Saturday, March 16, 2013

Wazimbabwe wanapiga kura ya maoni leo huku wanachama wa upinzani wakidaiwa kushambuliwa.

Wananchi wa Zimbabwe leo wanapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo itaweka kikomo cha muhula wa urais na kuongeza uhuru wa vyombo vya habari. 
Hata hivyo, wasiwasi umeongezeka baada ya wanachama kadhaa wa chama cha upinzani cha Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai kushambuliwa wakati wakifanya kampeni katika kitongoji cha Mbare kwenye mji mkuu Harare, hapo jana.
Msemaji wa chama hicho cha Movement for Democratic Change-MDC, Douglas Mwonzora, amewashutumu wafuasi wa Rais Robert Mugabe kuhusika na tukio hilo.
Katiba hiyo mpya itadhibiti mamlaka ya Rais Mugabe na kuweka misingi ya kufanyika kwa uchaguzi mwezi Julai, mwaka huu.
Uchaguzi huo utahitimisha makubaliano yaliyokumbwa na matatizo ya kugawana madaraka kati ya Rais Mugabe na Waziri Mkuu Tsvangirai.-DW.

MNYIKA::Tutaandamana kudai maji

MBUNGE wa Ubungo John Mnyika leo ataongoza maandamano ya amani kwenda Wizara ya Maji kupata majibu kuhusu matatizo ya maji, licha ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi. 
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, ACP Charles Kenyela amekataza maandamano na mkutano huo kwa madai kuwa eneo la Manzese Bakhresa walilopanga kufanyia mkutano ni maegesho ya magari ya mizigo. 
Akizungumza kwa niaba ya Mnyika, mratibu wa maandamano hayo kutoka ofisi ya mbunge, Gaston Garubindi, alisema kuwa maandalizi yamekamilika na mbunge huyo ataongoza kama ilivyopangwa. 
Garubindi alisema kuwa Kenyela amewadanganya wananchi kwa kueleza kuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe hakuwa na taarifa wakati ofisi ya mbunge ilimwandikia barua yenye kumbukumbu namba OMU/MJ/001/2013 na nakala nyingine kupelekwa kwa viongozi wengine wa wizara hiyo.

RAFIKI WA RAILA ODINGA AMPA TALAKA MKEWE KWA KUMSIFIA UHURU KENYATTA KUWA NI HANDSOME

Rafiki wa karibu wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga Jumatatu hii anadaiwa kumpa talaka mke wake baada ya kumsifia Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta ni ‘handsome’ mbele yake.

Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Kenya, mwanasiasa huyo wa chama cha CORD anayetokea magharibi mwa Kenya, alikuwa akitazama taarifa ya habari akiwa na mke wake na ndipo alipoonekena Uhuru Kenyatta kwenye TV akizungumza na wawakilishi wa nchi mbalimbali nyumbani wake.
Baada ya kumuona mke huyo ambaye ana miaka 30 na kitu alisikika akisema kwa sauti ya chini kuwa anapenda muonekano wa Uhuru Kenyatta.
Hata kabla hajamaliza neno Kenyatta, inadaiwa kuwa mwanaume huyo aliye na ukaribu na Raila Odinga, alimpa kichapo cha haja na kumfukuza nyumbani usiku huo.

Simba hapatoshi leo,mkutano wa wanachama wake wapigwa stop.!

 WAKATI wanachama takribani 700 wanatarajia kufanya mkutano wa dharura leo Mnazi Mmoja, uongozi wa klabu hiyo umepiga stop kumkutano huo kwa madai kuwa wanachama hao hawana haki ya kuitisha mkutano wakati tayari uongozi ulishatoa tamko la kufanya mkutano huo wa dharura wakati wowote kuanzia sasa.

Uongozi huo wa Simba kupitia kwa ofisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga ulisema  kuwa mkutano utakaofanyika leo ni batili kwa kuwa hauna baraka za uongozi na kuwataka wanachama wa Simba kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho mwenyekiti wao Ismail Aden Rage akiwa India kwenye matibabu na anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki ijao.

Kauli hiyo ya uongozi imekuja ikiwa leo wanachama hao wakitarajia kufanya mkutano wao kwa mujibu wa katiba yao ibara ya 22 ambayo inatamka wazi wanachama wasiopungua 500 wana haki ya kuandaa mkutnao mkuu kama mwenyekiti hayupo tayari kuitisha mkutano ndani ya siku 30.

