Thursday, April 18, 2013

Barua zilizotumwa kwa rais Obama zagundulika kuwa na sumu aina ya ricin.

Barua zilizokuwa zimetumwa kwa Rais Barack Obama na Seneta wa Mississippi Senator Roger Wicker  zmebainika kuwa na  sumu hatari aina ya ricin.
Idara kuu ya upelelezi ya Marekani FBI imetoa taarifa  hiyo na barua zilizotumwa kwa viongozi hao wawili zinahusiana.
Barua hizo zote zilitumwa kutokea Memphis, Tennessee na mtu mmoja mwenye umri wa miaka 45 amekamatwa Mississippi kuhusiana na barua hizo.
Pamoja na barua hizo, polisi mjini Washington wanavichunguza vifurushi vitatu wanavyovitilia mashaka vilivyogunduliwa katika ofisi za majengo ya seneti.
Kugunduliwa kwa vifurushi hivyo kwenye eneo  kubwa la majengo ya ser

ANGALIA PICHA ZA MAELFU WAHUDURIA MAZIKO YA MAREHEMU BI KIDUDE.


Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi R.I.P..........KIDUDE BINTI BARAKA

Jeneza la bibi likielekea msikiti kwa ajili ya kusaliwa

Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwamarehemu bi Kidude, Zanzibar

AUNTY EZEKIEL: WABUNGE BAADA YA MATUSI BUNGENI SASA WANATAKA KUVUNJA AMRI YA 6!!


DIVA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa chake na kudai kwamba
 kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata penzi kwake, 
Amani linasimulia aliyoyasema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar, Aunt alisema waheshimiwa hao 
wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na 
kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho anaamini kinaweza 
kuhatarisha ndoa yake.

"Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua tayari nimeolewa lakini 
wananitongoza, mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza:
 “Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu wazito, hawezi kuwa na
 amani, bado naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.”
Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunday Dimonte,
 Dubai na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume
SOURCE: GPL

HALI NI MBAYA SANA BUNGENI



Wabunge watano wa Chadema jana walitimuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano kutokana na vurugu zilizotokea jana usiku.Wabunge hao ni Lissu, Hezekiah Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).



Chanzo za kufukuzwa kwao ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya
Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba.


Kutokana na tafrani hiyo, Nchemba hakuweza kuhitimisha hotuba yake hivyo Ndugai alilazimika kukatisha mkutano wa Bunge.Hata hivyo wakati akiahirisha mkutano huo, tayari wabunge hao walikuwa wameshatolewa nje baada ya askari kuongezwa.


Mapema Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alitoa tusi zito la nguoni wakati wa hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, licha ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kupiga mkwara wa kuwashughulikia wabunge watakaorusha matusi.

MAJIRANI WALAMZIMISHA LIONEL MESSI KUNUNUA NYUMBA ZAO BAADA YA KUFULIA

Mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi, hivi karibuni alilazimika kununua nyumba za majirani wanaoizunguka nyumba huko Barcelona Hispania bila kupenda.   
Kwa mujibu wa taarifa kutoka SportsGrid ni kwamba majirani wa Messi walikuwa wanazifanyia marekebisho nyumba zao, lakini kwa bahati mbaya wakaishiwa na fedha katikati ya marekebisho hayo huko mjini Castelldefels, Spain, hivyo wakamuomba kijana tajiri Messi azinunue nyumba hizo zilizokuwa kwenye marekebisho na kwa utaratibu Messi akakataa.
Baada ya ombi lao kukataliwa majirani wakaamua kuanza kufanya vitimbi ili Messi aone kero na kuamua kununua nyumba zao, walizikodisha nyumba zao na wapangaji wao wakawa watu wa fujo wenye makelele muda wote na hatimaye vitimbi hivyo vikazidi kuwa kero kwa Baba Thiago na familia yake. Mara ya kwanza Messi alienda kuongea nao waache tabia hizo lakini hali haikubadilika hivyo akaamua kujenga ukuta mrefu wa kuitenganisha nyumba take na majirani - lakini jaribio hilo likawa linaenda kinyume na baadhi ya sheria za Spain kuhusu ujenzi na majirani wakatumia nafasi hiyo kutishia kumshtaki Messi.

