Spika mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa akikusanya baadhi ya vitabu
alivyoviandika alipokuwa akifanya mahojiano na wahariri wa gazeti hili
nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Makamu
Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa ametoboa
siri ya chama hicho kung’ang’ania Muungano serikali mbili akisema hiyo
ndiyo sera yake pekee iliyopitishwa na wanachama wake wote kwa kura ya
maoni.
Msekwa alieleza hayo katika mahojiano maalumu na wahariri wa gazeti hili yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam.
Msekwa ambaye katika habari iliyochapishwa na
gazeti hili jana alieleza kuwa binafsi, hana tatizo na suala la idadi ya
Serikali katika Muungano, alisema kamwe hawezi kukishauri chama chake
kukubaliana na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ya muundo wa serikali tatu.
“Siwezi kuishauri CCM kukubali serikali tatu. Hili
la Serikali mbili ni sera ya CCM, siyo tu sera ya kawaida, bali hii ni
sera pekee iliyopitishwa na wanachama wote kwa kura ya maoni,” alisema
Msekwa ambaye pia ni Spika mstaafu wa Bunge.
Alisema tofauti na sera hiyo ya serikali mbili,
sera nyingine za chama hicho huanzia katika ngazi ya Kamati Kuu,
kujadiliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na kupitishwa na Mkutano
Mkuu wa Taifa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz



