Hata hivyo jana Kamwaga alisema "Mwezi uliopita mwenyekiti alitangaza kuitisha mkutano wa dharura siku yoyote ajenda ingekuwa moja tu kujadili mwenendo wa klabu bahati mbaya alishikwa maradhi ikabidi aende India kutibiwa, kuna uwezekano mkubwa akarejea wiki ijayo.

"Uongozi umeridhia kufanyika kwa Mkutano wa wanachama. Kimsingi, kama uongozi umeridhia, hakuna mwanachama mwingine anayeweza kuitisha mkutano mkuu mwingine, hao wanaoitisha mkutano wana nguvu gani ya kisheria kufanya hivyo?  Walichaguliwa na nani kuwakilisha wanachama? Lini na wapi?" alihoji Kamwaga.

"Uongozi  unaweza kuitisha mkutano kwa vile wenyewe ndiyo wenye leja ya wanachama, Klabu ina database yake ya kompyuta inayotambua wanachama walio hai na wasio hai, hakuna mtu mwingine yeyote, aliye nje ya uongozi huu anayefahamu wanachama walio hai na wasio hai hao wanachama wanaoitana kufanya mkutano, wamehakikiwa na nani kubaini uhalali wao huo?"

Alisema wanachama wanaolazimisha kufanyika kwa mkutano wana ajenda  binafsi na si za maslahi ya klabu, Kama kweli wangekuwa na nia njema na klabu wangesubiri mkutano ambao utaitishwa punde na kwamba mkutano huo wa leo una lengo la kuleta vurugu na mifarakano ndani ya klabu yao.

" Michezo ni amani na furaha na michezo si vurugu,  uongozi wa Simba umetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na ubatili wa mkutano huo, tunapenda kuwaomba wanachama wetu wasiopenda fujo na vurugu kwenye michezo kukaa mbali na mkutano huo kwa vile vyombo vya dola vitaufuatilia.

"Uongozi hautajiingiza katika kutoa dhamana au msaada wa namna yoyote kwa yeyote ambaye atachukuliwa hatua na vyombo vya dola kutokana na kujihusisha na mkutano huo."alisisitiza Kamwaga.
Hata hivyo pamoja na kauli hiyo ya Kamwaga wanachama wa Simba kupitia kwa mmoja wa waratibu wa mkutano huo Mohamed Wandi wamesisitiza kufanyika kwa mkutano huo ambao utakuwa na ajenda mbili moja ikiwa ni mwenendo wa timu yao katika mashindano pamoja na kutokuwa na imani na uongozi wa Rage.

Watu wanne wafikishwa mahakamani wakituhumiwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe..


Marehemu John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe..