Hivyo ili kuepeukana na skendo ya kupelekwa mahakamani Messi akaamua kuwait a wanasheria wake na kuwaambia wafanye taratibu za kisheria kufanya manunuzi ya nyumba zote za majirani waliokuwa wakitaka kuziuza. Hatimaye mpango wa majirani ukafanikiwa na Messi akanunua nyumba zote za majirani wake hivyo kumfanya kuwa mmoja ya watu wanaomiliki maeneo makubwa kwenye sehemu ya Castelldefels, Spain.

HUKUMU YA PONDA NA WENZAKE LEO

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini iliwaona wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote matano yanayowakabili. Katika moja ya mashtaka hayo, Sheikh Ponda na wenzake anadaiwa kula njama na wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni.
Awali, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa alitoa uamuzi kuwa kina Sheikh Ponda wana kesi ya kujibu baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 17 wa upande wa mashtaka, ikaonekana shauri hilo limetokana na kipande cha ardhi.

Kesi hiyo iliposikilizwa mara ya mwisho, Hakimu Nongwa alisema kuwa baada ya Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kubadilisha ardhi ya ekari nne iliyopo Chang’ombe Markazi na ekari 40 za Kampuni ya Agritanza Ltd zilizopo Kisarawe, kuna baadhi ya Waislamu hawakuridhika.

Mbali na mashtaka hayo, Ponda na mshitakiwa mwingine Sheikh Mukadam Abdallah Swalehe wanakabiliwa na shtaka la uchochezi wakidaiwa kuwa kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka jana katika eneo la Chang’ombe Markazi, wakiwa viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, waliwashawishi wafuasi wao kutenda makosa hayo.

Pia inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 21 na 16, mwaka jana katika eneo hilohilo, washtakiwa hao pasipo uhalali wowote, walijimilikisha ardhi ambayo ni mali inayomilikiwa kihalali na Kampuni ya Agritanza Ltd na kusababisha uvunjifu wa amani.

Kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka jana, huko Chang’ombe Markazi, washtakiwa hao wanadaiwa kuiba vifaa na malighafi mbalimbali za ujenzi, yakiwamo matofali 1,500, tani 36 za kokoto na nondo vyote vikiwa na thamani ya Sh59,650,000 mali ya Kampuni ya Agritanza Ltd.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 18.04.2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS HAYA HAPA

8 d74fe

9 d2ab2

7 2ab60

6 e7756

Wednesday, April 17, 2013

HISTORIA YA BI. KIDUDE KWA UFUPI

Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Binti Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia leo mchana  huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa.Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. 

Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa nazi na hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102. 

Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....

Mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.

Bi Kidude pia aliwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni

Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen.

NDOA YA UWOYA NA NDIKU SASA YAFIKA MWISHO RASMI! KISA NI DIAMOND

Mapenzi bwana! Ukiambiwa yanaweza kuua usibishe kabisa, kwani ukiondoa mifano mingine ya kufikirika, kitu ‘live’ ni kwamba mwanasoka raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alianguka na kuzimia, baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu mkewe.Ndikumana, alianguka na kuzimia, asubuhi ya Aprili 8, mwaka huu, baada ya kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda, lililoandika habari ya usaliti wa mkewe, Irene Uwoya, aliponaswa hotelini na mwamuziki, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Habari za kuzimia kwa Ndiku, zimewekwa kweupe na Uwoya mwenyewe, aliyesema: “Maskini Ndikumana wangu, baada tu ya kusoma habari ya mimi na Diamond alianguka na kuzimia.”
Kwa tafsiri, Uwoya anamsikitikia mume wake kuanguka na kuzimia, upande wa pili anajuta kumfahamu Diamond, kwani ndiye aliyemsababishia majanga yote.

MIRATHI YA KANUMBA, BADO NI UTATA.

