Wednesday, April 17, 2013

MILA POTOFU ZACHANGIA KUONGEZEKA KWA MAAMBUKIZO YA UGONJWA MALARIA MKOANI MBEYA

......................................................................

Na Esther Macha, Mbeya
LICHA ya Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya vyandarua hali hiyo bado imekuwa tatizo kutokana jamii zilizo nyingi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuwa na imani potofu kuhusu matumizi ya vyandarua vyenye dawa kuwa hawapati usingizi na wengine kudai ni njia ya uzazi wa mpango.

Hayo yalisemwa jana Bwana afya katika Ofisi ya Wilaya ya Mbarali Bw.Yona Msyani wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili, kuhusiana na elimu ya ugonjwa wa maralia katika viwanja vya hospitali ya Chimala Mission .
 
Alisema kuwa suala la utumiaji wa vyandarua imekuwa changamoto kubwa kwa katuiika utendaji kazi kwa wataalamu wa afya kutokana na wananchi kuwa na imani potofu juu ya matumizi ya vyandarua vyenye dawa.

“Bado tuna changamoto kubwa sana hivyo inatupasa kujipanga na kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa matumizi ya vyandarua “alisema.

Hata hivyo alisema kuwa imani hiyo potofu si kwa Wilaya ya mbarali tu kwani hali hiyo ilijitokeza wakati wa kampani ya ugawaji wa vyandarua hivyo mwaka 2010 kwa nchi nzima.
Bw. Msyani alisema kuwa kama wataalamu wa afya bado wanaendelea kutoa elimu ya afya kwa wananchi jinsi ya kujizuia na ugonjwa wa maralia ikiwa ni pamoja na kuondokana na dhana potofu waliyojenga wananchi.

Akizungumzia kuhusu vifo ambavyo vinatokana na ugonjwa maralia ,Bwana afya huyo alisema kuwa maralia I ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“Tatizo hili lipo kwa kiasi kikubwa kwa watoto , mwaka 2012 mwezi januari mpaka desemba waliugua watoto 1,635 chini ya umri wa miaka mitano ambapo kati ya hao waliofariki ni 100 kwa mwaka jana kutokana na ugonjwa wa maralia.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...