*******


Watu wanne wamefikishwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya wakituhumiwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe..
Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe aliaambia Mahakama hiyo Mbele ya Jaji Samweli Karua kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Mei 15,2011 katika Kijiji cha Mpandapanda kata ya Kiwira Wilayani Rungwe kinyume na kifungu cha 196(16) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hakimu Mwakalinga ambaye ndiye mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo akiwa na Daudi Mwasipesya,Obote Mwanyimbili na Kelvin Maurus Myovela ambao wanatuhumiwa kumuua John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Awali baada ya kupandishwa kizimbani watuhumiwa kujibu kesi inayowakabili yenye namba 31/2012 walimkataa Wakili aliyejulikana kwa jina moja laMwakabubu aliyekuwa ameteuliwa kwa ajili ya kuwatetea kwa madai kuwa hawana imani naye kutokana na mwenendo wa kesi alizosimamia.
“Mtukufu Jaji kabla ya kesi yetu haijaanza kusikilizwa tunaomba kubadilishiwa Wakili kwa sababu huyu Mwakabubu hana uwezo na tumeona kesi ndogo tu anababaika na kesi yetu ni kubwa tunaona wazi kabisa kuwa hataweza kututetea” alisema Mwakalinga Mshitakiwa namba moja.
Kufuatia ombi hilo Jaji Karua alikubaliana nao ambapo alimteua Wakili mwingine ambaye ni Sambwee Shitambala ambaye walimkubali kabla hajawaongezea wakili mwingine ili asaidiane na Shitambala ambapo alimtaja Wakili Zakia Selemani.
Akisoma mashtaka yao Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 19, Mei 2011 majira ya jioni marehemu akiwa anatokea Mbeya mjini akirudinyumbani kwake Kiwira Wilayani Rungwe alifika Nyumbani akiwa na gari lenye namba za usajili T 127ACZ Nissan (Double cabin).
Namkambe aliongeza kuwa baada ya kufika nyumbani kwake alipiga honi ya gari kwa ajili ya kuomba kufunguliwa geti la mlango ambapo baada ya kusikia honi hiyo alitoka Mjomba wake ambaye baada ya kumfungulia aliambiwa ashushe Kuku aliyokuwa amewabeba nyuma ya gari yake.
Alisema kabla ya mjomba wa Marehemu hajaanza kushusha kuku kwenye gari alitokea mshitakiwa namba moja akiwa na siraha ambapo alimwamuru asifanye lolote ndipo akaanza kufyatua risasi akimwelekezea marehemu kisha kumuuana kutoweka kusiko julikana.
Akijibu tuhuma hizo Wakili wa Utetezi Shitambala na Zakia walikana washtakiwa hao kuhusika na matukio hayo pamoja na baadhi ya vielelezo vilivyotolewa na upande wa mashtaka kuthibitisha kuhusika kwa wateja wao.
Walisema mtuhumiwa wa kwanza hakuwepo Wilayani Rungwe siku ya tukio ambapo walisema atakuwa na mashahidi ambao watathibitisha kwamba hakuhusika ambao waliwataja kuwa ni pamoja na yeye mwenyewe, Askari Magereza wawili wa gereza la Tukuyu Wilayani Rungwe waliotajwa kwa jina moja moja la Hereda na Green.
Wengine ni Padeso Mwakipesile, Aneth Siandene Kalinga na Jumanne Mwakisole huku washtakiwa namba mbili, tatu na nne ambao hawatakuwa na mashahidi ambapo watasimama wao wenyewe kujitetea.
Namkambe aliiambai mahakama hiyo kuwa upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi zaidi ya 15 ambao aliwataja kuwa ni pamoja na Sofia Fungameza, Weston Gilbert,Magdalena Mgawe, Musa Jackson, Issa Mwaipopo, Teresia Ludovick na Williamu Mtanga.
Wengine ni askari Polisi Mwenye namba D2385 Sajent Michael wa Tukuyu, Inspekta Isaya Bwile wa Tukuyu, David Paul kutoka makao makuu ya Polisi Dar Es Salaam, Twaha kutoka kitengo cha Upelelezi makao makuu ya Polisi Dar Es Salaam, Haruna kutoka Polisi Tukuyu na WP3433 Agnes wa polisi Tukuyu.
Namkambe aliwataja mashahidi wengine katika kesi hiyo kuwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelezi (RCO) Mkoa wa Mbeya aliyehamishiwa makao makuu SSP Anacletus Malindisa, John Mayunga na Dk. D Z Matata kutoka ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali.
Jaji Karua aliahirisha kesi hiyo hadi hapo itakapopangwa tena kwa ajili ya kuendelea na kuwasilikiza mashahidi kutoka upande wa mashtaka baada ya kuambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika na mashahidi wote wako tayari.
Na Venance Matinya, Mbeya.

BREAKING NEWZZZZZ .... Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku Maandamano ya Chadema Leo, Latoa Sababu Za Kupiga Marufuku Maandamano

 
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela
---
Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam kanda ya Kinondoni limekataza maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika tarehe 16 Machi 2013 yaliyokuwa yameiratibiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika yaliyolenga kufika katika Wizara ya Maji ili kufikisha ujumbe kwa Waziri wa Maji, Prof Maghembe kuhusu kero ya maji katika jimbo hilo ambayo haijatatuliwa wala kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela amesema endapo maandamano hayo yatafanyika:
   
 1. Upo wasiwasi wa kutokea kwa vurugu pale watakaposhindwa kufikia muafaka kuhusu hoja zao.

2. Amewasiliana na Ofisi ya Waziri husika na kufahamishwa kuwa haina  taarifa rasmi za ujio wa maandamano hayo.

 3. Barabara yatakakopita maandamano hayo ipo katika ujenzi na hivyo  maandamano hayo yatazuia shughuli za mkandarasi kukamilisha kazi yake kwa  wakati na kuisababishia Serikali hasara.

