Thursday, March 14, 2013

Timuatimua yawakera wanafunzi vyuo vikuu

RAIS Jakaya Kikwete ameombwa kuchukulia kwa uzito vitendo vya timuatimua wanafunzi katika vyuo vikuu vya umma kutokana na wanafunzi hao kudai haki wanazopaswa kuzipata wawapo vyuoni.
Msemaji wa Umoja wa  Wanafunzi waliofukuzwa  katika Vyuo Vikuu nchini (UUEST), Philipo Mwakibingwa, alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa umoja huo na kusema kuwa lengo kubwa la umoja huo ni kutetea wanafunzi waliofukuzwa.
Alisema tangu miaka ya 2000 hadi sasa, suala hilo limezidi kukua nchini, watawala wa vyuo vikuu ambao ni maprofesa na baadhi ya viongozi waliopo serikalini kulichukulia kama mila na desturi.

Mwakibingwa alisema wanafunzi hao wamekuwa wakifukuzwa kutokana na kutoa mawazo mbadala, kuhoji mambo, kukosoa uovu uliopo na unaondelea kutendeka ndani ya vyuo, hivyo na kutoa ushauri pale inapobidi kwa masilahi ya taifa lao.

Akizungumzia umoja huo, alisema wamefikia hatua ya kuunda umoja huo kutokana na serikali pamoja na Bunge kushindwa kutatua matatizo yao na kuongeza kuwa hali hiyo imesababishwa na taarifa potofu zilizotolewa na watawala wa vyuo vikuu hivyo.

“Kwa sababu watawala wa vyuo vikuu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kututenganisha na jamii zetu, familia zetu, jamaa, viongozi wetu wa kidini na asasi kwa taarifa za uongo kupitia vyombo vya habari, tumeona suluhu ya maisha yetu ni kuungana. Muungano huu umeundwa kwa ajili ya kutetea maisha yetu,” alisema Mwakibingwa.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...