Wednesday, November 12, 2014

HII NDIO SAA GHALI ZAIDI DUNIANI

Saa ghali zaidi duniani iko Uswiss
Saa ghali zaidi duniani imenunuliwa mnadani huko Geneva,Uswiss kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 21.3.
Saa hiyo imetengenezwa kwa kutumia karati ishirini na moja za dhahabu na ina uzito wa nusu kilo,saa hiyo iliyoundwa kwa mbwembwe ilitengenezwa mahsusi kwa ajili ya mtoto wa mfanya biashara,Henry Graves mnamo mwaka 1930.
Na ilimchukua miaka nane kwa watengeneza saa maarufu wa Uswis kuikamilisha hiyo saa ghali ambaye ni Patek Philippe.
Saa hiyo ilinunuliwa siku mbili tu baada ya mmiliki wa mwisho kufariki dunia kutoka falme za kiarabu Saud Bin Mohammed Al-Thani.
Mmiliki huyo alikuwa na madeni mengi ambayo yangemgharimu nyumba yake kuuzwa na hivyo akaikabidhi saa hiyo kwenye nyumba ya mnada ya Sothebys. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...