Friday, April 06, 2018

UKUTA WA MADINI YA TANZANITE KUZINDULIWA LEO

 Rais wa jamuhuri ya muungao wa Tanzania Dr. John Magufuli, leo anatarajia kuzindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite, iliopo eneo la Mererani, mkoani Arusha.

Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umejengwa kufuatia agizo lililotolewa na Rais John Magufuli, kama jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.
Mwezi Februari mwaka huu, wakuu wa vyombo vya usalama, walitembelea eneo hilo, kuukagua ukuta huo uliojengwa kwa gharama za Kitanzania isiyozidi bilioni 6. 

Walisisitiza kuwa lengo la kujengwa kwake ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.

Wakitoa taarifa kwa viongozi wa ulinzi, wataalamu waliojenga ukuta huo, walisema licha ya kufanikisha ujenzi huo, changamoto mbalimbali walikutana nazo ikiwemo hatari inayoukabili ukuta huo, kutokana na wachimbaji kulipua baruti, karibu na ukuta, hivyo kusababisha hatari za kuharibika haraka. Ugumu wengine walioupata ni uchimbaji katika maeneo yenye miamba.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...