Mwanamuziki mkongwe katika
Taarab Fatuma Binti Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki
dunia leo mchana huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa
kipindi sasa.Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa
kesho.
Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha
Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa nazi na hakuna anayejua
haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa
alikwishafikisha miaka 102.
Katika
mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya
sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar
es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....
Mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa
amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi
Kidude pia aliwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na
katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba
katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni
Mungu
Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen.
No comments:
Post a Comment