WanaCCM wa Ifakara mjini ‘wamemshtaki’ Katibu Mkuu
wa zamani wa CCM, Yusuph Makamba kwa Katibu Mkuu wa sasa wa chama hicho,
Abdulrahman Kinana kwa ahadi yake aliyoitoa 2008 ya kuwapatia Sh1
milioni ambayo hajaitimiza.
Mwenyekiti wa
CCM wa tawi la Ifakara mjini, Felista Chakachaka alisema kwamba mwaka
2008, Makamba alipotembelea tawi hilo, aliwaahidi kuwapatia
Sh1 milioni
kwa ajili ya kazi za tawi hilo lakini hakuitekeleza.
Hata hivyo, Makamba aliyeko Bumbuli mkoani Tanga,
alisema jana: “Sawa, mimi nilitoa ahadi hiyo, sikuitekeleza, sasa
aliyepo si ndiyo anatoa...kwani ahadi za Mwalimu Nyerere si Mzee Ali
Hassan Mwinyi kazitekeleza, sawa na ahadi za Benjamini Mkapa ambazo Rais
Jakaya Kikwete anatekeleza.
Akijibu hoja hiyo, Kinana alisema kwa kuwa Makamba
aliahidi kiasi hicho cha fedha akiwa katibu mkuu, basi yeye atatoa fedha
hizo. “Katika kipindi cha wiki mbili fedha hizo zitakuwa zimeingia
katika akaunti yenu..nitawapatia kama alivyoahidi alisema Kinana.
Mbali na kutembelea tawi hilo, Kinana
alifungua mashina ya wakereketwa matano mjini Ifakara.Kinana yuko
ziarani mkoani humo kuangalia maendeleo ya chama hicho tawala.
SOURCE::MWANANCHI:
No comments:
Post a Comment