Thursday, April 05, 2018

CHADEMA WATAJA MAJINA 25 YA WAFUASI WAKE WANAOSHIKILIWA NA POLISI BILA KUPELEKWA MAHAKAMANI

Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa orodha ya majina ya watu 25, wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam na kuwaagiza wanasheria wake kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa kuwasilisha maombi ya ‘Habeas Corpus’, Mahakama Kuu, iwapo jeshi hilo halitawaachia au kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao kama taratibu zinavyotaka.

Chama hicho kimesema kimefikia uamuzi huo, kutokana na tabia ya Jeshi la Polisi kuendeleza utaratibu unaovunja haki na sheria kwa kuwakamata watu na kuwashikilia mahabusu za Polisi kinyume na matakwa ya taratibu za nchi.

Kati ya watu hao 25 wanaoshikiliwa na Polisi, mmoja ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, John Heche, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijiji huku watu wengine 24 wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA waliikamatwa juzi wakiwa maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakifuatilia hatma ya dhamana ya viongozi wakuu wa chama mahakamani hapo.

 Aidha kimedai kuwa miongoni mwa watu hao 24, wamo pia wananchi ambao walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kila siku lakini walikumbwa na kamatakamata hiyo iliyofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala.

Majina ya watu hao 25 wanaoshikiliwa na polisi ni:-
1. John Heche (Mb Tarime Vijijini)
2. Lilian Kumei
3. Jonathan Lema
4. Beatrice Mdanya
5. Charles Kakumbi
6. Neema Nyimbo
7. Elizabeth Tossy
8. Ernest Mbuya
9. Damas Mwita
10.Daniel Mshana
11. Paul Shija
12. Jerry Kerenge
13. Patrick Peter
14. Christina Darabe
15. Adinani Mushi
16. Mbezi Mombeki
17. Jonathan Kimaro
18. Paulo Makali
19. Meshak Mwacha
20. Godfrey Jackson Kayanda
21. Ramadhani Mkude
22. Happy Baega
23. Novatus Tesha
24. Jonathan Robert
25. Fikirini Vicent

CHADEMA wameeleza kuwa wanakwenda mahakamani, ili Mahakama Kuu iliamuru jeshi hilo na mamlaka zingine zinazohusika, kujieleza kwanini zinavunja haki na sheria kwa kuendelea kuwashikilia watu hao bila kuwaachia au kuwafikisha Mahakamani.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...