KIMENUKA!
Vigogo wa madawa ya kulevya wakiwemo viongozi wa dini sasa wanaanza
kupukutika kutoka kwenye mstari wa siri huku baadhi yao wakikimbilia nje
ya nchi kufuatia oparesheni kali inayofanywa na Kikosi cha Kupambana na
Kudhibiti Madawa ya Kulenya Tanzania kuwanasa kila kukicha, Uwazi lina
mchoro kamili.Askofu Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Hivi karibuni kikosi hicho kimemkamata askofu (mwangalizi mkuu wa
kanisa) aliyetambulika kwa jina la Emeka Nwachukwu Mert raia wa Nigeria
ambaye ana kanisa la kiroho maeneo ya Sinza jijini Dar.
Jina la kanisa hilo limedhibitiwa na vyombo husika kwa sababu ya uchunguzi zaidi na uhalali wake wa kuwepo nchini.
SIKU YA TUKIO
Vyanzo vyetu makini ndani ya
kikosi kazi vinaeleza kwamba, mchungaji huyo alikamatwa Oktoba 31, mwaka
huu saa kumi usiku Tegeta wilayani Kinondoni, Dar es Salaam akiwa na
madawa ya kulevya ‘unga’ aina ya heroine kilo 35.
KAMA UNGEINGIA SOKONI
Habari za ndani kutoka
kwenye oparesheni hiyo zinasema kuwa, endapo unga huo ungeingia sokoni
na kununuliwa, basi mtumishi huyo wa Mungu angevuna kitita cha zaidi ya
shilingi bilioni mbili.
NYUMBA ALIYONASIWA YA PROFESA
Mchungaji huyo
ambaye serikali imeanza kazi ya kulichunguza kanisa lake, alidakwa na
mzigo huo haramu kwenye makazi aliyopanga ambayo ni nyumba ya profesa
mmoja wa chuo kikuu, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Askofu akiwa chini ya ulinzi.
WASHIRIKA NAO WADAKWA
Kwa mujibu wa chanzo,
kamatakamata ya mchungaji huyo pia iliwakumba watuhumiwa wengine ambao
ni Walyat Khan raia wa Pakistani, Chuksi Sylvester Agbazuo na Tony
Olafor wote raia wa Nigeria na inadaiwa kwamba walikuwa wakikamatwa
maeneo mbalimbali na kutoroka.
HABARI NYETI
Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz