Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora na Wadaau wa Usafiri
wamependekeza uanzishwaji wa matumizi ya vitabu (log book) kwa magari ya
mizigo ili kudhibiti madereva kusafiri mwendo mrefu bila kupumzika na
hivyo kusababisha ajali kwa magari yao au kugongana uso kwa uso na
magari mengine kutokana na uchovu.
Tamko hilo limetolewa jana wilayani
Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya kikao cha
kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za barabarani
mkoani humo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitabu hivyo
vitasaidia kuonyesha muda alitoka , mahali alitoka na kama amesafiri
muda mrefu atalazimisha apumzike ili kuepusha ajali.