  4. Eeo ambamo maandamano hayo yanakusudiwa kutamatia ni dogo na hivyo  itasababisha usumbufu mkubwa
 
Credits: Lukaza Blog

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU KWA PAPA FRANCIS WA KWANZA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Ijumaa 15 Machi, 2013 mchana amemtumia salamu za Pongezi Baba Mtakatifu Francis I kwa kuchaguliwa kwake kuwa Papa wa kanisa Katoliki Duniani na Vatican.
“Kuchaguliwa kwako ni ushuhuda tosha wa imani na heshima kubwa ambayo kanisa Katoliki inayo kwako, historia yako  na upendo wako wa kujali na kuwapenda wanyonge, unyenyekevu ni sababu tosha ya kuwapa wakatoliki, wasio wakatoliki na wasio wakristo pia kusherehekea uteuzi wako” Rais Kikwete amesema kwenye barua yake ya Pongezi kwa Papa Francis I.
Vatican na Tanzania imekua na uhusiano wa muda mrefu na hivyo Rais Kikwete amemhakikishia Papa Francis kuwa uhusiano huo utadumu na anatarajia utaimarika zaidi chini ya uongozi mpya wa Papa Francis I

“Mwisho”
Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
IKULU
DAR ES SALAAM
15 March, 2013

Waziri Dkt. Mwakyembe abariki uzinduzi wa ‘Showroom’ mpya ya Magari ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (kulia) akiongozana na  Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani (kushoto) baada ya kuupokea Ujumbe kutoka nchini Ujerumani kunakotengenezwa magari aina ya Volks Wagon walipofika kushuhudia uzinduzi wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos wauzaji wa magari ya Volkswagon. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mh. Klaus Peter Brandes aliyeambata na ugeni huo.
  Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya  Kampuni ya Alliance Autos iliyopo Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa CFAO Motors Mama Maria Petro akipokea wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa pamoja na ujumbe wa wafanya biashara kutoka Ujerumani walioongozwa Balozi wa Ujerumani nchini Klaus –Peter Brandes katika hafla ya kuzindua Showroom ya magari ya kampuni ya Alliance Autos inayouza magari aina ya Volkswagon ambapo pamoja na mambo mengine amepongeza hatua hiyo na kusema serikali iko bega kwa bega na wafanya biashara wabunifu na pia kuuhakikishia ujumbe kutoka Ujerumani kuwa serikali imeweka mazingira bora ya kuwekeza hivyo wasisite kujitokeza.

Thursday, March 14, 2013

Mchumba wa Bwana Misosi asema na yeye ya Moyoni baada ya Wema Sepetu Kunyoa nywele


MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa katika maisha yake hakuna kitu anachokichukia kama kushikwa nywele.
 
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Amanda alibainisha kuwa kama ingekuwa ni hiari yake basi angenyoa hata kipara ili asipate usumbufu wa kwenda kushikwa nywele saluni.

“Kwa kweli mwenzenu sijui nipoje, sipendi mtu anishike nywele zangu... yaani sijui najisikiaje,” alisema Amanda ambaye ni mpenzi wa Mbongo Fleva  Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’.

DIAMOND ATANGAZA KUJENGA MSIKITI

Kwa mujibu wa staa huyo ambaye kwa sasa anaminya kimapenzi na mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’, msikiti huo utakuwa kumbukumbu yake kwa watakaoutumia kama sehemu ya kurudisha kwa…
 Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Na Sifael Paul Global Publishers
SIKU chache baada ya kuwachefua Waislamu wenzake kwa kutimba kwenye Maulid na kuomba dua akiwa amevaa hereni na mkufu, msanii wa Bongo Fleva mpenda totoz, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kujenga msikiti jijini Dar es Salaam, kwani ni jambo alilolipanga kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa staa huyo ambaye kwa sasa anaminya kimapenzi na mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’, msikiti huo utakuwa kumbukumbu yake kwa watakaoutumia kama sehemu ya kurudisha kwa jamii inayompa sapoti kubwa.
Diamond ambaye amemjengea mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ nyumba ambayo hadi sasa imegharimu Sh. milioni 260 alifunguka: “Ninajitahidi sana kununua viwanja au vinyumba vidogovidogo maeneo tofauti. Nipo kwenye plan (mpango) ya kujenga msikiti japo sijapanga sehemu hasa hadi nipate eneo la kutosha.
“Nataka iwe kumbukumbu ili hata kesho na keshokutwa nikifa, vizazi vijavyo wawe wanaswali kwenye msikiti uliojengwa na Diamond.
“Kwa kufanya hivyo itanipa baraka kubwa sana na soon tu nina imani mwenyezi Mungu atanisaidia nijenge huo msikiti.”