Ngoma inaonekana kuwa bado ni nzito kuhusiana na mirathi ya marehemu Steven Kanumba kwani taarifa zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza kuwa, hakuna kitu kilichofanyika mpaka sasa kutokana na mvutano uliokuwepo ndani ya familia.
 

Akizungumza na Risasi Jumatano hivi karibuni, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema yeye aliamua kukaa pembeni na kumuachia baba wa marehemu, mzee Charles Kusekwa afuatilie suala hilo lakini anashangaa mwaka umepita hakuna kilichofanyika.
Akasema, alisikia mzee huyo alituma wawakilishi wake walishughulikie suala hilo lakini wakachemsha kutokana na kukosa viambatanisho muhimu.
 

“Mimi niliamua kusubiri upande wa baba Kanumba wafungue mirathi kwa sababu Kanumba hakuwa na mtoto kusema nina ulazima wa kuharakisha ili apate haki zake, cha ajabu hakuna kilichofanyika mpaka sasa,” alisema mama Kanumba.
 

Akasema, kutokana na kwamba ametoa muda mrefu kwa mzee Kusekwa kushughulikia suala hilo bila mafanikio, ameamua kuingia ‘front’ mwenyewe ili kuhakikisha haki za mwanaye zinapatikana.
Credit:Global Pubishers.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUSAMBAA KWA HABARI ZA MISHAHARA YA WALIMU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII



BI KIDUDE AFARIKI DUNIA

.
 
MSANII WA MUZIKI WA TAARABU NCHINI TANZANIA KUTOKA VISIWANI ZANZIBAR FATUMA BINT BARAKA MAARUFU KAMA BIBI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA LEO HUKO VISIWANI ZANZIBAR.
 
BI. KIDUDE AMEFIKWA NA MATUTI HAYO LEO KUTOKANA NA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU.
 
BI. KIDUDE  AMESHAWAHI KUFANYA KAZI NYINGI IKIWEMO MHONGO WA JANG'OMBE, KIJITI, ALAMINADURA, YA LAITI, AHMADA NA NYINGINE NYINGI.

Mwana Mziki wa Tanzania AY awa Verified on Twitter


Account ya mtandao wa kijamii ya Twitter ya mwanamuziki maarufu Afrika kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya (AY) yatambulika rasmi na kuwa mwanamuziki wa kwanza hapa Bongo account yake kutambulika yaani (Verified Account) .

Twitter ambayo hufanya hivyo kwa kukuwekea alama ya tick ya blue mbele ya jina lako ili kukutambulisha kwa marafiki, ndugu, jamaa, mashabiki wako wanaokufuata [followers] kuwa wewe ni mtumiaji halisi wa account hiyo walifanya hivyo kwenye account ya Ambwene ndani ya masaa kadhaa yaliyopita.

Twitter pia hufanya hivi ili kukutofautisha na watumiaji wengine wanaoweza kutumia jina lako katika mtandao huo na wamekuwa wakifanya hivyo kwa watu maarufu katika nyanja mbalimbali.
AY amekuwa mmoja kati ya watanzania wachache ambao account zao zimekuwa hivyo akiwemo mcheza kikapu wa Oklahoma City Thunder(OKC) Hasheem Thabeet [@hasheemthedream], Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete [@jmkikwete] Flaviana Matata [@FlavianaMatata] na Waziri January Makamba

VIGOGO WIZARA YA ARDHI KORTINI KWA UBADHIRIFU

Simoni Lazaro (kushoto) akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Gerald Mango.
Watuhumiwa hao wakiwa mahakamani.
Charles Kijuba akikwepa kamera mahakamani.
MAOFISA watatu waandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi leo wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za ufujaji wa pesa za serikali zaidi ya milioni 200. Watuhumiwa hao ni Simon Lazaro ambaye alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Sera, Gerald Mango, Mkuu wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi , na Charles Kijuba, Kaimu Mhasibu Mkuu.
Watuhumiwa hao wamekana mashitaka na mahakama hiyo imesema kuwa dhamana iko wazi

MAGAZETI YA LEO APRILI 17, 2013

.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...