Mapenzi bwana! Ukiambiwa yanaweza kuua usibishe kabisa, kwani
ukiondoa mifano mingine ya kufikirika, kitu ‘live’ ni kwamba mwanasoka
raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alianguka na kuzimia, baada ya
kupata taarifa mbaya kuhusu mkewe.Ndikumana, alianguka na kuzimia,
asubuhi ya Aprili 8, mwaka huu, baada ya kusoma Gazeti la Ijumaa
Wikienda, lililoandika habari ya usaliti wa mkewe, Irene Uwoya,
aliponaswa hotelini na mwamuziki, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Habari za kuzimia kwa Ndiku, zimewekwa kweupe na Uwoya mwenyewe,
aliyesema: “Maskini Ndikumana wangu, baada tu ya kusoma habari ya mimi
na Diamond alianguka na kuzimia.”
Kwa tafsiri, Uwoya anamsikitikia mume wake
kuanguka na kuzimia, upande wa pili anajuta kumfahamu Diamond, kwani
ndiye aliyemsababishia majanga yote.
Hivi
sasa, Ndiku yupo Rwanda, alitimka nchini baada ya kusoma habari ya
Uwoya na Diamond kunaswa hotelini, ila kabla ya kuondoka, alitamka rasmi
kuvunjika kwa ndoa yao.
Habari ya kuvunjika kwa ndoa,
ilitoka kwa Uwoya mwenyewe ambaye alimweleza mwandishi wetu siku Ijumaa
Wikienda, lilipodondosha ‘jiwe’ hilo mtaani. Uwoya alisema: “Na ndoa
yenyewe imevunjika asubuhi ya leo, kila kitu kimeharibika.”
KWELI
ANAJUTA KUMFAHAMU DIAMOND
Uzungumzaji
na hata sauti, ni dhahiri Uwoya hataki tena kumsikia Diamond, kutokana
na ukweli kuwa ‘brazameni’ huyo, amemharibia kila kitu, ikiwemo
kuipeleka kaburini ndoa yao.
Yafuatayo
ni mahojiano kati ya Uwoya na mwandishi wetu;
MWANDISHI:
Habari za kazi?
UWOYA: Salama tu.
MWANDISHI:
Vipi shemeji yetu hajambo?
UWOYA:
Shemeji gani? (anatukana) mume wangu ameniacha kisa stori ya Diamond.
MWANDISHI:
Duh, imekuwaje tena jamani?
UWOYA:
Alipoona stori ya mimi kuwa hotelini na Diamond, aliumia sana.
Akaanguka na kuzimia.
MWANDISHI: Shida ilikuwa habari
ya Diamond au mgogoro ndani ya ndoa?
UWOYA:
Alipoona ile habari kwenye gazeti alianguka ghafla, akazimia kisha
alipozinduka akarudi kwao. Ameamua kuniacha sijui kama atanirudia.
MWANDISHI:
Pole sana, kwa hiyo familia yako inasemaje kuhusu hilo?
UWOYA:
Familia yangu imenitenga kwa sasa.
MWANDISHI:
Pole sana Uwoya.
UWOYA: Haina haja. Andikeni tu,
mume wangu amenitosa rasmi.
MWANDISHI:
Kwani amekupa talaka ndugu? Maana ndoa haiwezi kuharibika kirahisi.
UWOYA:
Mimi na wewe hatutaniani, nakwambia ndoa yangu haipo tena.
MWANDISHI:
Lakini shemeji yetu anakupenda sana.
UWOYA:
Unataka kuandika hayo? Ukweli familia yangu haitaki kabisa kusikia
habari za Diamond.
MWANDISHI: Kwani magazeti ya
Global hayajasaidia kurejea kwa ndoa yako?
UWOYA:
Mliandika habari nzuri ya ndoa yetu, tukarudiana, mlinisaidia sana na
familia ilifurahi kuona hayo kwa wakati huo.
MWANDISHI:
Sasa nani wa kulaumiwa juu ya ndoa yako?
UWOYA:
Mimi niko ‘siriaz’, nimeachwa.
MWANDISHI:
Ok, asante ndugu.
UWOYA: Asante, Mungu atawalipia
tu.
KUHUSU DIAMOND NA UWOYA
Machi
25, mwaka huu, Diamond na Uwoya, walinaswa na kamera za Global
Publishers Ltd (nyumba kubwa ya magazeti pendwa), kwenye hoteli moja
yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Ijumaa
Wikienda ambalo ni gazeti ndugu na hili, lilianika kila kitu, huku
likiwa na ushahidi wa kutosha jinsi Diamond na Uwoya, walivyolala kwenye
hoteli hiyo, chumba namba 208, wakiingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka
kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.
No comments:
Post a Comment