PAPA MPYA FRANCIS 1 AMEANZA KAZI


Papa mpya Francis Vatican

   

....akiwa pungia mkono waumini waliofika eneo hilo wakati wa kutangazwa kwake
 
Kazi ya kuchaguwa wasaidizi…
 
Papa Francis I (katikati) akiwa na Kardinali Santos Abril wa Hispania (kushoto) na Kardinali Agostino Vallini ambaye pia ni Kasisi Mkuu (Vicar General) wa Roma (kulia) wakiupungia umati leo asubuhi.
 

Papa Francis I akihutubia kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa.
 
....akiwapungia mkono waumini waliofika eneo hilo wakati wa kutangazwa kwake.
Siku yake ya kwanza ofisini kama Papa mtakatifu wa kanisa Katoliki, Papa Francis 1 tayari anaanza kazi. Papa anatarajiwa kuwateua
wafanyakazi wakuu watakaohudumu katika Vatican chini ya uongozi wake. Ameanza siku yake kwa maombi ya kibinafsi katika hekalu ya mtakatifu Maria Maggiore mjini Rome. Baadaye Papa atafanya misa ya sherehe katika kanisa la Sistine.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa uteuzi atakaofanya Papa Francis, utatizamiwa kama ishara ya mageuzi katika uongozi uliozongwa na kashfa nyingi na pia utaonyesha mwelekeo anaonuia kuchukua kwa kanisa hilo.
Baadaye wikendi ijayo, Papa mpya anatarajiwa kukutana na vyombo vya habari vya dunia katika mkutano maalum.
Na Jumapili, ataongoza misa yake ya kwanza kama papa. Hata hivyo yeye mwenyewe atatawazwa rasmi kuwa Papa Francis 1, siku ya Jumanne.
Chanzo: BBC SWAHILI

Timuatimua yawakera wanafunzi vyuo vikuu

RAIS Jakaya Kikwete ameombwa kuchukulia kwa uzito vitendo vya timuatimua wanafunzi katika vyuo vikuu vya umma kutokana na wanafunzi hao kudai haki wanazopaswa kuzipata wawapo vyuoni.
Msemaji wa Umoja wa  Wanafunzi waliofukuzwa  katika Vyuo Vikuu nchini (UUEST), Philipo Mwakibingwa, alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa umoja huo na kusema kuwa lengo kubwa la umoja huo ni kutetea wanafunzi waliofukuzwa.
Alisema tangu miaka ya 2000 hadi sasa, suala hilo limezidi kukua nchini, watawala wa vyuo vikuu ambao ni maprofesa na baadhi ya viongozi waliopo serikalini kulichukulia kama mila na desturi.

Mwakibingwa alisema wanafunzi hao wamekuwa wakifukuzwa kutokana na kutoa mawazo mbadala, kuhoji mambo, kukosoa uovu uliopo na unaondelea kutendeka ndani ya vyuo, hivyo na kutoa ushauri pale inapobidi kwa masilahi ya taifa lao.

Akizungumzia umoja huo, alisema wamefikia hatua ya kuunda umoja huo kutokana na serikali pamoja na Bunge kushindwa kutatua matatizo yao na kuongeza kuwa hali hiyo imesababishwa na taarifa potofu zilizotolewa na watawala wa vyuo vikuu hivyo.

“Kwa sababu watawala wa vyuo vikuu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kututenganisha na jamii zetu, familia zetu, jamaa, viongozi wetu wa kidini na asasi kwa taarifa za uongo kupitia vyombo vya habari, tumeona suluhu ya maisha yetu ni kuungana. Muungano huu umeundwa kwa ajili ya kutetea maisha yetu,” alisema Mwakibingwa.

