua na kushoto mtoto aliyezaliwa akiwa amebebwa.
“Hali ilipozidi kuwa mbaya
tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika na kunibeba huku mume
wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake,” alisema Josephine kwa
uchangamfu.
Binti huyo alisema
kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa
kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa
bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.
Wananchi waliofika eneo hilo wakiwa na
Josephine (aliyekaa chini).
Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki
na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi
alipojifungua salama.
Dereva wa bodaboda
aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri
barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya
Josephine kujifungua salama mtoto wa kiume.
No comments:
Post a Comment