Saturday, April 07, 2018

MARAIS WALIOPANDISHWA KIZIMBANI NA KUHUKUMIWA KIFUNGO WIKI HII

  Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma
 
Wiki hii tumeshuhudia baadhi ya marais wastaafu wa nchi mbalimbali wakifikishwa mahakamani kusomewa mashtaka na wengine kuhukumiwa vifungo gerezani. Miongoni mwa marais hao ni:-

Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma amefika mahakamani kujibu mashtaka ya ulaji wa rushwa yanayohusishwa na mkataba wa ununuzi wa silaha miaka ya tisini.

Baada ya Zuma (75) kufika mbele ya Mahakama Kuu kwa dakika 15 huko Durban, kesi hiyo iliahirishwa hadi tarehe 8 mwezi Juni.

Ameshtakiwa kwa makosa kumi na sita ya ulaji wa rushwa, ufisadi, ulaghai na ulanguzi wa fedha, aliyoyaepuka wakati wa utawala wake na kurejeshwa tena mwaka 2016. Bw Zuma alitolewa madarakani kwa nguvu mwezi Februari mwaka huu.
  Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geuin Hye 
Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geuin Hye  

Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Park Geuin Hye, amehukumiwa kifungo cha miaka 24 jela, baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi, iliyomuondoa madarakani.

Mahakama hiyo pia imempiga faini ya takriban dola milioni 17 baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka kumi na sita zikiwemo, kupokea hongo, matumizi mabaya ya madaraka na kutawala kwa vitisho.

Mahakama iliamua kuwa Bi Park, alitumia wadhifa wake vibaya kushawishi kampuni kuchangia fedha wakfu kadhaa zilizoongozwa na mshirika wake.
Luiz Inacio Lula da Silva, Rais wa zamani wa Brazil

Mahakama ya rufaa nchini Brazil Alhamisi nayo iliagiza kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva, ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka kumi na miwili gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na ufisadi.

Majaji watano kati ya kumi na mmoja wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watatu kati yao wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasiwasi kisiasa nchini humo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...