CHADEMA yalisulubu Bunge

WANASHERIA wameunga mkono msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wale wa NCCR- Mageuzi kupinga hatua ya Ofisi ya Bunge kuliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata wabunge wake ili wakahojiwe.
 Wakizungumza mwanasheria mashuhuri hapa nchini na wakili wa kujitegemea, Mathew Kakamba, alisema ni kinyume cha sheria na ni matumizi mabaya ya madaraka kwa Ofisi ya Bunge kutumia polisi kuwakamata wabunge katika masuala yanayolihusu Bunge.

Wanasheria hao walitoa maoni yao kuhusiana na mvutano mkubwa wa kisheria uliozuka baina ya CHADEMA na Ofisi ya Bunge ambayo imeagiza kukamatwa kwa wabunge kadhaa wa upinzani ili wakahojiwe na Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, ambayo CHADEMA wanadai kuwa haipo.

Wakili Kakamba katika maoni yake alisema ni makosa kisheria kutumia nguvu za mhimili mwingine katika kuendesha masuala yanayohusu mhimili wa pili.

“Kuna mgogoro unaojulikana kwa  Watanzania karibu wote kuhusiana na vurugu zilizotokea katika mkutano wa Bunge lililokwisha, na kuvunjwa kwa kamati za kudumu za Bunge.

“Pamoja na kuvunjwa kwa kamati hizo, bado kama sikosei, wajumbe wake hawajateuliwa na kwa maana hiyo, kisheria utendaji wake haujaanza. Kwa lugha nyingine, haziwezi kuitwa kamati rasmi kwa sababu hazina wajumbe,” alisema Wakili Kakamba.
Kauli ya Wakili Kakamba imeungwa mkono na wakili mwingine, Aloyce Komba, ambaye  amekiita kitendo cha Ofisi ya Bunge kutumia polisi kuwakamata wabunge wao wa upinzani kuwa ni udhalilishaji mkubwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Komba anayetoka Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza, alisema Bunge ni chombo kinachojitegemea na linazo sheria na kanuni zinazopaswa kutumika kumlazimisha mbunge kutimiza agizo la wito.

“Masuala yote ya Bunge yanatakiwa kuendeshwa kibunge bila kutegemea vyombo vingine vya nje, labda tu ikiwa kuna mwingiliano kutoka katika mhimili mwingine.
“Si sahihi kwa spika kutumia polisi kuwakamata wabunge wakati wanazo kanuni na taratibu nzuri tu, na sidhani kama ni utaratibu mzuri na unaolenga kudumisha demokrasia.
“Mbunge akishindwa kufika, kwani hakuna sheria nyingine hata za kuzuiwa kuhudhuria vikao kadhaa vya Bunge, hadi leo wanataka kutumia polisi kuwakamata?” alihoji Komba.

Akizungumzia uhalali wa kamati hizo, Komba ambaye ni mtaalamu wa sheria katika mambo ya utawala, alisema kimsingi hazipo, kwa sababu tangu kuvunjwa kwake na kuundwa nyingine, bado spika hajateua wajumbe wa kamati mpya.
“Hajateua wajumbe wa kamati hizo, na ni sawa kabisa kuwa hazipo. Sasa wanaitwa kuhojiwa na kamati gani? Mtazamo wa kisheria ni kwamba hazipo.

Alikwenda mbali zaidi na kuilaumu Ofisi ya Bunge kwa madai ya kuvunja haki za msingi kwa sababu aliyetendewa kosa ni spika (kiti), anayelalamika ni spika, mteuzi wa kamati ni spika na ushahidi mwingi utatoka kwa spika, hivyo kupingana kabisa na haki za sheria ambazo mlalamikaji hapaswi tena kuwa mwendesha mashitaka.
Hata hivyo, mawakili hao walikubaliana na kuwataka wabunge wote waliopata barua za wito kutoka Ofisi ya Bunge kuitikia na si kukaidi.
“Pamoja na kasoro hizo, kama wameitwa na Ofisi ya Bunge, wanatakiwa kwenda na si kugoma. Huko ndiko mahali pekee wanakotakiwa kuwakosoa hao wakubwa, na hata wanao uwezo wa kukataa kuzungumza hata kama kamati yenyewe ingekuwa hai kisheria,” walisema wanasheria hao.

CHADEMA wagoma
Juzi  Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alimwagiza Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni kuiandikia barua Ofisi ya Bunge ya kukataa wabunge wake kukamatwa na polisi ama kuhojiwa na kamati waliyodai ni hewa, kwa kuwa zilizokuwapo zilivunjwa na Spika Anne Makinda katika kikao kilichoisha mwezi uliopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kisheria, kanuni na taratibu za Bunge, kamati ambazo zimeshavunjwa haziwezi kufanya kazi yoyote kwa kuwa ni batili mpaka hapo zitakapoundwa kamati nyingine.

Alilitaka Bunge kurejea kanuni za kudumu za Bunge namba 113 (7), inayozungumzia ukomo wa uhai wa kamati za Bunge, uhai wake unaishia Mkutano wa Kumi wa Bunge ambapo inakuwa ni nusu ya kwanza ya uhai wa Bunge lenyewe.
Dk. Slaa alisema kutokana na kifungu hicho, inaonesha dhahiri kwamba Spika Anne Makinda na wasaidizi wake wana matumizi mabaya ya sheria, kutoifahamu vizuri ama kulewa madaraka, hali ambayo CHADEMA haitakubaliana nao.

Hivyo alisema Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge ambayo ilikuwa chini ya Mbunge wa Mlalo, Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi (CCM), haitawahoji wabunge wake kwa kuwa imekwisha kumaliza kazi yake tangu Februari 8, mwaka huu.
Msimamo wa CHADEMA unakuja zikiwa ni siku mbili tangu Ofisi ya Bunge kupitia Katibu Mkuu, Dk. Thomas Kashililah, itumie Jeshi la Polisi kuwataarifu baadhi ya wabunge wa chama hicho kuwa wanahitajika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kamati hiyo.

Katibu Mkuu huyo alisema kama wabunge wa CHADEMA wanaitiwa kuhusu vurugu zilizotokea bungeni Februari 4, mwaka huu, tayari zimeshatolewa hukumu yake kwa kuwataja wahusika kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), John Mnyika (Ubungo), Paulina Gekul (Viti Maalumu) na Joshua Nassari ( Arumeru Mashariki).

Alisema katika hukumu hiyo ambayo ilisomwa na Spika Makinda ilikuwa ya upande mmoja wa kamati yenyewe iliyokaliwa na wabunge wa CCM ambao waliwaona wabunge wa CHADEMA pekee ndio waliofanya vurugu huku ikishindwa kuwaita wahusika kwa mahojiano.
Aidha, alisema hata kama kamati ya Brigedia Ngwilizi ingekuwa hai, wabunge wake wasingeitii, kwa kuwa tayari imekwisha kuwahukumu.
Hata hivyo Dk. Slaa alitumia nafasi hiyo kumtaka Spika Makinda kwenda kozi kwa ajili ya kujifunza sheria za kuongoza Bunge kutokana na kushindwa kwake katika kipindi chote alichokalia kiti hicho.
“Nasikia Spika Makinda huwa anasema kuwa niwafundishe wabunge wangu sheria, kanuni na  taratibu za Bunge kwa kuwa nazifahamu vizuri, kwani yeye na wanasheria wake wanafanya nini? Kupoka kwake sheria na taratibu za bungeni ndizo zinazosababisha vurugu?” alihoji Dk. Slaa na kuongeza:
“Nataka nimwambie kwamba wakati nipo bungeni, maspika waliokuwa wakiongoza Bunge akiwamo Samuel Sitta walikuwa wakijua kuongoza, kwa kufuata sheria na kanuni zake na ndiyo maana hakuna vurugu zilizokuwa zikitokea na si yeye.”
Aidha, alisema maspika hao walikuwa wanajua kwamba mabunge yote ya Afrika na yale ambayo Tanzania inaiga kutoka kwao yana sheria na taratibu zinazowaruhusu kushangilia hata kuzomea kwa kutaja chama chao na si hivi ambavyo Spika Makinda anavyofanya.
Lissu anena
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Lissu alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni za Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, zinamtaka Katibu Mkuu wa Bunge Dk. Kashililah kuandika barua hizo kwa niaba ya Spika Makinda lakini hakufanya hivyo.
Lakini pia Lissua alisema hata barua ya polisi (police message) waliyopewa si taarifa tosha ya kujipeleka wao kuhojiwa bali walipaswa kupelekewa taarifa ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano na Bunge.
Kutokana na maelezo hayo Lissu alisema hakuna jambo lililofuatwa kisheria, hivyo hakuna watakayemwona, na alidai kuwa tayari hukumu yao ilishatolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Brigedia Ngwilizi Februari 8, mwaka huu.

WANYARWANDA WAKOMALIA NDOA YA UWOYA

KATIKA kile kilichoonekana ni kuikomalia ndoa ya msanii wa filamu Bongo Irene Uwoya, baadhi ya wadau nchini Rwanda wameendelea kutambua kuwa yeye ni mke halali wa msakata kabumbu, Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Hayo yalibainika hivi karibuni baada ya Uwoya, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Jacob ‘JB’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ kutua nchini humo kuhudhuria utoaji wa tuzo za filamu zilizopewa jina la Rwanda Movies Awards.
Wakiwa Rwanda, matangazo yaliyokuwa yakirushwa kupitia redio na televisheni yaliainisha kuwa Uwoya ni mke wa Ndikumana, kitendo kilichowashangaza wasanii hao.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, inavyoonekana Wanyarwanda wengi hawataki kuamini kuwa ndoa ya Uwoya na Ndiku haipo na ndiyo maana wameikomalia.
“Katika matangazo yaliyokuwa yakisikika katika redio na televisheni, jina lililokuwa linatajwa ni Oprah umugore wa Kataut, wakimaanisha Oprah mke wa Kataut.
“Jina la Oprah kwa Uwoya limekuwa maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday iliyowashirikisha yeye, Ray na marehemu Kanumba,” kilieleza chanzo hicho.
Chanzo Global Publishers

ADAIWA KUMCHINJA MPENZI WAKE KAMA KUKU

Na  Globalpublishers
VILIO vilitawala Kata ya Nyahanga wilayani hapa wakati wa kuuaga mwili wa binti Jessica Elialinga (19) aliyeuawa kinyama kwa kuchinjwa kama kuku na mpenzi wake, Musa Petro (27) mkazi wa Shunu kwa sababu zinazodaiwa ni wivu
wa kimapenzi.
Tukio hilo lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana, lilijiri saa 12:45 Februari 6, mwaka huu.
Kitendo hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la kutaka kujitoa roho kwa kisu.
Akisimulia juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.
 “Unajua Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake kama mzaha.
“Alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kwa mpenzi wake huyo tangu walipoanza uhusiano, msichana akiwa kidato cha pili, lakini anatoka kimapenzi na mwanaume mwingine,” alisema rafiki huyo.
 Hata hivyo, inadaiwa baada ya mtafaruku wa usaliti, wawili hao walipatana na kuendelea na mapenzi, lakini baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha nne alibadilika ambapo mwanaume alisikia kuwa tayari ana mwanaume mwingine kutoka jijini Mwanza ambaye walikubaliana kufunga pingu za maisha baada ya kumaliza masomo.
 Inadaiwa siku chache kabla ya mauaji hayo, rafiki mmoja wa karibu wa mtuhumiwa alikutana na marehemu njiani na kumsimamisha kwa lengo la kumweleza kauli zenye kutishia maisha yake anazozitoa mpenzi wake, lakini binti huyo hakusimama kumsikiliza.
 Baada ya Musa kudaiwa kufaulu kumchinja mpenzi wake huyo na yeye kujikata koromeo na kuanguka akiwa ameishiwa nguvu, kijana mchunga mbuzi ambaye wengi katika eneo hilo humchukulia kama kaka yake Jessica, ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshuhudia Musa akiwa katika hali hiyo.
Alipomhoji kulikoni, hakupata jibu zaidi ya kushuhudia jitihada za mtuhumiwa huyo kufungua mlango wa chumbani mwake zikishindikana.
Kijana huyo alitoa taarifa kwa watu ambao walifika na kumchukua Musa na kumkimbiza hospitali ya wilaya kuokoa uhai wake.
 Watu waliobaki nyumbani walifuatilia michirizi ya damu hadi kwenye zizi la mbuzi ambako walimkuta Jessica ameshafariki dunia baada ya kuchinjwa.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Everest Mangala alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kahama katika Hospitali ya wilaya hiyo anakoendelea kupatiwa matibabu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...